EFD Kibaha ni changamoto

PrN-kazi

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2011
Posts
2,900
Reaction score
445
Nimeenda kwenye Duka Moja pale Mailimoja Kibaha kwa ajili ya kununua zawadi za watoto, baada kuchagua vitu nilivyokuwa nahitaji nakufanya malipo nimeshangaa kuona naomba RISITI na kunyimwa kibaya zaidi muuzaji ameanza kunitolea maneno makali akidai Serikali inawapigia kelele wakati TRA haiwapatii hizo EFD Machine ingawaje wanaziitaji.......kilichonishangaza zaidi ni pale muuzaji aliposema MKOA WA PWANI mzima hauna utaratibu wa kutoa RISITI.

TAFADHALI WAHUSIKA WA MAPATO BILASHAKA KUNA HAJA YA KUONGEZA KAZI KUANGALIA HUU MKOA
 
Ushawahi kuuza hata ICE cream?!

Ungekuwa ushawahi kufanya biashara bongo huu ....... usingeandika.
 
Labda wakala wa EFD hajalipwa na serikali sikivu na ya wanyonge. Hivyo hawezi kuendelea kuzisambaza ikuwa halipwi.
Kumbuka serikali hii haitaki hasara, inataka itengeneze hizo machine humu nchini kama zile meter za luku kisha walazimishe wafanye biashara wazinunue. Kwasasa bado zinaletwa kutoka nje nadhani wakala msambazaji hajalipwa ukiona hivyo, rais wetu anapenda pesa zetu wananchi yani kodi hasingeacha mkoa mzima bila EFD mashine.
Lakini Kumbuka wakizipata ukadai risiti yako.
 
Ushawahi kuuza hata ICE cream?!

Ungekuwa ushawahi kufanya biashara bongo huu ....... usingeandika.
Yeye ni mzalendo, usimuhukumu kuitafutia serikali yetu mapato.
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…