Elly B
JF-Expert Member
- Jan 11, 2011
- 1,194
- 906
Well,
As much as I would love to see this as busara ya Mzee, Lakini ningeomba Mheshimiwa E.Mtei ukane aliyosema Tundu Lissu kwa hoja. Kwamba useme kuwa aliyosema amemsingizia Mwalimu!
Tuambie kuwa siyo Hayati Mwalimu aliyesema Wazanzibari wakiamua kwa hiyari yao kuuhoji Muungano, hatawalazimisha kuendelea nao. Tuambie siyo yeye aliyewasimamisha kazi Wawakilishi wa Zanzibar wakiwemo Aboud Jumbe kienyeji bila hata kujali haki zao kisheria, kwa kuwa walihoji uhalali wa Muungano! Tuambie kuwa siyo Hayati Mwalimu aliyeandika baadaye kuwa "waliwakatalia hoja yao kwa nia njema kabisa"... Na kisha tuambie kama alisema na alifanya hayo, kwa kiongozi wa hadhi yake, tumsemeje! Kwamba alikuwa Mtakatifu sana? Kwamba alichowafanyia Wawakilishi wa Wazanzibari ni haki? Kwamba hakukiuka haki za wenzake? Au kwamba ni utamaduni tunaotaka kujijengea wa mtu tunayemheshimu akifanya upuuzi tuendelee kumwabudu na kumsifia!
Mzee Mtei hii nchi inabadilika! Na pamoja na kupenda kwangu kuwaheshimu wazee lakini nashindwa kulifumbia macho swala la kupotoka kwa uadilifu katika taifa kulikoasisiwa na Waanzilishi wa Taifa, upotofu ambao umekuwa ukirithishwa kwa vizazi vilivyofuatia na kupelekea kufikia hali ya sasa ambapo haki katika Taifa imepotea kabisa na Wananchi wamekuwa watumwa ndani ya nchi yao wenyewe!
Napenda mtuelewe tunapopigania haki za wanyonge walio wengi. Ambao kwa muda mrefu wa utawala wa haohao unaodhani ni wa kuabudiwa umewafanya dhalili na wageni kwenye nchi yao wenyewe, huku wenye fedha na wenye majina makubwa wakiwa juu ya sheria na kupanga mwelekeo wa taifa letu, huku wakijipangia madaraka na majukumu kama vile hii nchi ni mali yao binafsi!. Napenda ufahamu siyo Tundu Lissu, ni Wapenda mabadiliko. Na wapenda mabadiliko wote watakubaliana nami kuwa ili tufanikiwe, ni lazima kwanza tujue tulipoangukia. Kwa sasa nadhani ni sawa kabisa, ili kupata mwelekeo sahihi, tukubali pale kulipo na ukweli hata kama ukweli huo unakera na unawahusu marehemu tunaowapenda!
Vinginevyo nasikitika kuwa kwa hali ilivyo, kinyume kabisa na unavyofikiria nchi hii inawahitaji kina Tundu Lissu wengi zaidi. Watu ambao watasimamia ukweli kama msingi wa haki kwa wote, katika jamii huru inayoamini katika usawa na utu! Na nasisitiza usiwaambie wanaosema wanyamaze eti kwa sababu nyie hamkusema wakati wenu! Mzee wetu mpendwa, "Kila zama na kitabu chake"