Edward Ngoyai Lowassa VS Edward Moringe Sokoine

Sokoine kama alivyokuwa Mwalimu sio watu wa kulinganishwa na kiongozi yeyote kwa sasa nchi hii. Tuwaache wapumzike kwa amani huko waliko.
 
watu wengine bibi eeh, mtu akisema anasikia harufu ya madafu ya libya wanajidai hawamwelewi, akisema hapa anasikia harufu ya maembe je?
 
huu ni ubwege mwingine kwann usiwasilishe mada kwa Kiswahili? hawa ni watu waliokuja ktk mazingira tofauti hata angekuja Nyerere mpya leo angetofautiana na Nyerere wa 1922 - 1999, leo ni nguvu ya Soko hata Sokoine angekufa leo angekufa akiwa tajiri, Mtazame Kingunge Ngombale Mwiru je ni masikini? Rushwa ni system ya Taifa hili Sijamuona Josef Stalin wa Tanzania so Lowassa kosa lake ni kuwa mkweli kwa kuwajibika kwa Makosa ya wengine? au kwakuwa ni utaratibu mgeni ktk Taifa hili, Tusipambane na mtu TUJENGE SYSTEM KAMA MTU AKIIBA AU KULA RUSHWA MAMLAKA AU DOLA ITAMKATA KA sYLVIO BERLUSCON AU GAV. BLAGOVICH WA ILNOIS TUACHE POLITICAL MOTIVATION ZA KITOTO (CYNICISM)
 
PRESIDENT ELECT FEKI

Nyie mnasema kwamba mnaskia harufu ya pesa za Gaddafi. Kwa akili yenu fupi mmeshindwa kupambanua hoja mnakimbilia kuongelea upuuzi! Hoja hapa ni aina ya Kiongozi anaetufaa. Na mwanzo nimeandika kua kuanzia leo wale wote walioonyesha nia ya kwenda Magogoni ntawalinganisha na Viongozi wetu wa zamani na kwa kuanzia naanza na the two edwards. Sasa hapo cha ajabu ni nini?? Tatizo lenu nyie mnaempenda LAIGHWANAN so mkiona uzi wowote unaomkosoa mnakuja juu kama moshi wa kifuuu na kuacha kujadili hoja iliyopo mbele. Hata akina Membe, Magufuli, Sita, Migiro etc wote watafananishwa au huelewi maana ya "As from today, I will be comparing.... katika ile para ya kwanza, Mkuu au Lugha gongana????
 
WILDCARD

Umesema kwamba Nyerere na Sokoine ni watu ambao si wakulinganishwa na viongozi wa sasa. naheshimu maoni yako but naamini sio kila Mtanzania ni FISADI mf Marehemu Daud Mwakawago alikua mtu safi kabisa na kamwe hakuwaza kujilibikizia mali na hata alipoacha utumishi akawa anashika mchuma ie daladala! Dr A.M. Shein ni kiongozi mwingine safi kabisa asiye na makuu wala tamaa na mchapakazi hodar, Salim A. Salim etc. Wapo wengi tu. Siamini kwamba kati ya waTZ 45M hakuna mwenye walau baadhi ya sifa za Sokoine na mwalimu
 
NCHI hii haijaanza kuwa tajiri leo wala jana. Infact, wanachoiba akina Lowasa leo ni kile alicholinda, kuhifadhi na kutengeneza Mwalimu na Sokoine walipokuwa madarakani. Wangeweza kutuibia sana tu wakati ule kwani WATANZANIA wengi tulikuwa mbumbumbu kabisa. Kuiba ni TABIA, ni HULKA. Mwalimu na Sokoine hawakuwa wezi.
 
Mwalimu na Sokoine mbali na kutokuwa wezi waliuchukia wizi na wezi. Waliweka na kusimamia sheria kali mno kwa vitendo hivi viovu. Walichukua hatua kila ilipobidi kwa wezi na wala rushwa. Uongozi wa kisiasa hawakuugeuza kuwa mtaji wa kuchuma mali kiharamu. Hii ndio tofauti ya Mwalimu na Sokoine na viongozi wengine.
 
kwa uhalisia uliopo mpaka sasa na muonekano wa kisiasa pamoja na ccm kujitahidi kuwarudisha viongozi wenye kashfa wa zamani kama Kinana (nyara za serikali),Zakia (Richmondul) na wengine ni dharihi wanataka wamsafishie njia Lo-RUSHWA
maana wote pamoja na katibu mkuu alihusika kwa njia moja au nyingine kuhusu Richmonduli so kumpata E.sokoine mwingine ni uamuzi wa watanzania wenyewe kupitia chama hicho cha CCM kwa mfano 1.walioko huko CCm kuwajibisha wote wanaohusika ktk ufisadi kwa pamoja then tutapata sokoine mwingine ndani ya CCM na tutasonga mbele lakini hili lina ugumu wake maana nani wa kuanzisha??? Raisi mwenyewe yupo kwenye list of shame waliyotaja CDM au kupitia upinzani hususani CDM ambacho kimeonekana kuleta changamoto watanzania tuamue kwa pamoja kuwa CDM chukua hatamu ya kuongoza nchi na ukiingia kwenye usukani basi mafisadi wote wachukuliwe hatua kali pia hilo linawezekana kama tu watanzania wataona nia na uhitaji wake maana watanzania bado wengi hawaoni hata umuhimu wa kura
 
WILDCARD

Ina maana kati ya watanzania Miloni 45 hakuna hata mmoja anaeuchukia ufisadi?
 
KISHALU

Tuna uhakika gani kwamba waliopo chadema nao si mafisadi au niseme tutajuaje kua wakipata nafasi hawawezi kufisadi maana wengine tunaishi nao mitaani na mienendo yao na kashfa zao hata walipokua shuleni na vyuoni tunazijua!!
 
WILDCARD

Spot on. Mkuu umenena UFISADI NI HULKA YA MTU
 
Edward Lowasa vs Edward Sokoine = J.k Nyerere vs J.k Mk.were
 

Huyu Hana Hoja ya msingi,na ametawaliwa na siasa za chadema badala ya utaifa kwanza.Msubirini JK aongee kisha mpate cha kuongea maana hamuwezi jenga hoja zenu ila lazima mpesti toka kwa vyama vikuu.
 
Maji na mafuta vyote ni vimiminika lakini havina tabia sawa kikemikali.


 

Bubu Msemaovyo natamani ningekuwa kizazi cha Moringe alipotea ndo kwanza nina 2yrs katuachia balaa la mafisadi kupigana vikumbo
 
nngu007 Mkuu! Nimeipenda sana hii post zako! Ningekuwa ninaiona kitufe cha LIKE hakika ningekuangushia Mkuu! CCM ni janga kwa Nchi yetu ila hakika mwisho wao waja!

Unasema @ the bottom right hakuna kitufe cha LIKE?
 
Wote walifanya kazi pammoja wakati fulani,na yasemekana Lowassa alikuwa ni mshauri wake Sokoine.Tusipoteze muda kujadili-: kulinganisha au kutofautisha au kuoanisha watu hao wawili.Wote walikuwa PM katika vipindi tofauti za tawala na mifumo tofauti.
 
MAKETE

Mkuu nakubaliana na wewe tumeachiwa mafisadi kibao
 
MOODUKE
"Maji na mafuta vyote ni vimiminika lakini havina sifa sawa vya vimiminika".. Mkuu, nimeipenda sana hii inaonekana Sokoine na lowasa ni sawa na MAFUTA na MAJI!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…