Edward Lowassa special thread

SAFARI ya matumaini kuelekea ikulu imewadia. Tulianza pamoja kwa umoja na tutamaliza pamoja kwa umoja. Tumaini letu ni kwa mgombea mwenye maamuzi. Njoooni hapa wana LOWASSA tupeane update kwa yanayojili tangu sasa mpaka magogoni.

Safari ya huzuni imeshakaribia endeleeni kujipa moyo .
VOTE FOR UKAWA.
 

"........nawaomba maaskofu wote,masheikh wote,na vijana wote.......wanaotaka fedha za haraka haraka........wamfuate EDWARD NGOYAI LOWASA atawapatia! Lakini hana sifa ya kuwa RAIS.............." -Dc Makonda.
 
Hakuna cha matumaini wala nini wewe sema tu njia uliyoamua kusakia tonge.
 

Acha kufiri kwa makalio, ulipewa kichwa uitumie kufiri
. km unadhani hela zake zitakusaidia umwombe kibarua za kuchunga ng'ombe wake. Nchi hii ina watu wengi wazalendo, hivyo hakuna haja ya kuwarudia wenye tuhuma za ufisadi hata km hawajathibitika na tuhuma hizo lkn ujue kuwa wenye mamlaka za kuchukua hatua za kuthibitisha ukweli na uongo huo walikaa kimya kwa sabb wanazo jua wao.
 
"........nawaomba maaskofu wote,masheikh wote,na vijana wote.......wanaotaka fedha za haraka haraka........wamfuate EDWARD NGOYAI LOWASA atawapatia! Lakini hana sifa ya kuwa RAIS.............." -Dc Makonda.

Mh Dc nakuongezea pia kuwa ikiwa Lowasa atachaguliwa kuwa mgombea urais Mwisho au kifo cha cc ndio kitawadia. Kweli Lowasa anataka kwenda ikulu kwa masilah binafsi tu nakama ccm hawatolitambuwa hilo ndio najuwa utakuwa mwisho wao. All tanzanian 2lio na mapenz mema na hili taifa tuungane kusema NO BIG NO TO LOWASA. Wasomi na wazee wataifa hili simameni nakumwambia hatufai ku2ongoza ila anafaa kuongoza familia yake na ng'ombe zake zaid ya 800. Imetosha.
 
Nilimis sana habari za karamagi,kumbe yupo ktk vinyanganyiro vya siasa za tz?wapi msabaha?
 
Macho ya wa Tanzania hayapo kwa Lowasa yapo kwa Mungu na chama cha ccm, naimani hata mgomba unaweza simamishwa na ukatuongoza ila Lowasa, taifa litakatika vipande viwili kama sio vinne. MaJeshi yote ya ulinzi, usalama wataifa na idara zake zote zinazofanya kazi kwa siri, pamoja na watanzania na wazee wenye utumishi ulio tukuka öneni dam na visas vitakavyo enda kufanywa na Lowasa namchukue hatu mapema kumzima. Huu niwakati wakumshughulikia kwanjia zote, hewani, nchi kavu,majini na hata milimani. Shughulikeni naye ili ajuwe yeye na wenzake kuwa tahasisi ya urais hainunuliwa kwa fedha wala kwa dhahabu. Idara zetu zinauwezo kama wa cia kumzima nakumpoteza kama Mrema!
 
Lowasa ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa kuiongoza nchi hii tunamuitaji ili atutoe tongotongo kwenye macho yetu wakati umefika wtz kuwa natumaini jipya tusidanganywe na tuhuma za kipuuzi lowasa ni kiongozi mwenye kila sifa kwenye nchi mwenye uwezo na uzoefu wa kiuongozi lowasa anatosha tusifanye kosa wanaccm tunaijua kazi
Kubwa aliyoifanyia nchi hii kama kiongozi ndani Chama na ndani ya serikali lowasa anatutosha wanaccm na watz kwa ujumla tumpe kijiti aendeleze Yale yote mazurii atakayo yaacha mh. Jakaya lowasa atosha 2015 tumpe uongozi atuletee maendeleo
 

 
Nikikumbuka alivyoshupalia dili la kutengeneza mvua, sina hamu na ubunifu pamoja na mbinu zake atumiazo kufanya kazi.
 
Kitu ambacho mnatakiwa kujua kwa sasa ni UTAWALA WA CCM HAUTAKIWI TENA
 
safari ya matumaini kuelekea ikulu imewadia. Tulianza pamoja kwa umoja na tutamaliza pamoja kwa umoja. Tumaini letu ni kwa mgombea mwenye maamuzi. Njoooni hapa wana lowassa tupeane update kwa yanayojili tangu sasa mpaka magogoni.
thread ya vitoto vya fisadi e.l!
 
Tatizo siyo Lowasa bali shida kuu ni CCM haifai.
Hata ungekua msafi vipi ukiwa ccm haufai kutuongoza.SHIDA NI MFUMO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…