Edward Lowassa na Wanaomzunguka

"If you want to judge others, start yourself"
Think big and ask yourself how good you are than others?

rangau I.q yako ni kubwa mno!
wapo watu wenye akili nzito,na nyepesi kimaamuzi!
 
Last edited by a moderator:
Nyie lieni tu lakini watanzania wameshasema,awe mchafu awe msafi wameshamtaka mtu wao,matope yote aliyopakwa lowassa miaka nane iliyopita sasa amesafishwa na wale wale waliomchafuwa
 
Hii ni kawaida kutokea hasa ktk nchi za Afrika.Mmesahau Rais Jacob Zuma Wa South Afrika,alituhumiwa kukwiba hela pamoja na uasherati, Hadi akatimuliwa umakamu Wa Rais na Rais Wa wakati ule bwana Thabo Mbeki?.Mfano mwingine ni Kenya,Rais Uhuru Kenyata alishtakiwa ICC kwa kushiriki kikamilifu ktk mauaji wakati Wa uchaguzi 2007, Lakini Leo ndie Rais Wa Kenya, sasa ajabu iko wapi kwetu sisi watanzania kuongozwa na Edward Lowasa? Kwani sisi tumestaarabika kuliko hao wenzetu?
 
Tatizo la Lowasa ni nyota,yani hata muongee nini Ikulu ni ya Lowasa mungu ndo ameamua hivyo
 
Sio tu wanaomzunguka hata yeye mwenyewe ni mashaka matupu
 
Alienda kuleta wawekezaji kwenye mvua ya kutengeneza Thailand, ili Mtera yajae maji, umeme uzalishwe... na pia barabara ya Bagamoyo/Ali Hassan Mwinyi aliifanya njia tatu, foleni ikapungua....; alifinyanga kama udongo shule za kata...na mwisho alijiuzulu kwa kuwa akina Sitta walikuwa wanamuonea gele na uwaziri mkuu......JUST IMAGINE hayo ndo maamuzi magumu hadi inakuwa kete ya kupata Urais!!!!
 
"If you want to judge others, start yourself"
Think big and ask yourself how good you are than others?

Mheshimiwa Rangau, tumia kiswahili ili ueleweke vema na wana jukwaa wote. Kiingereza ilichoandika hakipo sahihi.

Sina chuki na Edward Lowassa. Nina shida na nafasi anayoitaka kwa sababu hafai.
 
Kule China mafisadi wanapigwa risasi bila kujali vyeo vyao.
Kuwa fisadi ni uamuzi mgumu. Maamuzi magumu ya Lowassa anayo jinasibu nayo zaidi ya ufisadi siyaoni.
 
Anaposema anauchukia umaskini anamanisha kabisa. Ni tajiri kupindukia.
Sijui wangapi wanaelewa kwamba kawa tajiri at our expense! Sehemu ya kubwa ya umaskini wetu ni matokeo ya ufisadi wa watu kama yeye.
Akiwa Rais, tutatoka kwenye umaskini hadi ufukara wa kutupwa.
 
ameisha waambia mlete ushahidi wapi kala rushwa na ningapi na nani kampa. sasa mbona hamtaki kuelewea. kama hamna ushahidi mnatuandikia ngonjela na hadithi za kusadikika tu.


Nachelea kusema kwamba, Edward Lowassa amezungukwa na watu wanaotiliwa shaka na taifa. Wengi wao ni watuhumiwa wa ukiukwaji wa maadili ambayo ni msingi muhimu wa uongozi. Katika mazingira kama haya, Edward Lowassa hawezi kukwepa kuitwa si mwadilifu ikiwa rafiki zake si waadilifu.

Nitaendela........[/QUOTE]
 
mimi nilikwenda kumsikiliza wala sio mshabiki wake na sikuwa nimehongwa kwa hiyo hoja ya kwamba wote waliokwenda kumuona wamenunuliwa sio kweli na sio vizuri kujenga hoja kwa misingi ya uzushi na uongo
 
mimi nilikwenda kumsikiliza wala sio mshabiki wake na sikuwa nimehongwa kwa hiyo hoja ya kwamba wote waliokwenda kumuona wamenunuliwa sio kweli na sio vizuri kujenga hoja kwa misingi ya uzushi na uongo

Ndugu gnassingbe,

Pole sana. Nadhani nimekukwaza kwa kuandika juu ya umpendaye. Bahati mbaya sana suala la urais ni zito na linagusa maisha ya kila mtanzania. Mimi kama mtanzania ni wajibu wa kutoa maoni yangu juu ya rais ajaye. Hii si dhambi.

Naomba usome vizuri andiko langu. Sijasema Edward Lowassa anawalipa pesa wanaohudhuria mikutano yake. Lakini mazingira ya mikutano yake yanapelekea watu waamini hivyo. Huyu jamaa hana hoja nzito lakini watu wanashangilia kupita kiasi. Hapa pana walakini. Inaewezekana watu wanalipwa kushangilia au upeo wao wa kuchambua mambo ni mdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…