ECL: Barca, Liver, Bayern ktk hatihati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ECL: Barca, Liver, Bayern ktk hatihati

Discussion in 'Sports' started by AljuniorTz, Nov 23, 2009.

 1. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  LIGI ya Mabingwa Ulaya inaendelea Juma4 na Juma5 huku timu tatu kubwa na maarufu zikiwa katika hatari ya kuondolewa katika michuano hiyo mapema.

  Timu hizo, bingwa mtetezi Barcelona, Liverpool ambao wameshinda taji hilo mara tano na Bayern Munich ambao ni washindi mara nne zinakabiliwa na mtihani mgumu.

  Mabingwa Barcelona wanaikaribisha Inter ikiwa naye mshambuliaji wao wa zamani, Samuel Eto’o katika mchezo ambao wakishindwa huku wawakilishi wa Russia, Rubin Kazan wakiwashinda jirani zao, Dynamo Kiev, watakuwa wamevuliwa ubingwa.

  Washindi mara tano, Liverpool wana mchezo dhidi ya wageni na vibonde, Debrecen ya Hungary, lakini wanaweza kuondolewa endapo Fiorentina watawafunga Olympique Lyon nyumbani.

  Hali kadhalika, Bayern Munich ambao wanacheza na Maccabi Haifa wa Israel ambao hawana pointi hadi sasa, wanaweza kutupwa nje ya michuano hiyo hata wakishinda endapo Juventus watailaza Girondins Bordeaux , ambao wamefuzu na kuingia hatua ya 16 bora.

  Katika mechi nyingine Arsenal itaungana na Lyon, Bordeaux, Chelsea, Porto, Manchester United na Sevilla kwenye hatua hiyo huku AC Milan na Real Madrid, pia zikiwa na nafasi hiyo ya kufuzu.

  Ziara ya Inter kwa Barcelona kwenye Uwanja wa Nou Camp leo Kundi F ndio unaosubiriwa na wengi.

  Inter wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi sita baada ya ushindi dhidi ya Dynamo Kiev wiki mbili zilizopita, mbele ya Rubin Kazan na Barcelona, wenye pointi pungufu.......


  Source: Mwananchi


  Je, watafuzu???
   
Loading...