Bongo yetu ndy ilivyo, watu wanaandaa seminar kwa ajili ya ulaji tu. Aug nilikuwa sehem kwenye seminar ya siku saba (mm si mfanyakazi wa serikali, tulialikwa tu kama wadau) Jumla ya washiriki walikuwa 40 kati ya 50 walioalikwa, kwa ufukunyuku wangu nikadadisi mpaka nikapata bajeti halisi ya seminar hiyo, kam 285,000,000/= mia mbili themanini na tano millioni! Posho walikuwa wanatoa laki2/day, chakula malazi na nauli jumla haizidi 400,000/= kwa siku kwa kila mshiriki! Hesabu za mwisho nazo nilibahatika kuziona-Hakuna pesa iliyobaki, na idadi ya washiriki waliandika 49 (hakuhudhuria mmoja tu!).....wakati kuna waalimu wanalipwa 210,000/=pm!!!