Ebu Ichukuwe hii na Uielewe Itakusaidia

Ebu Ichukuwe hii na Uielewe Itakusaidia

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
3,930
Reaction score
4,939
KWANINI MWANAUME UMPENDE MKEO..?

Katika Maandiko matakatifu Mwanamke anaagizwa Kumtii mumewe na mwanaume kumpenda mke wake.. Efeso 5 :22 ,24.

Ni Kwanini Mwanamke anatakiwa amtii mume wake? Ina maana Yeye hatakiwi kumpenda? La hasha..! Atawezaje Kumtii bila ya kumpenda? Maana Utii usiotokana na Upendo si Utii Bali ni Hofu au kutimiza wajibu naweza kusema ni utumwa.

Na ni Kwanini Mwanaume anaagizwa kumpenda mkewe? Ina maana Yeye hatakiwi kumsikiliza mke wake? Hatakiwi kukosolewa? Yeye anafahamu kila Kitu kwa kuwa ni kichwa? La hasha..! Hata Yeye pia anatakiwa kumsikiliza, kushauriwa na kukosolewa pale anapoenda kinyume (japo hili linatikwa kufanyika kwa Hekima).

Wapo wanaume wasiowashilikisha mambo yao wake zao wala hawataki kushauriwa kwa kujiona kuwa wao ndio viongozi wa familia, Lakini kwa kufanya hivyo wanajikuta wakikaribisha Maafa makubwa katika Ndoa zao.

Sasa ni Kwanini Mwanamke anatakiwa kutii na mwanaume kupenda? Hii ni kutokana na sababu za kisaikolojia (kimaumbile) baina ya mwanaume na mwanamke.

Mwanaume hujisikia vizuri zaidi pale ambapo ataona mke wake anafuata kile ambacho anamuelekeza kufanya maana ni Kiongozi, na Hakuna Uongozi Kama Hakuna anayeongozwa.

Wakati Mwanamke Yeye kwa asili hujisikia vizuri Sana Kama akioneshwa kujaliwa na mume wake, anaweza akawa Tayari kukosa vyote Lakini si Upendo.

Ninaposema upendo sizungumzii PESA maana wanaume wengi wanajua pesa Pekee ndio inayoonesha Uanaume wao Lakini Sivyo. Upendo ni zaidi ya hapo.

Mwanamke anapenda kusikia neno Nakupenda Mara kwa Mara anaweza asisikie Kiu ya kunywa maji siku nzima akastahimili Lakini si Kiu ya kusikia anapendwa kutoka kwa mwanaume wake. (Mwanaume Chukua Hii).

Mwanamke anapenda kusifiwa kwa maneno mazuri kuwa amepemdeza jinsi alivyovyaa, jinsi alivyosuka nk, Sasa akiona wewe humsifii basi atatafuta watu wa nje wa kumsifia.

Ndipo hapo utaona kapiga Ka [HASHTAG]#selfie[/HASHTAG] Halafu katupia facebook Ili apate comments za watu maana ndani hazipati (Ni hatari mkeo kusifiwa na watu wa nje ikiwa wewe unajifanya Huna Habari) .

Mwanamke anapenda kuona ukimtambulisha kwa marafiki zako, unapata muda wa kutoka naye bila kusahau kumletea zawadi za hapa na pale yaan hata pipi ya kijiti inatosha Sana kumfanya ajisikie furaha sio Mpaka umnunulie gari.

Hayo niliyoeleza hapo ni mambo machache yanayoelezea nini maana ya upendo kwa mwanamke. Sasa pale ambapo atakosa kuona upendo kwa mwanaume usitegemee kuona Utii.

Hapo ndipo kiburi, malumbano yanapoinuka na tukiyaona hayo tunasema mwanamke alikuwa anaficha makucha yake kabla hajaolewa.

Tatizo sio makucha, tatizo haoni upendo alioutarajia Kupata Kabla ya ndoa ,Kama ukiona ametoa makucha basi wembe wa kukata makucha hayo si kumtukana, kumpiga au kumtafutia nyumba ndogo, Bali ni Kuongeza Upendo.

Mwanaume, Nguvu ile ile uliyotumia kumtongoza (kumshawishi awe na wewe) ndio hiyo hiyo uitumie Sasa kipindi Upo naye.. Na hapo ndoa yako Itakuwa ni Paradiso Ndogo (small Heaven).

#Mwaume_mpende_mkeo.


Sent from my HUAWEI P6-U06 using JamiiForums mobile app
 
Jamaa sijui kwa nini watu wanamuovertake!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom