Ebola yatinga Marekani

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Mtu mmoja amegundulika kuwa na dalili na vimelea vya ebola Jimboni Texas Marekani. Mtu huyo ambaye alisafiri kutoka Liberia hadi Marekani kwa sasa ametengwa kwenye chumba maalum kwa matibabu na pia kudhibiti uwezekano wa maambukizo.



CHANZO: BBC
 

sio mbaya kwa vile walivitengeneza wao nadhani hata dawa yake wanayo, atapona tu msijali.
 
Sasa Dawa itapatikana

Asante Mungu kwa kuupeleka huu ugonjwa huko kwao

Cheza na Propaganda za wamarekani, mnahakika kweli anaumwa? Janja tu hiyo ni jasusi mmojawapo kaigiza katiwa kwenye karantini basi ili watu wajitangaze
 
Cheza na Propaganda za wamarekani, mnahakika kweli anaumwa? Janja tu hiyo ni jasusi mmojawapo kaigiza katiwa kwenye karantini basi ili watu wajitangaze

basi ni kheri mkuu, manake atasababisha watoe dawa.
 
Vizuri.., wiki hii haiishi utasikia kuna dawa imegunduliwa..
 
"Ebola ni ugonjwa hatari wa virusi kuwahi kuzuka duniani".

Hee.!!!!
Kuliko ukimwi.????
 
Ugonjwa wa ebola ambao umesababisha vifo vya watu 3,000 Magharibi umeripotiwa kutua nchini Marekani katika mji wa Dallas,Texas.
 
japo hujaweka chanzo,acha tu niseme asante yesu kwa kusikiliza maombi yetu sisi maskini wa bara la giza.haleluya.
 
japo hujaweka chanzo acha niseme asante yesu kwa kusikiliza maombi yetu sisi maskini wa bara la giza.haleluya.

kwahiyo uliombea huo ugonjwa ufike Marekani? akili yako inafanana na kile kinyago cha kizungu kilichosurubiwa.
 
kwahiyo uliombea huo ugonjwa ufike Marekani? akili yako inafanana na kile kinyago cha kizungu kilichosurubiwa.

jamaa kasema kweli ispowaumiza wao hawatoi dawa ya kweli wanafanya mtaji Afrika
 
Mliberia aliyekuwa Liberia alirudi US wiki ya tatu ya september anakoishi na huo ugonjwa, mwanzoni alikuwa fit kabisa baada ya siku chache akaanza kuumwa. Akaenda hospital na kutibiwa lakini hakuchunguzwa kama ana Ebola. Siku tatu baadaye akawa mahututi na kupelekwa hospital na ambulance ndipo alipofanyiwa uchunguzi na kukutwa ni muathirika wa huo ugonjwa.

umeingiaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…