Daktari wa Marekani aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huko katika hospitali ya ya mjini Newyork.
Dr Craig Spencer ambaye ni mmoja kati ya madaktari wasio na mipaka alianza kujisikia maumivu na homa siku chache tu baada ya kurejea Marekani akitokea Afrika Magharibi.
Siku ya Alhamisi wiki hii Craig alipelekwa hospitali kwaajili ya vipimo na kisha akatengwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Meya wa mji wa Newyork Bill de Blasio amesema watu hawapaswi kuwa na hofu kwani hatua zote mhimu zilifuatwa katika kumchunguza Dr.Craig na hadi alipobainika kuwa na maambukizi hayo.
Kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa Dr.Craig kunaongeza idadi ya waliobainika kuwa na ugonjwa huo nchini Marekani kutoka watatu na kufikia wagonjwa wanne.
Nami nasema bora hawa wenzetu US tuko nao pamoja katika shida na raha kiasi cha kuhatarisha maisha yao, ila kunanchi moja inajipambanua kama nchi kubwa lakin kwenye majanga inakuwa mtazamaji tu, sasa ndo ukubwa gani huo?! Yaan wao badala ya kushughulika na majanga yanayokabiri dunia wao wamekalia kujionyesha kijeshi na kujisifu wana miguvu, sasa miguvu gani hiyo haisaidii wanyonge.