EAC Kuipeleka shimoni Tanzania

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
236
Ndugu wadau,

Tumekuwa tukisikia habari tofauti tofauti kuhusu Jumuia ya Africa Mashariki, lakini habari hizi mara nyingi hutegemea jitihada za mwananchi mwenyewe katika kuzitafuta maana hakuna mfumo rasmi wa kuwaeleza na kuwaandaa watanzania (Wanainchi wa kawaida) katika kukabili changamoto na kutumia fursa zinazoweza kujitokeza kupitia shirikisho hili. Ikumbukwe pia wenye uwezo wa kutumia hii mitandao ya Internet ni wachache sana.

Hoja yangu ni kwamba wananchi wa kawaida wa Tanzania hawashirikishwi na hawaandaliwi ipasavyo katika mambo haya ya shirikisho. Yapo mambo kadhaa ambayo yameshaafikiwa na jumuiya hii lakini watanzania walio wengi hawana taarifa nayo.

Maswli yangu ni:
1. Jumuiya hii ni kwa maslahi ya wananchi wote au ni kwa viongozi pekee?

2. Hoja ya kwamba watanzania wanahofu na Jumuia hii kwakuwa watanyang'anywa ardhi yao imetoka wapi kwasababu hakuna mijadala ya wazi kuhusu jambo hili hapa Tanzania sasa aliyetoa maoni hayo alitumwa na nani?
3. Je katika eneo unaloishi au unalofanyia kazi unadhani watu wanauelewa juu ya jambo hili?
 

Attachments

  • Amended Treaty for the Establishment of EAC.pdf
    670.9 KB · Views: 36
Back
Top Bottom