E- learning kwa taasisi za elimu Tanzania

E- learning kwa taasisi za elimu Tanzania

Joined
Mar 31, 2020
Posts
67
Reaction score
59
Wanajamvi habarini za mihangaiko?

Najuwa wengi wenu mko vizuri mkiendelea kumuomba mungu na kuchukua tahadhari zote za gonwa hili la Covid 19, tuayaache hayo kwa muda ambapo janga hili limeingia duniani nchi nyingi hasa za dunia ya tatu zimepatwa na taabu sana.

Kwenye suala la wanafunzi kuendele na masomo yao, mfano Tanzania shule na vyuo vilifungwa kwa dharura kwa mda usiojulikana maswali ya kujiuliza je gonjwa hili likiendelea kwa mwaka mmoja shule na vyuo vitaendelea kufungwa?

Hapo ndipo tunapokuja kujua umuhimu wa E-learning. Kiukweli nimeshikwa na bumbuwazi hata vyuo kutojiwekea mikakati ya kujifunza kwa njia hii ambayo ni technolojia huhimu ili kwenda na mahitaji ya dunia. Wanafunzi wengi waliokuwa vyuo vya nje waliporejea kwa sababu ya nchi husika kuathiriwa vibaya na korona waliendelea na masomo yao kama kawaida kwa mfumo wa E-learning. Je, vyuo vyetu vimeshindwa hill?

Kwa upande wa mashule kiukweli nimeona juhudi mbalimbali zimechukuliwa. Mfano, SHULE YA SEKONDARI BARIADI ILIYOKO MKOANI SIMIYU, imeonyesha mfano wa kuigwa kwani kabla ya kufunga shule mkuu wa shule hiyo SIMBA ALLY MASOUD alikuwa ameshaandaa mafunzo ya aina hiyo na kuwasisitiza wanafunzi kuingia na kupata maswali na kuuliza maswali mbalimbali ambayo yanakuwa yamewekwa na waalimu katika web ya shule na group WhatsApp.

Waalimu wanaweza kuunda magroup ya WhatsApp mbalimbali yakiwahusisha wanafunzi wao ili waeze kupa hata kitu kidogo. Najua sio wote watakuwa na access ya kuingia kwenye mitandao ila yaweza kuwa chachu ya kufikia malengo ya baadaye.

E-LEARNING INAWEZEKANA MWALIMU TIMIZA WAJIBU WAKO.
 
hiyo E learning ikitumika ndio itaizika rasmi elimu yetu, wanafunzi wengi wametoka familia masikini hawana uwezo , darasani tu, wanafunzi hawaelewi, huko kwenye mtandao si ndio hatar zaidi
 
Ni vizuri ila hii njia ingefaa zaidi kwa watu wa vyuo hawa madogo wataanza vitu hovyo huko .com,kwa vyuo au secondary ni aibu kutokuwa na hii njia,hivi out univesrty wanefunga nao?
 
Ni vizuri ila hii njia ingefaa zaidi kwa watu wa vyuo hawa madogo wataanza vitu hovyo huko .com,kwa vyuo au secondary ni aibu kutokuwa na hii njia,hivi out univesrty wanefunga nao?
Mkuu

Bado nawazaga kitu

Mimi tokea Darasa la sita nilianza kumiliki simu... Lakin haikunizuia kufaulu vizuri Darasa la Saba.. Kuanzia form one had form four Nilikuwa Nina simu Japo nilisoma day lakini haikunizuia kufaulu vizuri kidato cha nne.

Kidato cha tano ilikuwa government school na ni boarding lkn Nilikuwa na simu toka siku ya kwanza mpaka namaliza form six na nikaulu vizuri tu

Je, hakuna namna ambayo vijana wataruhusiwa kutuma simu mashuleni bila kuathiri Masomo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Next week shule yetu itaanza 'trimester' mpya.
Tutafundisha kupitia Google classroom na lecture zitakua zinatumia meet.
Ni njia nzuri kujifunzia.

Na uzuri ni kwamba teknolojia zote hizo zinatolewa bure na Google. Na endapo taasisi imejiunga napi GSuite, zinaweza kuwa integrated vema kabisa.

Ni ya level ipi shule yenu, if you don't mind.
 
Na uzuri ni kwamba teknolojia zote hizo zinatolewa bure na Google. Na endapo taasisi imejiunga napi GSuite, zinaweza kuwa integrated vema kabisa.

Ni ya level ipi shule yenu, if you don't mind.
Kuanzia chekechea (nursery) hadi high school (class 13). Tunatumia mtaala wa Cambridge
 
Back
Top Bottom