Duuh usiombe ikukute maana......

Habari zenu wanajamvi..
salam hizi zinafatana na shukrani kwa MUNGU. Jana ndio nilirudi hewani baada ya tukio la juzi lililotokea maeneo ya beach.
ilikua hivi
nimetoka na washikaji naenda beach, Mtoto wa kike akapiga sim Stevoh unaenda beach nisubiri twende wote. Tukafika beach tumekaa kumbe bana jua linawahi kuingia kuja kushtuka mda umeisha duuh ikabidi nianze kuwawahi masela ile tunakaribia kufika si wakatokea wanaoitwa Vibaka wa3 wakatuweka chini ya ulinzi. Mtu mzima nikaambiwa kaa chini nikamcheki boya wangu kashika kisu kihasarahasara ile namalizia kumyang'anya akamwita mwenzake "oyaa huyu Mmbishi" ikabidi niachie kisu wakati huo wote tumejikata wakati wa purukushani. Ikabidi niwe mpole wakachukua simu yangu KIPENZI "NOKIA E51" ambayo ilikua inanisaidia kuperuzi JF na ku"Google"
yani leo ndo nimepata simu nyingine ikanibidi niadisie mkasa sasa ivi nauguza kidonda changu na machungu ya simu yangu. Omba Mungu lisikukute kuwekwa chini na Vibaka maana .......

pole mkuu jama noma ikorudisha maendeleo nyuma.
 
Back
Top Bottom