Duniani kuna mambo

MANILABHONA

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2015
Posts
462
Reaction score
351
Wakati watu wakiendelea kudai demokrasia na wenye busara wakielimisha umuhimu wa uongozi kuwa na ukomo kwa mustakabali wa maendeleo ya wananchi wao, hivi karibuni kumejitokeza watu tena ndani ya nchi hii eti wanaanzisha kampeni ya kiongozi fulani aendelee na madaraka/ utawala hata muda wake utakapomalizika. Huo ni uroho wa madaraka-wendawazimu kama alivyowahi kusema baba wa Taifa. Nawashauri wasirudie tena kutoa maneno ya namna hiyo. Tanzania si Rwanda wala Uganda, sisi tuna ustaarabu wetu. Hatutaki yaliyowakuta wenzetu na sisi yatukute. komeni komeni mshindwe na mlegee. Msitusababishie matatizo sie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…