Dunia na mambo yake

Dunia na mambo yake

Amani Dimile

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
243
Reaction score
399
Nimeonja vitu vyote vitamu lakini sijaona kitu kitamu kama kuwa na afya njema, hivyo jitahidi ujitahidivyo lakini usisahau kutunza afya yako. Nimeonja mengi yaliyo machungu, lakini sijaona kitu kichungu kama kupuuzwa na mtu ambae unamjali sana. Nilibeba vitu vyote viwili, chuma na jiwe lakini sijaona kitu kizito kama kuwa na madeni. Tena kuwa na madeni kipindi ambapo mfukoni huna kitu.

Nimeona vingi vizuri, lakini sijaona kitu kizuri kama kuwa na furaha dhidi ya watu wanaokupenda. Nimeishi sana kwenye huzuni, lakini hakuna huzuni kubwa kama kukumbuka maisha ya zamani uliyokuwa na furaha dhidi ya watu ambao hawapo tena kwenye dunia hii. Nilipewa nafasi ya kushukuru, lakini sikuona kitu cha kushukuru kama kumshukuru Mungu kuwa hai hadi leo hii, maana wapo wenzangu wengi niliokua nao pamoja lakini hivi sasa tayari nishawazika.

Nimehisi vitu vingi vyenye maumivu, lakini sijaona kitu chenye maumivu makali kama machozi. Maana machozi huzungumza yale yote ambayo moyo umeshindwa kuongea. Nilipewa vyote viwili asali na sukari, lakini hakuna kitu kizuri nilichokipenda kama kuthaminiwa na watu waliokuzunguka.

Hata hivyo nimeona vitu vingi vinavyouma, lakini sijaona kitu kinachouma kama kuchukiwa na wanadamu tena kutokana na maneno ya kuambiwa yasiyo na ukweli.

Imeandikwa na AMANI DIMILE

Screenshot_20210919-093520.jpg


Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
MIMI afya yangu ndio mtaji wangu, kijana katika vitu vyote jali sana afya yako
 
Back
Top Bottom