Dunia mapito

Dunia mapito

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Posts
7,479
Reaction score
5,161
Hamjambo?Haya ni mapito yangu.......niliyapita nikiwa binti mdogo sana (soon after high school)

Ni kama miaka 5 au 6 iliyopita nilipokutana na huyu kijana kutoka kanda ya ziwa kwa jila X (sio jina lake halisi). Tulianza mahusiano na huyu kijana. Mwanzoni kila mtu hakuwa that serious lakini tulivyokuwa tukisonga mbele kila mmoja wetu hasa mimi (sina uhakika na mwenzangu ila alijesemea tu) nilijikuta nikimpenda na kuhitaji kuwa karibu nae. Kijana huyu wivu ulimzidi sana, akawa kila mtu wa kiume kwenye phone book yangu anamhisi ni boyfriend wangu, aliwapigia simu rafiki zangu hao wa kawaida na kuwatukana. Ilifikia kipindi hadi akawa anaamua hadi kuchunguza namba ya simu ya baba yangu mzazi kkama ni kweli ni ya baba au ni jina tu limesaviwa. Hakuishia hapo alianza kunipa kipigo heavy hata kwa pale ambapo sikuwa na kosa na kosa alilitengeneza mwenyewe kwa kujifanya mwanaume anatuma meseji kwangu kwa namba nyingine. then haraka haraka anakuja na kuiangalia simu yangu na akiikuta hiyo meseji analazimisha nimjibu kuwa huyo mwanaume ni nani nikikosa jibu kwa kusema simjui mtumaji ananipiga. Alilazimisha kujitambulisha kwa mama yangu (alippiga simu mimi nikiwa sijui) na kumwambia mama eti yeye ni boyfriend wangu na kuanzia hapo daily akawa anampigia maza (nilichukia sana kwa kulazimisha kwake but sikuwa na jinsi). Nilipokuwa nikimsema why anafanya hivyo alilalamika eti simpendi ndio maana sitaki aongee na maza.

Alizidi kunionea wivu hadi niliamua kuacha kazi niliyokuwa nafanya kwani kila siku alikuwa anazusha jipya. Maisha yangu hayakuwa tena ya amani nilikuwa mtu wa kulia sana kiasi kwamba nilianzwa na tatizo la moyo kwenda mbio kila wakati.

Ilifikia mahali na mimi niliamua kwamba akinipiga tu lazima nilipize kwa kumrudishia. Kweli nilikuwa nafanya hivyo. Siku moja wakati ananipiga (kwa kosa ambalo hata sikulifanya aliamua tu kutunga akijitetea ati marafiki (tribe mate) wake ndio wamemwambia) niliamua kukibana kidole chake kwa meno tena kwa nguvu zote hali iliyomsababishia ulemavu wa kidole hadi leo. Kila nikumbukapo hili tukio roho inaniuma sana......kumsababishia ulemavu mtu?? ee Mungu unisamehe kwa hili lakini sikuwa na namna ya kujitetea kwani ukweli huyu mkaka alikuwa ananipiga sana.

Ilifikia hatua nikawa jeuri, alipokuwa akianza wivu wake wa from no where nikawa namjibu mbovu (alikuwa akinikkera sana kwa mambo yake ya kutunga). Nilikuwa namjibu jeuri si kwa maana kwamba sikumpenda bali nilichoshwa na ugomvi wa kila mara uliosababishwa na wivu wake.

Nilikuwa nashindwa kumuacha kwa sababu nilimpenda na nilijua siku moja angebadilika, lakini haikuwa hivyo. Nilishinda nikilia kila siku nisijue niamue lipi. Kila siku zilivyozidi ndivyo kaka huyu (ambae kwa sasa ni mme wa mtu) alivyozidi kuwa na roho mbaya kwangu na kuniangushia kipigo japo tulikuwa marafiki tu na si mke na mume. Mama yangu alinionya sana kuhusu mwenendo wa huu uhusiano lakini sikumsikiliza na nilimuona kama mtu anayeniingilia kwenye maisha yangu.

Hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho, uhusiano huu ulivunjika siku moja kwa sababu hizi hizi za kugombana kusiko kuwa na mwisho. Inshort, sababu kubwa za wivu wake ilikuwa ni kutojiamini kwake, yeye alinituhumu kwamba mimi sikuwa mwaminifu kitu ambacho nakiri kwa mwenyezi Mungu haikuwa hivyo. Kipindi chote pamoja na vipigo hivyo sikuwahi kumsaliti.

Kuhusu kilema cha kidole, naomba msamaha kwake(nilishamuomba japo hakujibu kama ndio au hapana) na kwa Mungu wangu. Najua akikiona atakuwa ananikumbuka lakini hata mimi nikiona mtu wa kabila lake nakumbuka vipigo vyake visivyokuwa na ubinadamu ndani yake bali unyama. Lingine, namtakia kila la heri katika ndoa yake, asije kufanya kama alichokuwa akinifanyia kunipiga kama punda. Akumbuke mke hapigwi kwa fimbo bali ni kwa mapambo.

Asanteni kwa kunisoma.

Mwisho
 
Kanda ya ziwa kabila gani? Pole na msoto...
 
duh nawewe ulijitoa mhanga yaani kwenye stage ya boyfriend na girlfriend unachezea kipigo kiasi hicho haukua serious na roho yako,pole kwa yaliyokusibu lakini mie kabla ya ndoa na baada ya ndoa kuchezea kichapo ni issue ndani lazima pageuke wwe john cena na undertaker aiseeh huo ni upuuzi.
 
Huyu Jamaa ni lazima atakuwa ni Mkurya...Bisha!!!

Hawa Wakurya wanaboa sana na tabia yao ya kupiga wanawake
 
Baada ya kuachana hakukubembeleza mrudiane?hebu nisaidie kidogo
 
Hapa ndipo wanawake wanaposhangaza, unapigwa na boyfriend?! Mtu ambaye hata hajaji-commit kwako!!

Angekutia kilema halafu akakutupilia mbali si ungejiua?
 
Hawa jamaa wanaopiga wanawake inaonekana wana kitu kingine ambacho wadada huwa hawataki kukisema, huyu anasema nilikuwa nampenda nilkuwa nategemea atabadilika. Mie nafikiri lazima kuna kitu wanachowapendea na kuwafanya wavumilie kipigo. Wengine pia wanasema msichana au mvulana mwenye wivu ana wapembeni wengi hivyo kila wakati huwa wanafikiri kuwa kwa vile wao wanaiba na wao wanaibiwa pia
 
Hawa jamaa wanaopiga wanawake inaonekana wana kitu kingine ambacho wadada huwa hawataki kukisema, huyu anasema nilikuwa nampenda nilkuwa nategemea atabadilika. Mie nafikiri lazima kuna kitu wanachowapendea na kuwafanya wavumilie kipigo. Wengine pia wanasema msichana au mvulana mwenye wivu ana wapembeni wengi hivyo kila wakati huwa wanafikiri kuwa kwa vile wao wanaiba na wao wanaibiwa pia

Kweli kabisa, wanakuwaga na wa pembeni coz tulivyobreak tu haikupita hata wiki nakawa na mdada mwingine, kuhusu kuwa na la ziada sio kweli kwani wengine Mungu alivyotuumba hatuwezi kubadili badili wanaume kama nguo, sso unavumiliaaa weee hadi nuone mwisho.....lakini by now uonevu sitaki tena,
 
Baada ya kuachana hakukubembeleza mrudiane?hebu nisaidie kidogo

Attempt za kuachana zilikuwa nyingi tu, ila anabembeleza weeee, atakupiga shopping zaa kufa mtu, maumivu ya kipigo nayasaahau basi tunaanza upya. Haipiti siku yanaanza yale yale.......marafiki zake walikuwa mbulula sanaa coz katika kugombana kwetu wao wana mchango 80%.
 
Huyu Jamaa ni lazima atakuwa ni Mkurya...Bisha!!!

Hawa Wakurya wanaboa sana na tabia yao ya kupiga wanawake

Me sijui ila sifa ya kabila la huyo X ni kutembea katika makundi kama kanga, hata maamuzi yao ni ya kimakundi.....hapo ndipo waliponichosha, yani kitu kinachonihusu mimi lazima kipelek´we kwenye kundi la kabila kijadiliwe ndipo mtu aambiwe aamue nini,
 
Kanda ya ziwa kabila gani? Pole na msoto...

Asante kaka/dada, ulikuwa msoto hasa, alafu mkaka ukimuona alikuwa mpole sana huwezi kufikiria kama ndio anaweza kuwa ndio alikuwa vile. Nilishasahau na kumsamehe
 
duh nawewe ulijitoa mhanga yaani kwenye stage ya boyfriend na girlfriend unachezea kipigo kiasi hicho haukua serious na roho yako,pole kwa yaliyokusibu lakini mie kabla ya ndoa na baada ya ndoa kuchezea kichapo ni issue ndani lazima pageuke wwe john cena na undertaker aiseeh huo ni upuuzi.

acha kutuzuga we mwenyewe uskute ulikua unadundwa kama sio kudundwa hata kusemwa kama mtoto
 
Hapa ndipo wanawake wanaposhangaza, unapigwa na boyfriend?! Mtu ambaye hata hajaji-commit kwako!!

Angekutia kilema halafu akakutupilia mbali si ungejiua?

ndo mana wanasema mapenzi upofu hata we pengine ulikua una mmind dem wako kwa vitu flan lakin hujamuoa yeye elewa hicho kitu pale unakua una uhakika coz hujui ya mbeleni
 
Yeye alikuacha akaoa au wewe ulimwacha?

Je mwingine huyu mpya hapigwi?

Jichunguze pia na wewe!
 
acha kutuzuga we mwenyewe uskute ulikua unadundwa kama sio kudundwa hata kusemwa kama mtoto

we nae umekurupuka ulikotoka unaniletea uchuro,yawezekana we ndo huwa unanidunda siwezi jua.
 
Back
Top Bottom