Nimeingia mkuku-mkuku hapa nikidhani kuna kitu nitajifunza kutokana na kichwa cha habari ambacho kwa kiasi fulani kinaakisi tawala nyingi za ulimwengu wetu.
Mtoa mada hujatuonesha "HOW" umefikia hilo hitimisho/conclusion, umekua mchoyo wa maarifa, tafadhali funguka Mkuu, naamini kuna mambo mengi sana ya kujifunza kutokana na kichwa cha habari cha uzi wako.
Na jambo jingine ningeomba wanabodi kupunguza kutupiana vijembe hasa kwenye masuala ya imani, na ikitokea mchangiaji utaongea kitu kitakasogusa imani/dini, hebu jaribu kujenga hoja bila dhihaka kwa imani/dini husika kwa kukumbuka hapa ni jukwaa la intelegensia, siyo uwanja wa imani/dini, tulitendee haki jukwaa na tusiharibu 'nyuzi' kwa vijembe, ubishi na ushabiki wa kidini/imani