Dunia ilitokea by chance

Dunia ilitokea by chance

Omari Makoo

Member
Joined
Sep 6, 2016
Posts
78
Reaction score
39
Scientist.gif

Siku moja wanayasansi walikuwa wakibishana wengine wakisema MUNGU yupo na wengine wakisema MUNGU hayupo. Waliosema Mungu hayupo waliulizwa swali kama MUNGU hayupo je dunia iliumbwa na nani?

Wakasema DUNIA ilitokea by chance (yaani ilitokea tu) pasina kuwa na muumbaji. Wengi waliamini katika hilo kwamba dunia ilitokea by chance, Mwanasayansi mmoja ambaye alikuwa bado anaamini MUNGU yupo aliamua kuwafanyia jambo flani wenzake.

Siku moja kabla ya kikao chao cha mambo ya kisayansi aliingia kwenye chumba cha mkutano kwa siri na kuamua kuweka mpira kwenye meza kisha akatoka.
Muda wa kikao ulipofika wanasayansi wote waliingia humo ndani na kuanza kujadili mambo mbali mbali ya kisayansi, kisha wakati walipomaliza kikao kila mtu alikusanya mafaili yake na kutaka kuondoka.

Yule mwanasayansi akachokoza kwa kuuliza mpira huu ni wa nani kila mtu akasema sijui jamaa akasema inamaana hauna mwenyewe wote wakanyamaza kimya kuashiria kutomfahamu mmiliki wa mpira ule.

AKAWAAMBIA BASI MPIRA HUU UTAKUWA UMETOKEA BY CHANCE
wote wakabisha na kusema haiwezekani mpira utokee by chance kwenye chumba cha mkutano, walibisha kwa kiwango kikubwa sana. Kisha akawaambia kama mpira mdogo hivi hamuamini kutokea kwake BY CHANCE vipi kuhusu dunia ambayo ni kubwa zaidi?
 
Mungu yupo na ndie alieumba ulimwengu na vilivyomo kwa ustadi usioweza kumithilika.

Hakuna chance inayoweza kutengeza mifumo ya maumbile mbalimbali iliyopo ulimwenguni kwa ustadi ambao akili zetu huishia kustaajabu na kujiuliza ni kivipi kuna umbile kama hili na kwa nini lipo.

Ufinyu wa ufahamu wetu umetufanya kila leo wanasayansi kubadili kauli juu ya sayari na mifumo yake. Na bado hata kwa elimu hii ndogo tunayofunguliwa hatutaweza kuyamkini na ku comprehend kila jambo la Muumba.

Mwenyezi Mungu ametupa akili na Free will / freedom of choice katika kuyaendea yale ambayo ameyaamrisha na kuyaumba. Ni katika uhuru huo wapo watakaopinga uwepo wa Mungu na kuyapinga Maandiko yake kwa kuwa tu akili zao zinaona kuna contradictions. What if hizo contradictions zina exists katika akili zao tu kwa kuwa wameamua kuchagua kujifunga kuelewa yale ya Mungu Muumba?

Leo watu wanasema kwa nini aumbwe shetani kama kweli Mungu ni All Loving, the most merciful. Je shetani aliumbwa Shetani au kwa uamuzi wake alichagua kuwa shetani na kukataa misingi ya haki aliyoumbiwa? Tunaambiwa kwa miaka Dahr Iblees alikuwa ni katika kundi la waabudio waliokuwepo mbinguni, lakini kwa jeuri, inda, kiburi na inadi aliacha kufuata ktk misingi ya haki na kuchagua njia ya udhalimu.
Kuna njia kuu mbili za kufuata, moja ya kuamini na njia ya kukufuru. Uhuru ni wako kuchagua yale aliyochagua iblees na kukataa ya Mungu. Hivyo ndivyo utakavyochagua outcome ya maisha yako baada ya kifo.

Huyo ndie Mungu alieumba kila kitu, cheupe vs cheusi, kizuri vs kibaya, imani vs kufuru, pepo vs moto, +vs -, mume na mke na variations zote zilizopo ili apate kututahini (LICHA ya kuwa anajua outcome ya mtihani) nani kati yetu ni mbora katika kuyafanya mema.

Ushauri kwa wanaobishana kuhusu Dini, Tukae chini tuzisome dini zetu. Tumfahamu Mungu ukweli wa kumfahamu ili tuweze kunuabudu ipasavyo na kujua hekima yake katika kila alichokiumba.
 
Vipi na GOD na yeye alitokeaje/alianzaje..?
 
Swali hili ni kwa wakina nani walijibu, wale wanaoamini uwepo wa Mungu, au kwa wale wasioamini uwepo wake ????
 
Hawa wanasayansi wanajifanya ni wanajua sana ila ukweli wanaweza kugundua vyote ila hapo kwenye Mungu wataendelea kuchemka maana mpk Leo Bado wanapingana wao kwa wao
 
Hebu wasaidie basi ili wasiendelee kuchemka,wafanye nini ili waamini Mungu yupo ......... ???
 
ko
Wale ni Thomas hawaamin mpk waone kwa macho hapo ndio penye shida ila sie watu wa Mungu hatuna shida na hilo kwani tunaongea nae kama kawa
 
Hizi mada za waamini na wasioamini zimekuwa nyingi! Sijui tafsiri yake nini?
 
Mungu yupo na ndie alieumba ulimwengu na vilivyomo kwa ustadi usioweza kumithilika.

Hakuna chance inayoweza kutengeza mifumo ya maumbile mbalimbali iliyopo ulimwenguni kwa ustadi ambao akili zetu huishia kustaajabu na kujiuliza ni kivipi kuna umbile kama hili na kwa nini lipo.

Ufinyu wa ufahamu wetu umetufanya kila leo wanasayansi kubadili kauli juu ya sayari na mifumo yake. Na bado hata kwa elimu hii ndogo tunayofunguliwa hatutaweza kuyamkini na ku comprehend kila jambo la Muumba.

Mwenyezi Mungu ametupa akili na Free will / freedom of choice katika kuyaendea yale ambayo ameyaamrisha na kuyaumba. Ni katika uhuru huo wapo watakaopinga uwepo wa Mungu na kuyapinga Maandiko yake kwa kuwa tu akili zao zinaona kuna contradictions. What if hizo contradictions zina exists katika akili zao tu kwa kuwa wameamua kuchagua kujifunga kuelewa yale ya Mungu Muumba?

Leo watu wanasema kwa nini aumbwe shetani kama kweli Mungu ni All Loving, the most merciful. Je shetani aliumbwa Shetani au kwa uamuzi wake alichagua kuwa shetani na kukataa misingi ya haki aliyoumbiwa? Tunaambiwa kwa miaka Dahr Iblees alikuwa ni katika kundi la waabudio waliokuwepo mbinguni, lakini kwa jeuri, inda, kiburi na inadi aliacha kufuata ktk misingi ya haki na kuchagua njia ya udhalimu.
Kuna njia kuu mbili za kufuata, moja ya kuamini na njia ya kukufuru. Uhuru ni wako kuchagua yale aliyochagua iblees na kukataa ya Mungu. Hivyo ndivyo utakavyochagua outcome ya maisha yako baada ya kifo.

Huyo ndie Mungu alieumba kila kitu, cheupe vs cheusi, kizuri vs kibaya, imani vs kufuru, pepo vs moto, +vs -, mume na mke na variations zote zilizopo ili apate kututahini (LICHA ya kuwa anajua outcome ya mtihani) nani kati yetu ni mbora katika kuyafanya mema.

Ushauri kwa wanaobishana kuhusu Dini, Tukae chini tuzisome dini zetu. Tumfahamu Mungu ukweli wa kumfahamu ili tuweze kunuabudu ipasavyo na kujua hekima yake katika kila alichokiumba.
1473275400578.jpg
 
Back
Top Bottom