mwekundu
JF-Expert Member
- Mar 4, 2013
- 22,475
- 21,046
Zamani,Mwanaume ili uwe na soko hapa mjini ilikuwa lazima upige chuma,uwe na mwili wa mazoezi,soap soap pamba kali,moka mchongoko kama mchaga wa mbarali,basi una uhakika unan'goa mzigo kiulaini...Wazee wetu waliopenda dogodogo walikuwa bize sana Saloon kupaka Superblack na Picol ili kuficha mvi ili soko lao liwe japo angalau... Ukitaka kuamini dunia duara siku hizi walaaaaa,we kuwa na mtumbo mkubwa suruali saizi 52,midevu,sura mbaya,mvi kibao kama lowasa ila uwe na hela,unapata watoto wote,kuanzia form 2,mademu wa chuo ndo kabisa elimu haiwasaidii wakiona mvi ndo pichu zinapwaya,utaitwa baby japo una wajukuu.. Na Hii ni nguvu ya Mpesaaaaaaaaa,hela ilimsaliti Yesu...Hela inauza utu wa wanawake,wanalala na baba zao bila aibu ili wapate hela ya high heels...Na kuna wanaume wanainamishwa ili wapate magari...Mungu okoa hiki kizazi maana watoto wetu watakaozaliwa na kizazi hiki cha nyoka sijui watakuwaje kama mama zao hawana tofauti na changudoa wa Corner Bar.