Kama ulisoma hapa TZ si kweli kusema ulijifunza DUNIA NI DUARA peke yake bila KONA YA DUNIA,Vinginevyo uwe umesahau.
Ni kweli tumejifunza kua dunia ni duara [ki-jiografia],.Ila ktk somo la kiswahili tunajifunza FASIHI,huko ndio kuna misemo mbali mbali yenye kusisitiza au kuweka mkazo au kuelezea/kufunza kitu fulani ili kuielimisha jamii,Ndio hapo utakapokutana na maneno kama "kila kona ya dunia","kila pembe ya dunia":Uwe mwangalifu wapi linatumika hilo neno na kwa lengo gani.