Duh! Hivi suala la Katiba Mpya halimo!!?

Duh! Hivi suala la Katiba Mpya halimo!!?

Click Hapa

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2013
Posts
479
Reaction score
206
Wanajamvi,
Mniwie radhi mtakaokerwa na post hii na hasa kwa wale wenye mihemuko ya kisiasa.
Jana nimesikiliza kwa umakini hotuba ndefu ya Muh. Magufuli kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni pale viwanja vya Jangwani.
Muh. Magufuli aliongea mengi kwa maana alikuwa akiongozwa na ilani ya uchaguzi ya ccm.
Nilichoshangaa ni kutokuzungumzia kabisa suala la Katiba Mpya.
Ikumbukwe kuwa suala la Katiba Mpya halikuwemo kabisa kwenye ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2010-2015, ni ajenda waloipoka kutoka upinzani, baada ya kufanikiwa kuipoka iliundwa tume ya kukusanya maoni ya wananchi, hii ilijulikana kama tume ya Warioba, tume ilimaliza Kazi ile kwa mizengwe ndipo likaja suala la bunge Maalum la Katiba, yaliyojiri huko wengi tunajua, ila cha muhimu ilizaliwa UKAWA, baadaye ilikuja iliyoitwa katiba Mpya inayopendekezwa, katiba hiyo pendekezwa ilikuwa ikisubiria kura ya maoni tu ili iweze kupitishwa na Taifa Tanzania liwe na katiba Mpya.
Cha kushangaza, kwa Mara nyingine tena suala la Katiba halimo kwenye ilani ya uchaguzi ya ccm, yaani katiba si kipaumbele cha ccm.
Sasa najiuliza, hii ccm inaona katiba iliyopo inatosha? Na kama hivyo ndivyo, ilikuwaje wakatumia mamilioni ya shilingi za walipa kodi kugharimia bunge Maalum la Katiba, na mamilioni ya shilingi kuchapisha nakala za katiba pendekezwa kwa jambo lisilokuwa na umuhimu???
Na je, kama suala la Katiba Mpya lipo, ni lini sasa litafanyiwa kazi, maana si kipaumbele kwa ccm au ndo tuseme ccm inataka kuendesha nchi bila katiba.
Mzee Warioba mwenyewe Jana kasema mengi, mbona la Katiba hakulisema, au naye kasahau??

Karibuni kwa tafakari
 
Wakiongea katiba mpya ni sawa na kuipa promo UKAWA so hilo kwa CCM Ni kama mti washawasha hata hawataki kulisikia kabisa.
Hili la katiba bila shaka ni hoja kubwa kabisa itakayotumiwa na UKAWA kUONESHA roadmap ya kutatua maloloso meeeengi yaliyozalishwa na mfumo wa kutawala nchi hii chini ya CCM.

Pia najiuliza UKAWA wakisafiri na hii hoja ya katiba mpya mzee Warioba na yule Polepole(controversial guy) wataongea hoja gani kumpamba mgombea wao wa MAGAMBA tofauti na kuporomosha matusi kwa mgombe wa UKAWA.

UKAWA = UMOJA WA KATIBA (MPYA) YA WANANCHI.
CCM = CHAMA CHA MKAPA.
 
Back
Top Bottom