DSTV na Vodacom acheni utapeli

DSTV na Vodacom acheni utapeli

Kwa mujibu wa hiyo Sms uliyo pata mbona ina onyesha VODACOM, wameisha fikisha pesa zako DSTV………kitu kingine je ume reset Decoder yako?
Hilo nimeshalifanya mkuu,

Hata DSTV nimepagia wanisaidie kufanya reset baada ya mimi kufanya na kutokuona mabadiliko yoyote na jibu wanalotoa ni hakuna pesa kwenye account yangu ya DSTV.
 
Mimi ilishanitokea enzi za kifurushi cha 147000/- mwaka juzi mpaka leo sijarudishiwa hela kwa tukio kama hili
 
Naam,

Hatimaye nimeunganishiwa kifurushi changu....

Nashukuru DSTV ila naomba mjitahidi kuonyesha njia ya uwajibikaji na mfano wa kujali wateja...

Sio mpaka tuwaanike ndio muamke maofisini na kufanya kazi zenu.

Laah sivyo mkileta na kuendekeza dharau mtapotea fasta.

USHAURI KWA WATEJA MLIODHURUMIWA:
Msikubali kupoteza pesa zenu kirahisi, hawa watu wameweka vijana ofisini kwasababu yetu sisi, sasa hawa vijana wamekaa tu maofisini wanajisahau wanaona wao tu ndio wenye kuzijua kazi wazifanyazo! Nilazima tuwaamshe.

Naomba DSTV na VODACOM ifundishe wahudumu wao kitu kinaitwa '' Logical thinking'' na wasiishie kupokea simu za wateja na kuleta siasa tu-kupiga domo tu. Yaani mtu anakasirika unapomwelekeza tatizo lako, anaona ni usumbufu eti-haaa!

Vijana wamekalilishwa majibu. Hawafikirii unachowaambia na wajibu inavyotakiwa. Wamekalili majibu tu.
Screenshot_2018-09-22-14-57-18-764_com.google.android.gm.jpeg
 
DSTV subscription payment successful.
Smartcard/account 10210616099
TZS 109000.00
Trans ID 5IK11OAPTMF
Reference 5IK11OAPTMF
If the service is not restored (E16 error), SMS the word RESET with your smartcard number to 15727. For assistance call 0768 988 800

Mimi pia nimelipa jana nimepewa maneno tu toka jana...
Mie nililipia siku tatu zilizopita, leo asbh wakakata channels, nikapiga simu wakanipa majibu account yako haina hela uzuri nilipia kwa kutumia simu nyingine nikaanza kumsomea meseji herufi kwa herufi.......ooh tunaomba radhi kwa usumbufu ulioupata, tunashughulikia suala lako, baada ya dk tano wakarudisha channel zote.....ni wapuuzi ukizubaa hela zinaenda na maji
 
Hatari sana, ukizubaa unapigwa
 
Naam,

Hatimaye nimeunganishiwa kifurushi changu....

Nashukuru DSTV ila naomba mjitahidi kuonyesha njia ya uwajibikaji na mfano wa kujali wateja...

Sio mpaka tuwaanike ndio muamke maofisini na kufanya kazi zenu.

Laah sivyo mkileta na kuendekeza dharau mtapotea fasta.

USHAURI KWA WATEJA MLIODHURUMIWA:
Msikubali kupoteza pesa zenu kirahisi, hawa watu wameweka vijana ofisini kwasababu yetu sisi, sasa hawa vijana wamekaa tu maofisini wanajisahau wanaona wao tu ndio wenye kuzijua kazi wazifanyazo! Nilazima tuwaamshe.

Naomba DSTV na VODACOM ifundishe wahudumu wao kitu kinaitwa '' Logical thinking'' na wasiishie kupokea simu za wateja na kuleta siasa tu-kupiga domo tu. Yaani mtu anakasirika unapomwelekeza tatizo lako, anaona ni usumbufu eti-haaa!

Vijana wamekalilishwa majibu. Hawafikirii unachowaambia na wajibu inavyotakiwa. Wamekalili majibu tu. View attachment 874653
Hapa nilikuwa natafita DSTV special thread kama ipo, nikaishia kukutana na huu uzi.

Mkuu tuambiane umefanikiwa vipi? Maana hata mimi naona lao wananizingua, nimelipia kwa Mpesa na text nikaridishiwa ila channels hazijarudi mpaka sasa, nimewapigia watu wa multichoice wanasema hawajapokea hela toka voda kwa account yangu... Hapa sijui niwafanye nini maana najua hata nikiwapigia voda wao watasema tu wameishalipa hela.
Sio siri wanaboa yani wanakera vibaya DSTV hii niliyoiamini miaka na miaka naona wanafanya vitu vya ajabu ajabu
 
Happ si kuna ujumbe unasema "if the service is not restored E16 error, SMS the word RESET with your smartcard number to 15727..je ulifanya hivyo
 
Halafu pia ukiwa unajiunga na kifurushi lazima decoder iwe on..je ulifanya hivyo?
 
Naam,

Hatimaye nimeunganishiwa kifurushi changu....

Nashukuru DSTV ila naomba mjitahidi kuonyesha njia ya uwajibikaji na mfano wa kujali wateja...

Sio mpaka tuwaanike ndio muamke maofisini na kufanya kazi zenu.

Laah sivyo mkileta na kuendekeza dharau mtapotea fasta.

USHAURI KWA WATEJA MLIODHURUMIWA:
Msikubali kupoteza pesa zenu kirahisi, hawa watu wameweka vijana ofisini kwasababu yetu sisi, sasa hawa vijana wamekaa tu maofisini wanajisahau wanaona wao tu ndio wenye kuzijua kazi wazifanyazo! Nilazima tuwaamshe.

Naomba DSTV na VODACOM ifundishe wahudumu wao kitu kinaitwa '' Logical thinking'' na wasiishie kupokea simu za wateja na kuleta siasa tu-kupiga domo tu. Yaani mtu anakasirika unapomwelekeza tatizo lako, anaona ni usumbufu eti-haaa!

Vijana wamekalilishwa majibu. Hawafikirii unachowaambia na wajibu inavyotakiwa. Wamekalili majibu tu. View attachment 874653
Tatizo ulipaniki huenda hata hukufuata hatua za RESET au decoder yako haikua ON wakati ukinunua muhamala....sometime wateja na sisi hatuna uelewa tunakimbilia kulaumu tu
 
Mkuu, usiwe unachangia bila kusoma maelezo na ukaelewa.... Rudia kusoma nilichokiandika na nilichokuwa najibu toka kwa wadau waliochangia huu uzi.....
 
Hapa nilikuwa natafita DSTV special thread kama ipo, nikaishia kukutana na huu uzi.

Mkuu tuambiane umefanikiwa vipi? Maana hata mimi naona lao wananizingua, nimelipia kwa Mpesa na text nikaridishiwa ila channels hazijarudi mpaka sasa, nimewapigia watu wa multichoice wanasema hawajapokea hela toka voda kwa account yangu... Hapa sijui niwafanye nini maana najua hata nikiwapigia voda wao watasema tu wameishalipa hela.
Sio siri wanaboa yani wanakera vibaya DSTV hii niliyoiamini miaka na miaka naona wanafanya vitu vya ajabu ajabu
Wapigie tena DSTV mkuu na VODA, maana hata mimi niliwapigia mwanzoni wakazingua ila badae wamerekebisha baada ya kuwaanika hapa....

Vodacom walinirudishia ela yangu nikanunua kifurushi tena ila kipindi nasubiria pesa irudi-DSTV waliniwashia huduma
 
Leo nimewapigia tena, naona wamerudisha huduma, wahuni sana hawa
 
Mtu kuna mdau alisema ataanzisha dstv special thread naona kuna uhitaji huo
 
Kumbe hizi shida ni za siku nyingi sana, na bado zinaendelea!
 
""Kama mimi ndiye mfanyakazi wa DSTV au wa Vodacom Nitamwambia mteja anipe maelezo na mawasiliano na viambata vyake vya malipo kisha ninawasiliana na wenzangu(Voda/DSTV kutegemeana ni nani aliyeshugulikiwa) halafu ninampigia simu mteja na kumtatulia tatizo lake.
Kama litachukua mda kutatua basi mteja atarudishiwa fedha yake au huduma yake kisha sisi kama kampuni tutajua tunamaliza vipi tatizo""

Jamani Hayo ni Majibu ya mtoto wa jirani anasoma darasa la Tano yaani katoto kako very bright nimetamani kangekuwa ka kwangu.
Shame on you dstv na voda Hebu kuweni serious na hela zetu sisi wateja maana bila sisi hamtaweza kula
Alaaaaa
Siku moja natamani , Jamii forum , waweke kitufe cha kurekodi sauti ukihitaji kujirekodi sauti badala ya maandishi , ili nilivojikuta nacheka hapa iwe rahisi nirekodi kicheko changu.
 
Back
Top Bottom