DRC yapata mwaka wa mgogoro wa kisiasa

TangataUnyakeWasu

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,268
1,587
Rais Kabila na wapinzani wametiliana saini juu ya serikali ya mtoto. Makubaliano hayo yaliyopitishwa na kusimamiwa Kwa ushawishi mkubwa chini ya viongozi wa kanisa la Catholic ni kuwa utawala wa Rais Joseph Kabila Utakoma mwisho mwa mwaka huu 2017.
 
Ngoja tuone mwisho wao,cha msingi tuwaombee mwisho mwema na viongozi wao watangulize maslahi ya Wakongomani kwanza,ni jambo la kustaajabisha lakini ndiyo ukweli,Wananchi wa vijijini mashariki mwa Kongo wanashindwa kwenda mashambani kutokana na kutokuwa na uhakika wa usalama wao,kama nikienda nitarudi salama au nitachinjiwa shambani kwangu na Waasi wa ADF,kitu ambacho ni tofauti na hapa kwetu Tanzania,shamba usiende kwasababu unazoziona wewe zinafaa lakini si kwa kukosekana usalama,Wito wangu kwa Watanzania wenzangu tuithamini,tuilinde na kamwe tusiichezee amani yetu kwani ukibahatika kuishi sehemu ambayo haina amani,utagundua tumetunukiwa kitu adhimu ambacho hatuna budi kukilinda kama mboni za macho yetu,shukraan hayo ni mawazo yangu!
 
Back
Top Bottom