Niseme wazi kuwa kwa mara ya kwanza kumwona Dr.Tulia Ackson kwenye "public domain" ilikuwa ni kupitia kipindi cha "This week in perspective" cha Mzee Adam Simbeye pale TBC. Hakika siku hiyo niliyomsikiliza "Dada"huyo nilisema ni "Kichwa" na pia nilidhani si Mtanzania kutokana na sura yake nzuri ya "kijaluo" na kiingereza chake safi! ,hakika nilijua "Dada" huyu ni Mkenya! Hapa kwetu tumezoe viingereza vya Wanasheria wetu vya " Zeee, zeee, zat,zat, zis,zis !" Sio kwa Dr.Tulia Ackson, ni kweli "ametulia" mentally! Mara ya pili kujua Dr.Tulia Ackson ni "Kichwa" ni wakati wa Bunge maalum la Katiba alipokuwa katika Kamati ya Kanuni akiwa na Professor Costa Mahalu wakati bunge hilo likiongozwa na Mzee wa Busara nyingi,Mzee wetu Pandu Ameir Kificho bila kanuni zozote rasmi! Hongera sana CCM kwa kumuibua Dr.Tulia Ackson,kweli CCM ni mabingwa duniani wa "succession plan"! Nacheka saaana eti CUF wanataka Lipumba agombee tena Uenyekiti!hawana "watu"?! Shauku yangu ya kutaka kumjua zaidi Dr.Tulia Ackson iliongezeka pale alipogombea Unaibu Spika na ikawa Zitto Zuberi Kabwe Mbunge wa Kigoma mjini (ACT -Wazalendo) akawa anampinga kwa nguvu zake zote na badala yake akawa anamtaka Mhe.Zungu (Mbunge wa Ilala) ndo awe Naibu Spika! Nilijiuliza maswali mengi mno kuhusu dhamira ya Zitto Kabwe kumpinga Dr.Tulia Ackson kwenye Unaibu Spika! Nilijiuliza hivi Zitto huyu hajui kuwa Mhe. Job Ndugai mbali na kubobea kwenye masuala ya Wanyamapori si Mwanasheria! Na hata Mhe.Zungu huyu hajabobea kwenye sheria! Sasa kwa nini Zitto ampinge Mwanasheria Nguli kama Dr.Tulia Ackson kwenye nafasi ya Unaibu Spika ambayo kuwa kwake pale ni afya kwa Bunge ?! Tafakuri yangu ikanirudisha nyuma hadi mwaka 2002 nilipojiunga kwa ajili ya degree yangu ya kwanza pale Mlimani (UDSM).Nilipofika pale nilikuta Zitto Zuberi Kabwe ni Katibu Mkuu wa DARUSO (Dar Es Salaam University Student Organization),kwa kuwa niliambiwa kuwa Zitto Kabwe alitumia miaka 5 kuhitimu degree yake ya kwanza (BA.Economics) mwaka 2003,badala ya miaka 3 (sababu anazo mwenyewe) basi atakuwa alijiunga UDSM mwaka 1999! Na pia niliambia kuwa Dr.Tulia Ackson alihitimu degree yake ya kwanza (LLB) mwaka 2002,basi naye atakuwa alijiunga UDSM mwaka 1999 ! Hivyobasi yawezekana Zitto Kabwe alimjua Tulia Ackson tangu Mlimani! Na kama Zitto alimjua Tulia Ackson basi anajua na "Ukipanga" wake! Kwa mwanasiasa anayependa umaarufu kama Zitto Kabwe basi mtu design ya Dr.Tulia Ackson lazima awe kikwazo! Na kwa muda mfupi Dr.Tulia Ackson amesham-outsmart Zitto Kabwe! Ameshamfukuza Bungeni na sasa anaweweseka ! Mkutano wake wa ACT- Wazalendo pale Mbagala Zakheem amezidiwa na tamasha la wakaanga chips lililofanyika siku hiyo chini ya Clouds media! Zitto alidhani na hili Bunge live litamtoa kama issue ya Buzwagi! Hakuna na hata Mikoani mkienda mtaambulia aibu kwani watu wamechoka sanaa zenu na sasa wako busy kujenga maisha yao kuliko kuwajenga nyinyi na ajenda zenu za kijinga. Si Zitto Kabwe tu aliyeanza kuonja joto ya jiwe Bungeni chini ya Uongozi Shupavu wa Dr.Tulia Ackson! Wako wapi "ma-bush lawyer "waliong'ara kipindi cha Mama Makinda kama John Mnyika!? Yuko wapi Tundu Lissu Mwanasheria mropokaji! Wako wapi "VILAZA" kama Lema,Sugu,Mchungaji Msigwa,Esther Bulaya na kubwa lao Mbowe!? Hongera sana Dr.Tulia Ackson kwa uongozi wako shupavu! Keep it up Spika wetu wa baadaye!!