MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,255
- 8,027
Katika hii nchi kuna vituko sana mpaka mtu unajiuliza mambo mengi sana! Leo Kuna kundi linampamba Dr Slaa na kumwita Mzalendo, mpiganaji, upinzani wa kweli, mpinga ufisadi! Lakini kabla ya Lowassa Kuhamia Chadema hawa hawa watu walikua wanamwita Padri,kiongozi wa kanisa,Babu,Fisadi anayejikopesa pesa ndani ya Chama,walimwita ni mtu aliyetumwa toka vatkani na Ujerumani! Alipewa majina ya kila aina!
Leo Dr Slaa anasifiwa kinafki na watu wale wale wanamwita Mzalendo wa kweli, mpiganaji! Hawa watu wanashindwa kuelewa kwamba Dr Slaa ni Kichwa kingine anawasoma tu wanavyohangaika na mwisho wa siku aibu yao.
Ni mtu ambaye ambaye anazifahamu fika shida za watanzania, ameshaketi na wenzake mezani kuumiza vichwa ili kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi October na wakaona silaha pekee ni ile iliyoachwa na wapinzani wao wakuu!
Hawa hawa watu wanaelewa kua kukaribishwa Lowassa CHADEMA ni baada ya vikao vingi vya kamati kuu na kuridhia suala hilo maana Mwenyekiti hawezi kua na sauti peke yake bila ya watendaji wenzake.
Badala ya kupeana mikakati ya namna ya kupambana na nguvu inayokuja kutoka UKAWA wanabaki kummezea Dr Slaa mate huku yeye akiwachora huku yuko bize kuandaa mikakati zaidi ya ushindi mwezi October. Sawa na ile hadithi ya Fisi kumfuatilia binadamu kwa nyuma huku akusubiri mkono uanguke ili aufaidi kumbe binadamu anasonga mbele, kitu ambacho hakiwezekani.
Nionavyo mimi hata kama Lowassa asingekuja UKAWA bado nguvu ingekua kubwa kwa sababu tu kitendo chao cha kihistoria kuungana na kua wamoja mpaka wanafikia kumtoa mgombea urais mmoja,mbunge mmoja kwa kila jimbo na madiwani kwa kila kata ilikua ni ushindi tu.Sasa Lowassa ameongezea nguvu ambayo ni kubwa kwanini watu wasichanganyikiwe? Kwanini watu wasikose usingizi?
Tuwe wakweli tu kwa hili jambo!