Dr Slaa ni Sokoine Mpya, Tumaini Letu

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Kuna sifa mbili kubwa walizokuwa nazo Nyerere na Sokoine. Walikuwa waadilifu na walikuwa wana wezo wa kufikiri, wachapa kazi. Hizo ndizo sifa za rais tunayemtaka leo. Kuna watu wanamwomba Mungu atupe tena kiongozi kama Nyerere na Sokoine. Ila jibu ni rais, Nyerere na Sokoine tupo nao ila labda hatuwaoni. Dr Slaa ni Sokoine ambaye baadhi ya watu hawaoni. Hata Jesus alipokuwa na watu wake hawakumtambua. Mungu atujalie tuone, tufanye maamuzi sahihi ya kuwaondoa CCM na kuweka watu wazuri kama Dr Slaa na Sitta
 
Hizi sifa mbili za uadilifu na uwezo wa kuongoza ni watu wachache sana wanazo. Mfano Nyerere alikuwa nazo zote, Sokoine pia. Lowassa ana uwezo mkubwa wa kuongoza lakini si mwadilifu, Pinda ni Mwadilifu ila hana uwezo wa kufanya maombo yaende, JK hana sifa zote mbili, Dr Slaa kwa kiasi ninachomfahamu ni mwadilifu na ana uwezo mkubwa wa kusimamia mambo, kupambana na rushwa na hana mzaa hata kidogo. Atakuwa kama Nyerere ukisikia anakuita ikulu hupati usingizi!
 
uadilifu ni dhana pana sana jamani
Definition ya uadilifu inategemea wewe ni nani. Kama wewe ni shehe au mchungaji halafu ukawa na nyumba ndogo tutasema wewe si mwadilifu. Ukiwa kiongozi wa serikali na ukawa si mla rushwa na unafanya kazi kulingana na kiapo chako wewe ni mwadilifu. Usifikiri Nyerere alikuwa hana nyumba ndogo, alikuwa nazo ila alikuwa hana utani kwenye kazi ya umma. Ni kwanini unasema Dr Slaa si mwadilifu?
 
Usimfananishe Slaa na waziri mkuu wetu aliyekuwa anavaa safari buti, ana pea tatu za viatu, alikuwa analipwa shilingi elfu sita kwa mwezi, alijitolea asilimia kumi ya mshahara wake kila mwezi kusaidia matatizo ya watanzania.
Sio mtu anayechukua mshahara mnono bila kulipa kodi akidai hiyo ni posho. Siyo mtu anayeiambia serikali ipunguze kodi ya sukari na nafaka ilhali akijua wafanyabiashara wana hoard bidhaa ili bei ipande (kumbuka enzi za wahujumu).
TWO DIFFERENT PEOPLE WITH TWO DIFFERENT IDEOLOGIES!!..... DONT COMPARE COMRADES WITH BOSSES.
 
Back
Top Bottom