Hivi UKAWA kama watampitisha dr. Slaa na kweli wakafanikiwa kushinda uchaguzi katika uundwaji wa baraza la mawaziri kwa mujibu wa katiba ya sasa mawaziri lazima watoke chama alichotoka rais sasa je UKAWA inatambulika kama chama? Na kama haitambuliki kama chama itakuaje katika muundo wa serikali yao ? Vyama vingine vinavyounda ukawa vitashirikishwaje katika serikali ijayo kwa mwenye kujua naomba anijuze.
..mawaziri siyo lazima watoke chama alichotoka Raisi.
..katiba yetu inaruhusu hata waziri mkuu na raisi kutoka vyama tofauti.
..waziri mkuu ni lazima awe mbunge toka chama chenye wabunge wengi ktk bunge la muungano.
..kwa hiyo ikitokea chama kilichotoa Raisi hakina wabunge wengi bungeni, basi raisi na waziri mkuu watatoka vyama tofauti.
..sasa hivi tunaye waziri wa fedha, Mama Saada Mkuya, ambaye aliteuliwa toka serikalini. mpaka sasa hivi hakuna anayejua waziri wa fedha ni mwanachama wa chama kipi cha siasa.
..pia kuna wabunge 10 wa kuteuliwa na raisi. sasa katiba hailazimishi Raisi kuteua wanachama wa chama chake.