Dr. Slaa na Prof. Ibrahim Lipumba na hatma ya UKAWA

Ilongailunga

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2012
Posts
1,388
Reaction score
896
Wakati mchakato wa uteuzi wa nafasi ya mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM ukiendelea kushika kasi, joto la mchakato huo ndani ya vyama vinavyounda ukawa nalo linazidi kupanda, ni hivi majuzi tu zimesikika habari kuwa Menyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba nae akitangaza kuwa na nia ya kupeprerusha bendera ya umoja huo. Kwangu mimi hapo ndipo tatizo linapoweza kuanzia, haiyumkini kuwa vyama vingine vinavyounda umoja huo hasa CHADEMA vikakubali kwamba CUF ipeperushe bendera ya umoja huo, na hii ni kwasababu mbili zilizowazi, mosi, inaelekea umoja huo umekubali kuwa CUF iwakilishe umoja huo visiwani Zanzibar, hapa ni vigumu kwa umoja huo kukubali CUF pia iuwakilishe Tanzania nzima.

Pili CHADEMA ina nguvu kubwa bara kuliko CUF hivyo itakuwa ni vigumu sana kwa chama hicho kukubali chama chochote kinachounda umoja huo kutoa mgombea wa UKAWA, mantiki ya kisiasa inakubaliana na hoja hii, kuwa CHADEMA tayari kina mtaji mkubwa wa wapiga kura kuliko chama kingine chochote ndani ya umoja huo hivyo kilipaswa chenyewe kiungwe mkono na wala sio kiunge mkono, kazi ambayo CDM ingepewa na umoja huo ni kutafuta na kuleta mgombea ambae anakubalika na makundi yote ndani na nje ya UKAWA.

CUF wakiongozwa na dhana ya kuwa sisi tuna mgombea bora kuliko vyama vingine itakuwa na taathira kubwa katika siasa za UKAWA ni maoni yangu kuwa CUF inaihitaji sana CHADEMA kushinda majimbo mengi ya ubunge bara kuliko CHADEMA inavyoihitaji CUF, Vivyo hivyo kura za wafuasi wa CHADEMA hata kwa uchache gani zitakuwa muhimu sana kuamua hatma ya Urais wa Zanzibar katika uchaguzi ujao, kwa ufupi CUF inaihitaji zaidi UKAWA kujiimarisha katika siasa za Tanzania bara.

Nimeongea na baadhi ya viongozi waandamizi na wanachama wa kawaida ndani ya CUF, wengi wao wamejaa na dhana kuwa CHADEMA iliwasaliti kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, hoja hii haina mashiko kwakuwa ukiangalia takwimu za chaguzi zilizopita za serikali ya mitaa CUF imepata viti vingi vya vijiji, vitongoji na mitaa kuliko chaguzi zilizotangulia,hii ni kusema kuwa CUF imeimarika zaidi ndani ya UKAWA kuliko ilivyokuwa nje ya UKAWA, hoja hii ni kweli kwa vyama vyote vinavyounda umoja huo. Hapa ninaunga mkono maneno yalisemwa bungeni wiki iliyopita na mbunge wa kilwa kusini(CUF) Selemani bungara maarufu kama "-----" kwa kauli yake kuwa viongozi wa UKAWA wakikubali umoja huo uvunjike watakuwa ni wanafiki kuliko CCM na ni wasaliti

Hapo ndipo ninapoiona dhima ya viongozi wawili wanaotajwa kuwania Urais kupitia umoja huo Dr. Slaa na Prof. Lipumba kuwa ni muhimu kuliko wakati wowote toka uanzishwe umoja huo, Lipumba itabidi awe na chaguo moja, kuwapuuza wahafidhina ndani ya chama chake hivyo kukiimarisha zaidi chama chake au kuwakubalia hivyo kukidhoofisha zaidi chama chake (kwa kuwa vyama vingine vitakataa CUF watoe wagombea Urais SMZ na SMT) hivyo kuvunjika rasmi kwa UKAWA, DR. Slaa atakuwa na kazi kubwa ya kuchagua ima akubali kujiweka pembeni hivyo kuwakatisha tamaa wafuasi wengi wa CDM na kumuunga mkono mgombea mwingine (kwa hili CHADEMA itadumaa) au au CDM iingie yenyewe katika uchaguzi mkuu (hili likitokea CDM itabaaki palepale, haitashinda Urais na idadi ya wabunge itapungua au kuongezeka kidogo mno)

Kwa kuhitimisha ni vizuri tukaitaja nafasi ya mwenyekiti wa NCCR Bw. James Mbatia, huyu ni mtu muhimu sana kwa vile anayajua mahitaji ya sasa ya kisiasa na mtu anayefuata political realities, ni mategemeo ya wapenda siasa za ushundani kuwa atakuwa ndio political stabilizer ndani ya UKAWA. Tanzania inahitaji ushindani mkubwa wa kisiasa kwa kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
 
Hivi UKAWA kama watampitisha dr. Slaa na kweli wakafanikiwa kushinda uchaguzi katika uundwaji wa baraza la mawaziri kwa mujibu wa katiba ya sasa mawaziri lazima watoke chama alichotoka rais sasa je UKAWA inatambulika kama chama? Na kama haitambuliki kama chama itakuaje katika muundo wa serikali yao ? Vyama vingine vinavyounda ukawa vitashirikishwaje katika serikali ijayo kwa mwenye kujua naomba anijuze.
 
Hiyo lazima inatoka wapi nyie achani kufikiri yakaribu wale wamesoma na wanajitambua vyama pembeni maendeleo kwanza.
 
Common sense inasema mgombea urais wa UKAWA inabidi atoke CDM. Anaweza akawa Dr. Slaa au mwingine yeyote ila lazima atoke CDM....

Viongozi wa UKAWA hawawezi kuwa wapuuzi kiasi cha kutokuona kitu kama hicho ambacho kiko wazi kabisa !. Mtu yeyote mwenye akili za kawaida atakubaliana na ukweli huu ulio wazi...

Kwa mawazo yangu hili walishakubaliana mapema kabisa na ndio maana CDM ndio itakuwa ya mwisho kabisa kupick mgombea urais (nadhani watampata August kwa mujibu wa ratiba yao) na siku chache baada ya hapo UKAWA utakaa kum-confirm....

Vyama vingine lazima viendelee na utaratibu wao wa kuchagua wagombea wao na ili kuifanya hii process kuwa realistic kwa wafuasi na mashabiki wa vyama hivi na kuondoa fitina kutoka CCM, vyama hivi inabidi vichague wale wagombea ambao vinadhani ni the best !.

Kama professor Lipumba asingeamua kuchukua form za Urasi kupitia CUF, si ingekuwa wazi kwamba mgombea atatoka CDM ? Na hapo wangewezaje tena kusema eti wagombea wetu watashindanishwa katika kinyanganyiro cha UKAWA ?!

Hizi ni taratibu za UKAWA tu kuondoa fitina na kuhakikisha kuna stability ndani ya UKAWA.....
 
Wakati mchakato wa uteuzi wa nafasi ya mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM ukiendelea kushika kasi, joto la mchakato huo ndani ya vyama vinavyounda ukawa nalo linazidi kupanda, ni hivi majuzi tu zimesikika habari kuwa Menyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba nae akitangaza kuwa na nia ya kupeprerusha bendera ya umoja huo. Kwangu mimi hapo ndipo tatizo linapoweza kuanzia, haiyumkini kuwa vyama vingine vinavyounda umoja huo hasa CHADEMA vikakubali kwamba CUF ipeperushe bendera ya umoja huo, na hii ni kwasababu mbili zilizowazi, mosi, inaelekea umoja huo umekubali kuwa CUF iwakilishe umoja huo visiwani Zanzibar, hapa ni vigumu kwa umoja huo kukubali CUF pia iuwakilishe Tanzania nzima.

Pili CHADEMA ina nguvu kubwa bara kuliko CUF hivyo itakuwa ni vigumu sana kwa chama hicho kukubali chama chochote kinachounda umoja huo kutoa mgombea wa UKAWA, mantiki ya kisiasa inakubaliana na hoja hii, kuwa CHADEMA tayari kina mtaji mkubwa wa wapiga kura kuliko chama kingine chochote ndani ya umoja huo hivyo kilipaswa chenyewe kiungwe mkono na wala sio kiunge mkono, kazi ambayo CDM ingepewa na umoja huo ni kutafuta na kuleta mgombea ambae anakubalika na makundi yote ndani na nje ya UKAWA.

CUF wakiongozwa na dhana ya kuwa sisi tuna mgombea bora kuliko vyama vingine itakuwa na taathira kubwa katika siasa za UKAWA ni maoni yangu kuwa CUF inaihitaji sana CHADEMA kushinda majimbo mengi ya ubunge bara kuliko CHADEMA inavyoihitaji CUF, Vivyo hivyo kura za wafuasi wa CHADEMA hata kwa uchache gani zitakuwa muhimu sana kuamua hatma ya Urais wa Zanzibar katika uchaguzi ujao, kwa ufupi CUF inaihitaji zaidi UKAWA kujiimarisha katika siasa za Tanzania bara.

Nimeongea na baadhi ya viongozi waandamizi na wanachama wa kawaida ndani ya CUF, wengi wao wamejaa na dhana kuwa CHADEMA iliwasaliti kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, hoja hii haina mashiko kwakuwa ukiangalia takwimu za chaguzi zilizopita za serikali ya mitaa CUF imepata viti vingi vya vijiji, vitongoji na mitaa kuliko chaguzi zilizotangulia,hii ni kusema kuwa CUF imeimarika zaidi ndani ya UKAWA kuliko ilivyokuwa nje ya UKAWA, hoja hii ni kweli kwa vyama vyote vinavyounda umoja huo. Hapa ninaunga mkono maneno yalisemwa bungeni wiki iliyopita na mbunge wa kilwa kusini(CUF) Selemani bungara maarufu kama "-----" kwa kauli yake kuwa viongozi wa UKAWA wakikubali umoja huo uvunjike watakuwa ni wanafiki kuliko CCM na ni wasaliti

Hapo ndipo ninapoiona dhima ya viongozi wawili wanaotajwa kuwania Urais kupitia umoja huo Dr. Slaa na Prof. Lipumba kuwa ni muhimu kuliko wakati wowote toka uanzishwe umoja huo, Lipumba itabidi awe na chaguo moja, kuwapuuza wahafidhina ndani ya chama chake hivyo kukiimarisha zaidi chama chake au kuwakubalia hivyo kukidhoofisha zaidi chama chake (kwa kuwa vyama vingine vitakataa CUF watoe wagombea Urais SMZ na SMT) hivyo kuvunjika rasmi kwa UKAWA, DR. Slaa atakuwa na kazi kubwa ya kuchagua ima akubali kujiweka pembeni hivyo kuwakatisha tamaa wafuasi wengi wa CDM na kumuunga mkono mgombea mwingine (kwa hili CHADEMA itadumaa) au au CDM iingie yenyewe katika uchaguzi mkuu (hili likitokea CDM itabaaki palepale, haitashinda Urais na idadi ya wabunge itapungua au kuongezeka kidogo mno)

Kwa kuhitimisha ni vizuri tukaitaja nafasi ya mwenyekiti wa NCCR Bw. James Mbatia, huyu ni mtu muhimu sana kwa vile anayajua mahitaji ya sasa ya kisiasa na mtu anayefuata political realities, ni mategemeo ya wapenda siasa za ushundani kuwa atakuwa ndio political stabilizer ndani ya UKAWA. Tanzania inahitaji ushindani mkubwa wa kisiasa kwa kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

KABLA YA YOTE KUMBUKA UKAWA NI KIMBILIO LACDM BAADA YA MVURUGANO NA ZITO
HIYO KWENYE
RED NDO UKWELI WENYEWE KWANI KATIKA KATA NINAYOKAA MIMI TUMEKOSA MITAA MITATU KWA UBISHI WA VIONGOZI WA CDM PIA SEHEMU AMBAYO CUF HAWAKUWA NA NGUVU HAWAKUTHUBUTU KUWEKA WAGOMBEA LAKINI CDM WALIFOSI MFANO NI KATIKA MITAA YA KATA ZA BUGURUNI NA VINGUNGUTI LAKINI CUF WALIIBUKA KIDEDEA

NA HIYO KWENYE BLUE YA KWAKO NDO HAINA MASHIKO
CUF NDO ILIKUWA INAONGOZA KUWA NA VIJIJI NA MITAA MINGI BAADA YA CCM KWA HIYO CDM NDO WANUFAIKA WAKUBWA NA UKAWA

Mwishokuna watu wengi nimewasikia wakishauri
NLD itumike kama chama cha dharura kuokoa umoja huu kwa kupewa nafasi ya urais kama KENYA , MWAI KIBAKI alitokea katika chama kidogo na vyama vikubwa vikamsapoti,wapo watu kutoka CCM wanataka kuipa kura ukawa wanashindwa kutokana na UCDM na UCUF
 
Wasiwasi wa nini kama alivyosema Mwenyekiti mwenza wa Ukawa Mzee Makaidi jana. Yeye kasema wao wanajua mgombea ni nani hivyo sie tusubiri tuu. Sasa hivi tuwaachie VIBAKA ( according to Makongoro) waparurane kwanza na kutangazana uchawi kisha sie tuone nani atatokeza mwisho.
 
Sikubaliani na wewe kuwa CUF ndio wanamgombea bora kuliko wenzake. Hakuna kitu chochote cha kimaendeleo cha mfano wa kuigwa alichokifanya cha kututhibitishia kwamba ndiye bora. Kwa mtazamo wangu nadhani Dr. Slaa ndiye kiongozi bora zaidi, ameonyesha kwa mifano alipokuwa mbunge wa karatu, jimbo lilipata maendeleo ya ghafla kwa kipindi kidogo kuliko mudawote tangu tanzania ipate uhuru. Pia alivyokuwa bungeni alikuwa mstari wa mbele kufichua walarushwa jambo ambalo ni tatizo pia katika uongozi wa nchi yetu.
 
Wacha uongo wewe, sisi sio watoto. Sasa ivi CDM imeenea kwa asilimia kubwa sana tanzania bara kuliko CUF kwa hiyo hata kwenye maeneo ambayo CUF ipo, bado CDM inanguvu vilevile na ndio maana unaona nao walikuwa wanasimamisha mgombea, na ndio maana utaona walikuwa hawapishani kwa wigo mkubwa. Huo mfano wako wa Mwai kibaki ni irrelevant kwa sababu hatakama Mwai kibaki alikuwa anatokea kwenye chama kidogo vipi, lakini alikuwa ni mtu anaye fahamika sana kwani alikuwa kwenye uongozi wa KENYA tangu enzi za KENYATTA, kwahiyo usifananishe na NLD
 
Kutangaza nia kwa Prof. Lipumba siyo tatizo hata kidogo. Ikumbukwe kwamba Prof. ametangaza nia ya kuiwakilisha CUF kwenye UKAWA. Vivyo hivyo vyama vingine navyo vitachuja watangaza nia wake kwa taratibu walizojiwekewa.

Mtangaza nia mmoja kutoka kila chama kinachopenda kufanya hivyo, atashindanishwa na waombaji wa kutoka vyama vingine vya ukawa. Na hapo kwa kufuata makubaliano yao, na taratibu walizojiwekea, UKAWa watampitisha mmoja ambaye ndiye atakayepigiwa kampeni na vyama vyote vya UKaWA.

Hili litafanyika tu hatuna haja ya kuwa na wasiwasi.

Prof. Lipumba ni msomi mzuri na anaelewa masuala yote kwa undani. Inahitaji utashi ambao tayari anao wa kuwatayarisha wapenzi wake kuyapokea mapendekezo ya UKAWA kwa maslahi ya taifa kwa sababu hata kama akingombea hawezi kuchaguliwa kuwa raisi wa nchi kwa sasa kutokana na sababu kwamba chama chao kinanguvu sana Zanzibar lakini hakijajiimarisha kiasi hicho huku bara.

Hakuna sheria inayosema baraza la mawaizir lazima watoke chama kimoja!. Hii ni kitu mazoea inayoonekana kama sheria.

Tunahitaji serikali Imara yenye watu safi wenye moyo thabiti, uwezo mpana na nia iliyo safi ya kuwatumikia Watanzania ili kuwapa kile wanakiota walichonyimwa na ccm kwa muda mrefu.

UKAWA TU NDIYO WANAWEZA KUFANYA HAYA NA SI WANAFIKI CCM WASIO KUWA NA HAYA.
 
Umemjibu vizuri sana Mkuu. Watu wanatabia ya kutoa mifano ambayo wala haina uwiano na hali iliyopo.

Wacha uongo wewe, sisi sio watoto. Sasa ivi CDM imeenea kwa asilimia kubwa sana tanzania bara kuliko CUF kwa hiyo hata kwenye maeneo ambayo CUF ipo, bado CDM inanguvu vilevile na ndio maana unaona nao walikuwa wanasimamisha mgombea, na ndio maana utaona walikuwa hawapishani kwa wigo mkubwa. Huo mfano wako wa Mwai kibaki ni irrelevant kwa sababu hatakama Mwai kibaki alikuwa anatokea kwenye chama kidogo vipi, lakini alikuwa ni mtu anaye fahamika sana kwani alikuwa kwenye uongozi wa KENYA tangu enzi za KENYATTA, kwahiyo usifananishe na NLD
 
Hivi UKAWA kama watampitisha dr. Slaa na kweli wakafanikiwa kushinda uchaguzi katika uundwaji wa baraza la mawaziri kwa mujibu wa katiba ya sasa mawaziri lazima watoke chama alichotoka rais sasa je UKAWA inatambulika kama chama? Na kama haitambuliki kama chama itakuaje katika muundo wa serikali yao ? Vyama vingine vinavyounda ukawa vitashirikishwaje katika serikali ijayo kwa mwenye kujua naomba anijuze.
Bojan , Katiba haisemi ni lazima Mawaziri watoke chama kimoja na rais, ila inasema Waziri lazima awe mbunge. Hivyo mawaziri wa UKAWA watatoka kwa wabunge wa vyama vyote. Na hata kama watataka kuchagua mbunge kutoka ccm watakua hawajavunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi wako
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom