Wakati Dr Slaa anajiunga na CHADEMA alikuwa ametokea CCM. Na kabla ya kujiunga na siasa inasemekana alikuwa anakabiliwa na tuhuma mbaya za kimaadili zinazodaiwa kuwa ndio chanzo cha yeye kuondoka kwenye utumishi wa kanisa. Haijathibitishwa lakini sababu inayotajwa kuwa Dr Slaa alishindwa katika kutii kiapo cha useja……..kwa maana nyingine alikiuka kiapo cha maadili ya upadre. Mimi sifahamu ukweli wa jambo hili, lakini habari zilizopo ndio hizo.
Dr. Slaa baadaye akajiunga kugombea ubunge kupitia CCM ambako huko ALIKATWA. Sababu kubwa iliyopelekea jina la kukatwa inasadikiwa kuwa ni tuhuma hizo za kimaadili. Ilionekana isingekuwa vyema yeye kupeperusha bendera ya ubunge katikati ya tuhuma hizo. Baada ya kukatwa alihamia CHADEMA ambao walimpokea kwa mikono miwili na kusema maadamu yeye anakataa tuhuma hizo wao CHADEMA ni nani hata wamhukumu? Alipokelewa na alishinda ubunge na ikiwa ndio mwanzo wa safari ya Dr Slaa kisiasa.
IKumbukwe Dr Slaa hakujiunga CHADEMA kwa kuvutiwa na sera zake, mikakati au jambo lolote, lengo lake ilikuwa ni KUTAKA UBUNGE basi. Laiti asingekatwa na CCM labda asingejiunga na CHADEMA. Dr. Slaa bila shaka alikuwa ni kada wa CCM, lakini CHADEMA iliweza kumbadilisha kutoka ukada wake na kuwa mwiba mkubwa kwa CCM. Lowasa amejiunga na CHADEMA kwasababu tu alikatwa. Amejiunga CHADEMA akiwa katika ya tuhuma za Richmond, ambaye kama Slaa anakataa kuwa hausiki nazo tuhuma hizo.
Leo Lowasa isingekuwa kukatwa na CCM labda asingejiunga na CHADEMA. Lowasa hajavutiwa na sera, wala mikakati ya CHADEMA ila tu kwa vile amekatwa. Kama CHADEMA walivyosema kwa Dr Slaa kuwa tunamuachia Mungu mwamuzi wa haki, ndivyo walivyofanya pia kwa Lowasa. Kama CHADEMA wanavyojinadi kuwa walianza na Mungu, basi wana uhakika mkubwa kuwa kama vile Dr. Slaa kukatwa na CCM kujiunga na CCM ilikuwa mpango wa Mungu, basi kwa njia ile ile hata Lowasa kuja CHADEMA ni mpango wa Mungu.
Tafakari ya mchunguzi huru