Hawakukaidi isipokuwa walikubali kusitisha kwa makubaliano ili sherehe za nanenane zipite, migomo ya waalimu itatuliwe, na hofu ya CCM kuaibishwa nyakati hizo...hivyo operesheni hiyo ikapata baraka kuanza baada ya mambo hayo matatu...Halafu kwa taarifa tu, hiyo haikuwa amri" halali" bali ilikuwa amri "kandamizi" chini ya mwavuli wa CCM.
Ushahidi huu unapatikana alipoulizwa Msajili wa vyama vya siasa nchini ndg;John Tendwa, kuhusu uhalali wa jeshi la polisi kupiga marufuku mikutano hiyo...majibu yake ni kuwa, polisi wasome alama za nyakati katika katiba inasema nini, na chadema wasome kilichoandikwa humo kila mtu atajua alipaswa kufanya nini.
Mtazamo wangu kuhusu hilo ni kwamba: Msajli wa vyama John Tendwa alimaanisha Polisi hawakusoma alama za nyakati katika "msahafu"huo unaoliongoza taifa hili, jambo ambalo ndio lilisababisha mambo yote "kufikia hapo yalipo".
Ushari wangu kwa polisi:Ni vizuri kama polisi wetu wangesoma sheria kwanza kuliko kuvamia mambo bila kujua nini hatima yake, Pili Serikali iwapatie polisi wote nchini nakala ya katiba, ile kuukuu na hata hii mpya tunayoitarajia wapewe zote kwa kugawiwa...hili liwe la lazima ili waujue ukweli wa mambo
Poleni polisi, hongereni Chadema