Dr. Slaa kesho atasema nini?

Critical thinking is the missing course in our college curriculum that is why most chase a followers. Your leaders might be wrong. Learn to think for yourself.
 

Hoja zako dhaifu sana. Dr Slaa amekuwa akiishi na ameendelea kuishi kwa kuamini Lowasa ni fisadi na hajawahi kubadili msimamo huo. Na alikubali ujio wa Lowasa kama mwanachama na kuna masharti alitoa kama katibu mkuu likiwemo la yeye mwenyewe kujisafisha hadharani jambo ambalo hata moja halikufanyika! Sasa huu upotoshaji unaouleta humu ni siasa nyepesi zisizo na tija kwa kuukwepa ukweli ulio dhahiri kuwa Lowasa bado ni Fisadi na huo ndio ukweli anaouishi Dr Slaa.
 
Nadhani atawananga hawa wafuatao
1.Mkewe Rose Kamili
2.Wanawe
3.Mbatia
4.Lowassa
5.Viongoz wa dini
6.Watanzania wanaotaka mabadiliko
7.Waandishi wa habari
 
Hiki kizee kinakoelekea kitaokota makopo,yaani kinapayuka tu hovyo hovyo.Kwa taarifa yenu ccm sasa basi,wametudanganya vya kutosha, tucheki na chama kingine.
 

Je kuhusu kikwete slaa anamuwazaje?
 

Great Thinkers mpo wachache sana.
Wengine ni washabiki tu wanaoshabikia wasivyovielewa.
 

Ahsante.
 
mi nimemuelewa sana Dr, Hajasema uchague ccm bali yeye haamini ktk fisadi lowasa.
yeye ndiye aliyetufungua macho juu ya ufisadi na ubaya wa ccm...
kubwa zaid ni list of shame, ufisadi wa lowasa... leo iweje mtu huyo huyo mwenye akili timamu amsafishe mtu huyu/??
ni unafiki ambao mm siukubali... Generally, CHADEMA dissappointed me,siamini ktk lowasa ambao wao walinambia hafai hafai, leo tena anafaa
NEVER
 
Kwa Thread hizi kweli CHADEMA mpo vizuri kwa Propaganda.
Mlimtukana sana Zitto.
Leo mmegeukia kwa Dr. Slaa
Sitawashangaa siku mkijitukana wenyewe.
Niliipenda CHADEMA ila kwa siasa hizi za kuchafuana mmh...
 
ZOEZI LA UUZWAJI WA NYUMBA LILIFANYIKA WAKATI WA UONGOZI WA AWAMU YA TATU.... 1995 - 2005
AZIMIO LILIPITISHWA NA BARAZA LA MAWAZIRI LILIOKUWA LIKIONGOZWA NA MALAMKA YA WAZIRI MKUU Ndugu FREDRICK SUMAYI.... Pamoja na yeye alikuwepo Waziri Mkongwe Lowasa ( alikuwa na uzoefu wa kufanya kazi ndani ya Serikali ya ccm kwa miaka 30) na Waziri asiye na uzoefu wa muda mrefu serikalini Ndugu John Pombe ( alikuwa na uzoefu wa miaka 5)
Natumain nimekusaidia Ndugu!
 

Jamani ifike mahali tukawa wazi tu kuwa dr slaa anatumiwa na ccm..kakatiwa mkwanja...amenyan'ganywa tonge mdomoni..kimada wake ndo mwenye maamuzi ya mwisho katika familia yao! Anakaa serena hotel a 5 ¤ hotel..analindwa na usalama wataifa24/7..that's incredible! Kama alivyosema naye ni binadamu ana moyo. .kuwa ni kweli kaumia sana kunyan'ganywa kugombea dkk za mwisho....kimada wake is the one who is running the show..alimtupia nguo zake nje na kulala kwenye gari..toka siku ile hakutoka tena!..strange! Ku sum up. .issues ya lowassa fisadi hapa haipo maana huko alipo au washika dau wake wapya ndo wachafu zaidi..hadi akajichanganya na kuifananisha ccm na choo! Ile list of shame ilikuwa na watu 11 katoka moja tu wengine wote wapo huko aliko hivi sasa..tafadhali tusipotoshe wapenda mageuzi kwa interest za pande tunazozishabikia!
 
Yaani kama kuna mtu anayejisahau na Dr.Slaa akiwemo kwamba watanzania hawajui lolote Kuhusu Richmond anajidanganya.Ndugu zangu Watanzania wa leo sio wale uliowaona jana wasiojua lolote ,hawa wa leo ni balaa kabisa wanajua wapi Richmond ilianzia na mpaka sasa mwenye Richmond yake ameshajulikana,Hivyo unayetaka Lowasa ashitakiwe unajifanya kuvaa tintedi eti humjui mwenye Richmond ww endeleza ngonjera zako SISI haturudi nyuma achaneni na hiyo kitu mtaongea sana mwisho mtapasuka midomo SISI haturudi nyuma LOWASA ndio habari ya mjini na inaitwa ALUTA CONTINUE.
 
Dr. Slaa amejimaliza mwenyewe kwa sababu anazo zijua yeye mwenyewe,tumuache apumzike kwa amani. Hana jipya tena ni mtu wa kutumiwa na maboss wake CCM kama doli la mtoto!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…