The Khoisan
Platinum Member
- Jun 5, 2007
- 18,922
- 18,803
Kwanza hizo ofisi wanazo? Kipindi cha uchaguzi mwaka jana nilibahatika kuwa mkoani Kilimanjaro, nikabahatika kutembelea kata ya Korongoni kujionea mchakato wa uchaguzi, kwa macho yangu nilimuona bwana Ndesamburo akifungua ofisi ya tawi ya CDM katika mtaa wa Wireless kwenye duka la mtu nilishangaa sana, dukani kwa mtu unafungua ofisi ya chama kikubwa kama CDM?
Taarifa nilizopata ni kwamba duka hilo limefungwa kwa maana mtaji umekwisha je na ofisi bado iko? Na nini mpango uliopo? Kimsingi CDM wanapaswa kujijenga kwa sasa na si kujibizana na CCM, huwezi ku-assume kwamba utachukua nchi ili hali huna ofisi za kutosha!
CDM itumie rasilimali watu iliyo nayo kuchangia gharama za ujenzi wa ofisi ama kukodisha majengo mbalimbali, hamuwezi kujifanya mnaipenda CDM wakati mnakuwa wagumu kuichangia! You must change

Bado wachangiaji hamjaniridhisha kiu yangu kuhusu utaratibu gani muafaka utumike ili watu wanaotaka kuwa wananchama wa CDM wataweze kupata kadi kama wengi wetu tunadhani kuwa na ofisi is a bit expensive. Can IT experts suggest an online registration facility? Vipi kuhusu CDM kuwa media firm yake ikihussha Radio, TV, magazeti na IT forums ambapo wapenzi na wanachama tutaweza kununua hisa pia?
with online registration naona ni mapema mno,wafuasi wengi wa cdm ni watanzania waliochoka na maisha na wengi wao ni masikini wakutupwa ambao kuafford gharama za internet ni kazi sana labda watumie teknolojia ya simu lakini hii unaweza kuwa na wafuasi wengi lakini monitoring itakuwaje? tutake tusitake lazima kuwe na ofisi,wanachama wa eneo lile wakutane wapange mikakati mbambali ya kuimarisha chama,narudia tena siasa siku hizi ni proffesional activity bila kuindesha kisayansi cdm itakwama,huwezi kujivunia umati wa watu ambao wengine hawajui sera za chama kimsingi mabadiriko lazima yaanzie kwenye grass root
Mimi nafikiri Mada hii ni Muhimu sana kwa wanachadema, Mawazo yangu;
1. Kila operation Sangara inapomalizika ni jukumu la wakazi wa eneo husika kuanzisha tawi kama wameshawishika na kukubaliana na sera, wao watachagua viongozi wa tawi na kuwasilisha majina makao makuu, na ndipo viongozi wa wakuu wa chama watakwenda kuzindua tawi rasmi na kugawa kadi kwa wanachama wapya, na pia kuacha kadi kwa ajili ya kugawia wanachama watakao jiunga baadae, viongozi watabuni miradi ya kuendesha office wakisaidiwa na makao makuu.
2. sisi vijana ambao wengi wetu asili yetu ni mikoani tuanzishe utaratibu wa makusudi kutembelea babu zetu na ukifika huko kama wewe ni wanachama wa Chadema na unao uwezo wa kujenga nyumba, jenga huko na utenge chumba kimoja kwa shughuli za chama, wasiliana na makao makuu utambulike na uanze kufanya shughuli za chama kwa kusimika viongozi. ukiweza kwenda hata mara mbili kwa mwaka inatosha kuhamasisha na utapata watakaokuunga mkono,
ni mtizamo wangu tu.