Dr. Slaa, chagua maneno...

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,279
Reaction score
7,681
Dr. Slaa ni mwanasiasa mlaghai.

Siku za hizi karibuni Dr. Slaa amekuwa akisema maneno bila kupima maana na ujumbe unaobebwa na maneno hayo.

Matokeo yake, Dr. Slaa amekuwa sababu ya mitafaruku kutokana na kauli zake.

Hali hiyo tuliishuhudia hata hapa JF ambapo sasa hivi Dr. Slaa anapaogopa kama ukoma kutokana na wadau kuwa wakali kwa kauli zake.

Kiujumla kauli za Dr. Slaa huwa zina madhumuni ya kuwalaghai wale watakaozisikia. Hata hivyo Slaa anapaswa kupima kiasi cha ulaghai anachokitumia kwa sababu sasa ameanza kupitiliza.

Akitoa salam za rambirambi kwa kifo cha aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini na Kiongozi wa ANC Mzee Nelson Mandela, Dr. Slaa ametamka kuwa matendo ya serikali ya CCM ni sawa na mfumo wa apartheid wa makaburu wa Afrika ya Kusini.

Kauli hii iliyolenga kulaghai watu (kwa sababu Slaa anajua kuwa anachosema sio ukweli au more correctly ni uongo) ina madhara makubwa kwa namna mbili.

Kwanza ni kupunguza uzito wa mateso waliyopata watu weusi wa Afrika ya Kusini, ambao hata kupiga kura walikuwa hawaruhusiwi. Slaa anaposema kuwa maisha ya watu wa Afrika ya Kusini kipindi cha ubaguzi wa rangi ni sawa na maisha ya watanzania wa leo chini ya serikali ya CCM anamaanisha kwamba watu weusi walikuwa wanalalamika bure bila kuwa na sababu ya msingi. Hapohapo anasahau kuwa yeye, Slaa, hajafungwa kama Mandela na wanasiasa wengine wa Afrika Kusini. Slaa anapata ulinzi wa polisi, anagombea Urais na kufanya kampeni kwa uhuru, lakini kwa vile tu ameshindwa kupata kura za kumfanya awe Rais, basi anaona hiyo ni kero sawa na apartheid!!!

Katikia hili Slaa, pengine bila kujua, anajiunga na wale wanaomuweka Mandela kwenye kundi la magaidi wasiostahili heshima yoyote. Katika mtandao wa CNN kuna wachangiaji wengi wenye mrengo huu wa Dr. Slaa. Mifano yake ni hii hapa chini.

JimmyBoston • 2 days ago


Mandela is dead. What scares me the most is the people on this board, left leaning liberals, who find the murder of innocent people, going about their daily business, as acceptable to promote a Socialist cause. It sickens me.


Confucius Say • 2 days ago



Whatever Mandela's reasonings, and they are questionable, his methods were criminal. He gave orders to plant I.E.D's and they killed innocent people. Women and children. Over 80% black. How can we be so blind as to forget that? Whatever the cause the means were beyond wrong and to celebrate this man is a shame. To simply gloss over or completely ignore this is atrocious. Church Street Bombings, look it up people. Stop drinking the Kool Aid and do some research.


Kwa mifano zaidi ya comments zinazofanana na hiyo na ya Dr. Slaa soma hapa http://edition.cnn.com/2013/12/05/world/africa/nelson-mandela-
humor/index.html#disqus_thread


Wenye maoni ya namna hii, yanayofanana na kile alichosema Dr. Slaa, ni watu ambao wanadhani mfumo wa ubaguzi wa rangi (apartheid) unaweza kufananishwa na maisha ya kawaida ya mtanzania wa leo, kama jinsi alivyofananisha Dr. Slaa. Pengine tunaweza kumvumilia hawa wamarekani walioandika hivyo kwenye mtandao wa CNN kwa vile hata ukiwaonyesha ramani ya dunia wanaweza kupata shida kuonyesha Afrika ya Kusini iko wapi kwenye ramani hiyo. Tatizo ni pale mwafrika mtanzania mwanasiasa wa ngazi ya kitaifa anapofananisha ubaguzi wa rangi wa Afrika ya Kusini na maisha ya mtanzania wa leo!!!

Wamarekani hawa wanafananisha mfumo wa apartheid na changamoto wanazokutana nazo kila siku kwenye maisha yao ya Marekani ya leo. Slaa anafananisha mfumo wa apartheid na changamoto za kisiasa anazokutana nazo katika maisha yake ya Tanzania ya leo. Slaa na wachangiaji hawa wote WAMEPOTOKA...

Tatizo la pili katika kauli ya Dr. Slaa ni kwamba inawasafisha makaburu mbele ya macho ya vijana wa leo. Unapomwambia kijana wa kizazi cha sasa kuwa mfumo wa ubaguzi wa rangi, apartheid, ulikuwa ni sawa na jinsi CCM inavyoongoza Tanzania, unampa ujumbe kuwa apartheid was not a problem. Mbaya zaidi ni kwamba unatoa ujumbe, pengine bila kujijua, kuwa apartheid ilikubaliwa na watu wengi.

CCM imekubaliwa na watanzania wengi kwa njia halali ya kidemokrasia ambapo kila aliyekidhi vigezo vya kikatiba kupiga kura aliruhusiwa kupiga kura.Vigezo vya kikatiba vya kupiga kura Tanzania havikutenga walio wengi ili wasishiriki kwenye kuchagua vionngozi. Vilevile, wale wote waliokidhi vigezo vya kugombea, akiwemo Dr. Slaa, waliruhusiwa kugombea. Katika Afrika Kusini ya apartheid, hali haikuwa hivi.

Pamoja na kwamba Slaa amebobea kwenye siasa za kilaghai, lakini sasa amefikia hatua anapaswa kuchagua maneno ya kusema. Slaa asiwe TOO DESPERATE kwenye kutaka kuwafanya watanzania waichukie CCM kiasi cha kutoa kauli za kukejeli harakati muhimu kama alizofanya Mandela za kupiga vita ubaguzi wa rangi.

Dr. Slaa anapaswa kujipima na kuomba radhi kwa kauli hii aliyoitoa. Vilevile anapaswa kuchagua maneno ya kusema katika siku zijazo...

Tafakuri: Katika taarifa yake ya kujiuzuru, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi, alikiri kushirikiana na Dr. Slaa kufanya mikakati mizuri na mibaya kwa nchi yetu. Je, Slaa amekuwa akihalalisha mikakati hiyo mibaya kwa kufananisha na jinsi ANC ilivyolazimika kutumia mikakati ya namna hiyo kupiga vita apartheid?

Rest in Eternal Peace Nelson Mandela...
 
Ukiendekeza ubaguzi wowote wewe ni Kaburu tu!

Kama watu weusi kutupiwa ndizi na wazungu tu inapigiwa kelele kuna tofauti na udini,ukanda mnaoneza makusudi?

Nyie ni makaburu tu!
 
Kuitumia Taaluma ya Udaktari kisiasa ni majanga sana.
Ninaamini wazazi wako wanasikitika sana......
 
Ukiendekeza ubaguzi wowote wewe ni Kaburu tu!

Kama watu weusi kutupiwa ndizi na wazungu tu inapigiwa kelele kuna tofauti na udini,ukanda mnaoneza makusudi?

Nyie ni makaburu tu!

Kwahiyo unaunga mkono kauli ya Slaa kuwa apartheid ni sawa na mfumo tulio nao?

If yes, je utaunga mkono matumizi ya matendo ya kigaidi kuuondoa huu mfumo uliopo Tanzania?

If no, je una tofauti gani na comments hizo kutoka CNN?
 
Kuitumia Taaluma ya Udaktari kisiasa ni majanga sana.
Ninaamini wazazi wako wanasikitika sana......

Udaktari ni taaluma adhimu, lakini ni kwa madaktari ambao walikuwa hawakariri, ukishakariri tu kwenye udaktari utaikimbia profession, sababu vifo vitatawala wodi yako.
 
Unafahamu kitu kinachoitwa point of view? Slaa, kama wewe, ana haki ya kutoa mtazamo wake. As long as hujaamrishwa kuafikiana nae, sanasana makala yako ndefu ni sehemu tu ya harakati za kuhalalisha hiyo posho mnazolipwa na CCM.

Apartheid ulikuwa mfumo wa kibaguzi kwa misingi ya rangi, sawa kabisa na mfumo wa kibaguzi unaitafuna Tanzania yetu ambapo genge dogo la mafisadi linakandamiza haki za walalahoi walio wengi.
 
“Sasa unaachaje kumsikiliza huyu na ukamsikiliza zaidi mtu ambaye hana sifa za kimageuzi katika ngazi ya kitaifa? Wanaozua tuhuma dhidi ya wenzao hawana hata miaka mitano ndani ya chama?
“Labda nikupe mfano mzuri. Hivi unategemea leo, CCM kwa mfano, eti akina Richard Tambwe Hizza, waanzishe mkakati wa kumng’oa kwenye chama mtu kama Kingunge Ngombale Mwiru kwa madai ni msaliti? Haya mambo yako CHADEMA tu,” alisema mwanasiasa huyo
 
Babu ameishiwa meno, kwa hiyo tusimulaumu kwa kuwa anatumia maneno ambayo yanakuwa rahisi kutamka na kusikika!
 
Slaa siku hizi hatishi wakawaida tu yan mwepesi,hana lolote kadharaulika sana,mpaka 2015 ataacha siasa ataanzisha Kanisa lake.
 

Sijamkataza Slaa kutoa maoni yake.

Hata hivyo Slaa kama kiongozi wa chama cha siasa, maoni yake hayabaki kuwa maoni tu hewani. Yanaweza kuwa na impact kwenye maisha ya watu.

Nakumbuka hata Mzee Mtei alipotoa kauli ya kibaguzi mlisema ana haki ya kutoa maoni yake. Well, hatukatazi mtu kuwa na maoni yake ndio maana wako huru na hiyo pia ni tofauti kati ya apartheid na nchi yetu. Lakini kila anayetoa maoni inabidi kupima kile anachosema kina madhara gani kwa jamii.

Kauli ya Slaa haiendani na nafasi yake kwa jamii...
 
Jana nilikuwa kwenye basi natoka Dodoma kuja Dar, kuna akina mama walikuwa wanakiri kuwa Slaa mtu mbaya sana kwa kauli zake tofauti na kazi aliyoitumikia awali.

Sasa nimeanza kuamini huyu Mzee amechanganyikiwa.
Ukiona umeanza kufikia kiwango hicho cha kukosa break ya ulimi basi ujue na break za maumbile mengine zimekata.

Suluhusho ni kustaafu tu ili usiendelee kujikojolea hadharani.
 
Kwahiyo unaunga mkono kauli ya Slaa kuwa apartheid ni sawa na mfumo tulio nao?

If yes, je utaunga mkono matumizi ya matendo ya kigaidi kuuondoa huu mfumo uliopo Tanzania?

If no, je una tofauti gani na comments hizo kutoka CNN?

tatizo neno au tatizo ni ubaguzi?CCM imeweka matabaka.hata wabunge wenu jana wamekili kuna vidume halmashauri haviguswi kisa wana watu mawizarani
 
Viherehere ndo vinasababisha mnatiwa mimba, ukila jiandae kuliwa,mnawaza kwa kutumia makalio, hizi indo kauli tunazopenda kuzisikia
 

Wananchi wameanza kuona true colours za Slaa...
 

Pumba!!!

Makaburu waliua waandishi wa habari na watetezi wao(Steveen Biko)Serikali ya CCM inaua na kutesa waandishi (Mwangosi)

Makaburu utendaji bora wa vyombo vyake vya dola ulikuwa unapimwa na ukatili wako kwa blacks na waliofanya hivyo walipandishwa vyeo ili kuhamasisha wengine waige,CCM na serikali yake weledi wa vyombo vyake vya dola unapimwa pia na ukatili wao kwa wapinzani na ukiua ni moja ya sifa kupandishwa vyeo (RIP Kamuhanda na CP Andengenye)

CCM na serikali yao wana sifa zote za makaburu!
 
tatizo neno au tatizo ni ubaguzi?CCM imeweka matabaka.hata wabunge wenu jana wamekili kuna vidume halmashauri haviguswi kisa wana watu mawizarani

Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi wakati anajiuzuru alisema kuwa ameshirikiana na Slaa kufanya mikakati mbalimbali mizuri na mibaya kwa taifa.

Pengine Slaa anaamini kuwa nchi yetu ina mfumo sawa na Afrika Kusini ya apartheid na anaamini kwamba matumizi ya kigaidi kuuondoa huu mfumo ni halali!!!
 

Div 5 ingine ya Mulugo hii hapa!
Dr Bilali awe wa kwanza kujiondoa madarakani kwa ukikongwe wake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…