Dr. Slaa alitushauri wa-TZ tukampuuza, sasa kulalama kwanini?

Status
Not open for further replies.
Papa D na Wana JF
Usemayo yana ukweli, tunavuna tulichopanda, unajua kila kitu kinaanzia na Mind Set ya Mtu, mimi naamini kabisa everything happen for the reason, hapa Mungu anatuonyesha na kutuonyesha njia halisi ya kutokea. Haya yoote ni Ishara tosha na ni kama wake up call
tunatakwa kujua tatizo ni nini hasa ??? ni system yetu ??? ni kulindana kwetu ??? ni katiba yetu ??? ni tume yetu ???? ni viongozi wetu ??? ni sisi watanzania ??? ni sheria zetu ???
ukishapata jibu hapo hatua ya pili nini kifanyike ???
sikio la kufa halisikii dawa, ila ipo siku yaja watanzania wakifunguka macho, watakuwa na hasira na hawa magambaz
My take: Mimi naona tatizo kubwa ni ELIMU, sio watanzania hatuna Elimu, hapana. Ni Elimu ya Uraia ya kila mtanzania kujua haki na msingi yake na katiba ya Nchi




Wakti wa kampeni za urais Dr. Slaa alitushauri waz-tz tusimchague JK. na kama hatumtaki yeye basi angalau tuchague hata Li-PUMBA! na endapo tutamchagua JK basi tutambue tumeingia katika matatizo.
hivi sasa petrol shida, umeme shida, shilingi inaekea kaburini, sukari usiseme,
Je kwa nini tusimwite Dr. Slaa kuwa ni mtume/nabii?
 
Hivi mnaong'ang'ania Dr. Slaa aliiba mke wa mtu je nani anamwanamke wake ilihali wanawake wote wanaolewa tayari walishakuwa na flani acheni kufikiri kama kuku.
 
Hivi mnaong'ang'ania Dr. Slaa aliiba mke wa mtu je nani anamwanamke wake ilihali wanawake wote wanaolewa tayari walishakuwa na flani acheni kufikiri kama kuku.
Futa usemi wako. Siyo wanawake waote wanaoolewa walishakuwa na watu kabla.
 
Tuwalaumu wale waliomchagua pamoja na tume ya uchaguzi. Ingekuwa ikulu ni kupaka carolyt tu, JK angeweza kuiendesha nchi vizuri...!
 
Mimi nakumbuka Dr slaa alipokuwa anafunga anamalizia kampeni kwa mdahalo pale Movenpick 2010 alisema "kuendelea kuichagua ccm ni maafa" naya kumbuka sana maneno yake kila nikisikia watu wakilalamikia ugumu wa maisha na mfumuko wa bei.

hua inaniuma sana nikikumbuka mdahalo ule. We had a chance and threw it away
 
tuache lawama zisizo na msingi na sifa za kijinga.slaa hawezi kuwa nabii,ana usafi gani wakati amepora/anatembea na mke wa mtu pili hali ya uchumi kuwa mgum inasababishwa zaid na external force,uchumi wa mataifa makubwa km US na UK umeyumba na una direct impact kwetu.kwa hiyo acheni kuhadaa watu.

hapo kwenye bold mkuu, what of 'at least import/export control'? kwa nini serikali iruhusu ku-import mpaka sidiria na chup za mtumba ilhali kuna viwanda kama mbeyatex kilichogeuzwa yada/parking ya maroli ya tumbaku, ambavyo vingezalisha bidhaa mbadala za hiyo mitumba? huoni kuwa hiyo imepelekea katika deficit in balance of trade, na hivyo Tsh kuzidi kuporomoka, inflation kuongezeka, & apparently hali kuzidi kuwa mbaya! sasa Jk kama m2 aliseyesoma uchumi (sijasema mchumi, wala msomi wa uchumi) kwa nini asilaumiwe?

kwa nini kila siku wewe na vilaza wenzio wengi mnadanganywa na serikali kuwa kuporomoka kwa uchumi we2 source kumbwa ni external impacts? nilijisikia aibu sana pale naibu waziri wa fedha alipowatoa wasiwasi waTz eti kwamba kuporomoka kwa thamani ya Tsh hakuna madhara eti kwa kuwa huwa inatokea kwenye uchumi-hv anatofautishaje devaluation na deflation?

halafu wewe na wenzio wengi 2 mnataka 2simlaani jk na vilaza wake, kwani hawajui kuwa inflationary control measure mojawapo ni kuzuia importation ya vi2 tunavyoweza kuzalisha wenyewe kwa gharama ndogo kama nguo?

zile kodi walizo wasamehe wadosi waingiza sukari zisingeweza ku2mika kufungua mashamba mapya ya sukari na kupanua viwanda vya kagera na mtimba kufidia ile deficit ya 150000 tonnes?

hizo direct impact unazozisema, chanzo chake ni pamoja na importation ya kijinga ya vitu kama mitumba, steel wire, tooth picks, na siku hizi hata banzoka-kutoka china. hayo ni yale ambayo serikali ingeweza kuyafanya bila kuathiri shughuli zake za kifisadi kwenye madini, ardhi, mbuga, nk...................sikia dawa ewe sikio la kufa
 
tuache lawama zisizo na msingi na sifa za kijinga.slaa hawezi kuwa nabii,ana usafi gani wakati amepora/anatembea na mke wa mtu pili hali ya uchumi kuwa mgum inasababishwa zaid na external force,uchumi wa mataifa makubwa km US na UK umeyumba na una direct impact kwetu.kwa hiyo acheni kuhadaa watu.

Kana kwamba viongozi wakuu wa CCM hawa cheat wake zao. Hizo ni siasa za majitaka ambazo CCM wamekuwa mabingwa sana kuzitumia. Walitumia wakati Mrema alikuwa maarufu, na pia kambi ya JK ilitumia kumchafua Salim katika mchakato wa ndani wa CCM kumpata mgombea.

Hiyo hoja haina uhusiano na uwezo wa mtu kuongoza. Ndio maana hata Nelson Mandela, Winnie si mke wake wa kwanza, naye pia alimwacha na kuoa mwingine.

Ndio maana hata Wamarekani walikubali Clinton aendelee licha ya kashfa ya Monica Lewinski.

Kigezo hicho ungekitumia ukiwa na standard moja, hakika huyu aliyeko madarakani asingekuwepo
 
Ili mpewe suti na waarabu??

safari hii tumefunga mkataba makini. Kila mmoja atanufaika. Tunataka isiwe "Handsomeboy" pekee ndo anunuliwe suti, bali kila Mwananchi atanunuliwa Kanzu, Balaghashia na Mkongojo! Tutakuwa na uhakika wa kugawa bure tende na harua nchi nzima. Huoni kama hii ni mikakati makini?!
 
MwanaJF Hojatete,

Hizo lawama zisizo na Msingi ni zipi? Hizo sifa za Dr. Slaa zinazohusu kuchukua mke wa mtu zinahusianaje na ugumu wa maisha unaowakabili WaTz kutokana na Serikali kushindwa kutupatia umeme wa hakika kwa ajili ya factories zetu?

Ajira kwa vijana ni finyu kutokana na uzembe wa watawala wetu. Kuyumba kwa uchumi duniani hakukusababisha mabilioni ya TShillings kukwapuliwa toka BoT, ambayo yameingizwa ktk mzunguko wa fedha na kuleta inflation tuliyo nayo sasa.
Dr Slaa na chama chake wameongea tangu wakati wa Mwembe Yanga, kwa ni lazima hatua dhidi mafisadi zichukuliwe kama tunataka kuendesha mambo kwa ufanisi. Mambo haya hayana uhusiano wowote na Slaa kumchukua Josephine kama mke.

Muulize Gavana wa BoT sababu za huu mfumko wa bei. Atakuthibishia kwamba kiini chake kikubwa ni fedha zisizotokana na jasho zinazoingizwa ktk circulation na jamaa za kina Kikwete na mafisadi waliozagaa nchini kwa vile hawajachukuliwa hatua. Zilianzia pale Ballali alipokubali kutoa fedha za EPA kwa claimants feki kama Rostam Aziz na mafisadi wote wanaohusishwa na huo ukwapuaji.

Sababu nyingine za inflation hapa Tz ni uhaba wa chakula hasa ktk sehemu zilizokumbwa na ukame. Tatizo la njaa lingeweza kupunguzwa kama Serikali ilikuwa makini kwa kugawa kwa uadilifu mahindi kutoka Strategic Grain Reserve.

Sehemu ya inflation inayosababishwa na uchumi wa dunia kuyumba, ingeweza kushughulikiwa na Serikali makini kwa kuagiza BoT kutoa fedha za kigeni kwa wingi kuagiza mahitaji na kupunguza au kuondoa kodi ktk bidhaa husika. Serikali makini na adilifu ingewezekana tu, kama Dr. Slaa na Chadema wangechaguliwa.

Mkuu umeongea vitu ambavyo naamini vimetoka moyoni mwako. U a very right, Tatizo huyo hojatete unayemwelewesha huwa haelewi. Aliyoyandika ndo ukubwa wa upeo wake. Wanasema kwenye demokrasia inabidi tuheshimiane hata kama mwenzio anaongea pumba. Ndio upeo wake. Kama vipi kumbuka mdahalo wa MUUNGANO AND THE TANZANIA WE WANT ambapo JJ Mnyika alikuwa na Francis Stola wa TLS na MZee Seif Khatib. Mzee Khatib alikuwa anaongea upupu wakati weznie wanaongea critical issues ila moderator Ayub Ryoba alishauri watu wasimzomee Khatib bali wamvumilie maana ndo uwezo wake huo wa ufaham. Inakera bt ndo Watanzani8a wenzetu hawa. tuwazoee tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom