..tumeshapata kuwa na Mashekhe wabunge, mfano: Shekhe.Professor.Mikidadi.
..pia tumewahi kuwa na wabunge Mapadri, mfano: Yohana Misigila , wa Tabora mjini.
..Dr.Slaa aliwahi mwanachama na kiongozi wa CCM alipokuwa Rome, Italy.
..sioni sababu ya kumsakama mwanasiasa yoyote ile kutokana na imani yake.
..mbona sisi wengine tuna imani zetu na bado tunashiriki siasa?
Salimia said:
Kwani nini kilimtoa kanisani/madhabahuni na kukimbilia siasa? Je alifukuzwa huko kanisani? Na kama alifukuzwa kuna mwenye data ni kwanini? Au ni kiu tu ya kuwa RAIS? Au kuna zaidi ya hilo? Je kondoo wa Bwana walimshinda na sasa anataka awachunge watanzania? Na alipokuwa CCM alitetea au kusimamia msimamo huu huu alionao au? maana hatukumsikia wakati ule.
Salimia,
..Dr.Slaa ni mwanachama wa JF. haya maswali yako alishayajibu yeye mwenyewe zaidi ya mara moja.
..hakuna haja ya kusubiri kusimuliwa alichokisema wewe tafuta majibu ya Dr utayapata.
..Dr.Slaa aligombea ubunge wa Karatu kwa tiketi ya CCM baada ya kuombwa na wananchi wenzake waliokuwa wamechoshwa na mbunge wa wakati huo.
..Dr.Slaa alishinda kura ya maoni, lakini jina lake likakatwa na Kamati Kuu ya CCM, na badala yake wakamsimamisha Patrick Qorro aliyekuwa amechokwa na wananchi.
..baada ya matukio hayo ndiyo Dr.Slaa akajiunga na Chadema.