Dr. Slaa aibuka tena, ammwagia Magufuli sifa kede kede

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,417
Dr Slaa ambaye yuko nchini Canada Masomoni akisomea Psychology amefanya mahojiano na Gazeti la Raia Mwema na kumwagia saifa nyingi sana Rais Magufuli, amesema anaridhishwa na kasi ya Magufuli na anamuunga mkono.

Mahojiano ni marefu ila nimejitahidi kuleta ufupi, kwa mahojiano yote fuata link hapo chini kwenye Source.

------------------

RAIA MWEMA: Ndiyo kusema umeamua kuachana na siasa na kujikita kwenye mambo hayo ya kitaaluma?

Dr. SLAA: Suala la kuacha au kubaki kwenye siasa nadhani ni tafsiri tu. Nilisema sitakuwa kwenye party politics (siasa za vyama), lakini nitakuwa mwanasiasa kwa kuzungumzia masuala yenye maslahi kwa taifa langu. Hakuna wa kunifunga mdomo kwenye hili.

Katika wakati huu, malengo yetu makubwa ni kujenga uchumi imara na mifumo sahihi ya utawala katika kipindi hiki na kukosoa pale panapohitaji marekebisho.

RAIA MWEMA: Katika siku za mwanzo za urais wa Rais John Magufuli kulikuwa na madai kutoka kwa vyama vya upinzani kwamba “ameiba sera zao”. Una mtazamo gani kuhusu dhana hii ya ‘kuiba sera’?

Dr. SLAA: Serikali iliyoko madarakani ina haki daima kuyachukua mawazo yoyote bora kutoka popote na kwa yeyote yanayozalishwa na wadau mbalimbali kwa manufaa ya umma (ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa) na kuyatekeleza bila hata kuhitaji ridhaa ya aliyeyazalisha.

Serikali makini zinazokuwa sikivu na kutekeleza mawazo hayo mazuri, huviweka vyama vya upinzani kuwa daima wasindikizaji kwa kutekeleza kila wazo jipya wanalotoa.

Wakati wa uchaguzi wanaweza kujikuta wamefilisika kama hawatakuwa na ubunifu mkubwa na kuwa kiwanda cha kuzalisha mawazo mapya kila wakati.
Hii ni changamoto kubwa kwa vyama vinavyofikiria kuwa wanayo hati miliki ya mawazo yaliyoko kwenye hadhara yaani public domain).

RAIA MWEMA: Rais Magufuli amekuwa madarakani kwa takribani miezi minne sasa. Una maoni gani kuhusu utawala wake kwa muda huo?

Dr SLAA: Kwanza, kwa dhati kabisa, napenda kumpa pongezi Rais Magufuli kwa kutembea kwenye ilani aliyoihubiri na ahadi zake binafsi alizozitoa wakati wa kampeni za kutafuta urais.

Wakati naeleza msimamo wangu kuhusu nani anafaa kupigiwa kura sikuficha msimamo wangu.

Nilieleza kuwa kwa mtazamo wangu naona JPM (Magufuli) anaonyesha dhamira ya kweli ya kupiga vita ufisadi. Nadhani Taifa linashuhudia jitihada kubwa katika utekelezaji wa ahadi hiyo.

Tatizo mmoja kubwa, ambalo Watanzania tumelipigia kelele kwa zaidi ya miaka 20 ni tatizo la ufisadi. Tumeeleza mara kadhaa kuwa nchi yetu ni tajiri lakini wananchi wake wengi ni masikini wa kutupwa. Si kwa sababu nchi haina rasilimali bali utajiri wa taifa unaishia mikononi mwa kundi la watu wachache.

Tangu Serikali Kuu hadi Halmashauri zetu na hata Serikali za Mitaa na Vijiji; watu wachache wanajinufaisha wakati umati mkubwa unakondeana mahali pengine hata mlo wa siku ni wa shida.

Japo siko Tanzania na napata taarifa nyingi kutoka huko kupitia magazeti, mitandao ya kijamii na marafiki wanaonijulisha mambo mbalimbali yanayoendelea, naamini taifa zima, isipokuwa kundi la watu wachache ambao ama ni wanufaika wa ufisadi na wizi wa mali ya umma au wananufaika kisiasa na ajenda hizo ambazo zina mvuto kwa wananchi –japo wao waliisha kuikimbia ajenda ya ufisadi tangu walipowakaribisha mafisadi miongoni mwao. Wote ni mashahidi wa hatua kubwa zinazochukuliwa katika vita dhidi ya ufisadi.

Ili funufaike na rasilimali za Taifa kuna hatua kadhaa muhimu kama vile kufunga mianya yote ya ufisadi na wizi wa mali ya umma. Hili limefanyika bandari, TRA, Idara mbalimbali na taasisi za serikali. Hii kazi imefanyika kwa kiasi kikubwa, japo mianya bado inajitokeza hapa na pale.

Bunge nalo halijasalimika. Wengine tulikwisha kumtaka CAG afanye ukaguzi maalum wa Bunge letu ambalo kama ilivyoonekana katika Bunge la 10, lilikuwa pipa la kupitisha mali za umma kwa matumizi mabovu ya chombo chenyewe kilichopaswa kuisimamia serikali.

Wabunge, hasa wa upinzani, wamekuwa wakipiga kelele, lakini inapofikia mabilioni ya pesa waliyayotumia wenyewe kwa matumizi ya " hovyo" ikiwemo dalili za ufisadi wa wazi utadhani wanakuwa wamepigwa sindano ya ganzi. Wote kimya na au kupitisha hoja inayowahusu kwa sauti kubwa ya ndiyoooo. Hii ni hatari sana.

Ni marais wachache sana duniani wenye ujasiri wa kuwagusa wabunge, tena kama taasisi. JPM ameonyesha ujasiri wa ajabu hivyo anahitaji kupigiwa makofi ya kumtia moyo huyu shujaa asiyejali hata maslahi yake. Binafsi, nimemvulia kofia Rais wangu !

Najua watu watasema maneno mengi. Namshauri Rais azidi kumtumaini Mungu wake na dhamira yake imuongoze. Mahitaji ya kuondoa umaskini wa Watanzania yamuongoze na mapenzi ya Mungu kwa taifa letu yawe ndiyo dira yake.

Hakuna Taifa Mungu ameliumba liwe maskini, mwandishi mmoja mashuhuri aliwahi kusema; “Viongozi wenu wa Afrika ndiyo wamewafanya maskini na si mapenzi ya Mungu”. Wizi na ufisadi uliokuwepo ulikuwa wa kimfumo, hivyo hauwezi kuisha bila kugusa mizizi yake.

Kupiga vita dhidi ya ufisadi na wizi wa mali ya umma vinahitaji mshikamano, dhamira ya kweli, hatua za makusudi na za dhati. Ni vita vya taifa zima kwani tuwe chama tawala, tuwe upinzani tunachopigania ni maslahi ya taifa.

Kama tuna nia ya kweli na hilo ndilo lengo kuu basi tutatofautiana katika njia za kufikia hilo lengo kuu lakini vita ni vyetu wote. Na wala hakuna uadui kati ya chama na chama au mtu na mtu. Tutasimamia misingi yaani principles.

Hatua ya pili ni kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika kwa kuwasimamisha kupisha uchunguzi. Wanaoonekana na dalili za kuhusika kufikishwa kwenye vyombo vinavyohusika vya kiutawala na vya kisheria. Hali hiyo imefanyika na inaendelea kufanyika nchi nzima.

Kwa wote tuliokuwa tumevalia njuga vita dhidi ya ufisadi hii ni hatua ya kupongezwa na kuungwa mkono kwa nguvu zote. Hata maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa hayaingiliwi, yameguswa.

Haiangaliwi sura ya mtu mapambano yanaongozwa na maslahi mapana ya taifa, kama yalivyoidhinishwa na wananchi kwa njia ya kura zao wakati wa uchaguzi.

Hapa ndipo penye kelele nyingi na wengine tulizitegemea kwani ukiisha kuingilia chakula cha watu ujue kuwa wanufaikaji wote, mmoja kwa mmoja au wale wanaonufaika kwa njia yao ( indirect beneficiaries) au hata " fuata bendera" wanaoburuzwa kwa ushabiki tu.

Hata hivyo, kamanda anayejua ahadi yake kwa wananchi, wajibu wake kwa Mungu wake, kwa taifa lake na dhamira yake hatatishwa na kelele hizo. Kikubwa ni kwa mheshimiwa Rais na watendaji wake asiwe na dhamira ya wazi ya kumnyanyasa mtu bila sababu.

Hatua hiyo ni dhahiri pia itakumbwa na majungu mengi, umbeya, kusingiziana na kuchafuana. Ni kweli katika hatua hiyo wako wachache watakaokumbwa na mtego wa panya ambapo huingia wahusika na wasiohusika.

Lakini huwezi kuacha kuchukua hatua kwa ajili hiyo. Wahenga husema, 'Uamuzi lazima uchukuliwe, tena kwa wakati unaofaa hata kama baadaye utaonekana ni mbaya, utarekebishwa! Hii ndiyo hali tuliyonayo. Mfumo ulikuwa umeoza, ni lazima maamuzi magumu yafanyike, na wakati wa maamuzi magumu siyo wa kubembelezana.

Hatua kubwa ya tatu ni kurekebisha watendaji wakuu wa zile taasisi za ufuatiliaji na za kichunguzi kama PCCB ( Takukuru). Mara ngapi tulipiga kelele kuwa TAKUKURU yenyewe inahitaji kuundiwa TAKUKURU ya kuichunguza?

Hali hiyo ilikuwepo tangu ngazi ya taifa hadi ngazi ya Halmashauri za Miji, Manispaa na Wilaya. Ilihitaji ushujaa mkubwa kuigusa TAKUKURU ili Raisi asiwe pia mpelelezi wa mashauri ya rushwa na wizi wa mali ya umma.

Japo kwa kiwango kikubwa Polisi, Usalama wa Taifa, Idara ya DPP na Mahakama hawajuguswa sana ni imani yangu kuwa punde kutakuwa na "shake-up" (safisha-safisha) kubwa pia ili mifumo ianze kufanya kazi.

Kuna baadhi ya watu walianza kupiga kelele tangu siku ya kwanza baada ya JPM kuanza kuchukua hatua. Ni kweli katika uwanja wa mpira wako ambao kazi ya ni kushangilia sana, wako ambao wanaweza kumpiga jirani teke kwa kuwa mchezaji alikuwa karibu na goli na badala ya kufunga akapaisha mpira juu !

Ebu huyo mtaalamu wa kupiga kelele na kuwasema wenzake apewe mpira na aachiwe goli bila hata kipa tuone kama ataweza kufunga bao.

Namuomba Magufuli asikatishwe tamaa na hao wanaoponda kila analofanya. Tunawajua kwa vile wao –katika wakati muhimu sana waliwakumbatia mafisadi.

Leo wana lipi la kumuambia shujaa wa Watanzania? Mimi namuambia Magufuli kaza moyo au kaza buti wasemavyo vijana.

Ni imani yangu kuwa muda mrefu hautapita kabla nafasi zilizo wazi katika ngazi zote zipate watendaji waadilifu na waliochujwa vizuri kufanya kazi za umma.

Mfumo haujengwi hewani, bali kwa kutumia watu waadilifu, wanaoaminika na wanaowajibika. Kwa kuwa uadilifu, uaminifu na uwajibikaji ni tunu adimu sana iliyoachwa kutekekezwa kwa muda mrefu, unatakiwa uangalifu mkubwa sana katika kuwapata vinara wa kujenga mifumo mbalimbali itakayorudisha taifa letu kwenye reli.

Kwenye miezi yake minne ya kwanza, Rais ameingilia tatizo kubwa linalofanana na kansa katika taifa letu. Tatizo la dawa za kulevya. Mwenye macho au masikio haambiwi tazama au sikiliza.

Kwa muda mfupi, Serikali ya Awamu ya Tano imeingia mpaka kwenye kiini cha tatizo hilo. Magazeti na mitandao ya kijamii ni mashahidi wa idadi kubwa ya watu waliokamatwa katika siku hizi chache.

Na haya yamefanyika kimyakimya. Hakuna kelele. Hivi ndivyo namna ya kupambana na mtandao huu wenye fedha nyingi, silaha na ' network' pana.

Dr SLAA: Kama ningelikuwa mimi Rais wa Tanzania ningelifanya nini tofauti?
Watanzania wengi wanajua vision na mtazamo wangu tangu mwaka 2010 na hata kwenye ziara zangu mikoani na vijijini kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.

Nimezunguka nchi nzima mijini na vijijini. Watanzania wanajua nilisimamia nini na bado nasimamia nini. Kwa Kuwa Rais wangu anayatekeleza na mengine ambayo hata mimi sijayasema, wajibu wangu sasa ni kumpa nafasi ya kutekeleza hiyo vision yake kwa manufaa ya Watanzania.

Source: Raia Mwema - Dk. Slaa: Kama wewe si fisadi, unamchukia Magufuli kwa lipi?
 
Ukitaka kujua wabunge wa upinzani waroho wa pesa

OMBA
1.Ruzuku za vyama ziondolewe
2.Posho za vikao vya bunge ziondolewe kwani wanalipwa mishahara.

Dr.Slaa anawajua vizuri
 
Dr Slaa ambaye yuko nchini Canada Masomoni akisomea Psychology amefanya mahojiano na Gazeti la Raia Mwema na kumwagia saifa nyingi sana Rais Magufuli, amesema anaridhishwa na kasi ya Magufuli na anamuunga mkono.

Mahojiano ni marefu ila nimejitahidi kuleta ufupi, kwa mahojiano yote fuata link hapo chini kwenye Source.

RAIA MWEMA: Ndiyo kusema umeamua kuachana na siasa na kujikita kwenye mambo hayo ya kitaaluma?
Dr SLAA: Suala la kuacha au kubaki kwenye siasa nadhani ni tafsiri tu. Nilisema sitakuwa kwenye party politics (siasa za vyama), lakini nitakuwa mwanasiasa kwa kuzungumzia masuala yenye maslahi kwa taifa langu. Hakuna wa kunifunga mdomo kwenye hili.
Katika wakati huu, malengo yetu makubwa ni kujenga uchumi imara na mifumo sahihi ya utawala katika kipindi hiki na kukosoa pale panapohitaji marekebisho.

RAIA MWEMA: Katika siku za mwanzo za urais wa Rais John Magufuli kulikuwa na madai kutoka kwa vyama vya upinzani kwamba “ameiba sera zao”. Una mtazamo gani kuhusu dhana hii ya ‘kuiba sera’?

Dr SLAA: Serikali iliyoko madarakani ina haki daima kuyachukua mawazo yoyote bora kutoka popote na kwa yeyote yanayozalishwa na wadau mbalimbali kwa manufaa ya umma (ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa) na kuyatekeleza bila hata kuhitaji ridhaa ya aliyeyazalisha.
Serikali makini zinazokuwa sikivu na kutekeleza mawazo hayo mazuri, huviweka vyama vya upinzani kuwa daima wasindikizaji kwa kutekeleza kila wazo jipya wanalotoa.
Wakati wa uchaguzi wanaweza kujikuta wamefilisika kama hawatakuwa na ubunifu mkubwa na kuwa kiwanda cha kuzalisha mawazo mapya kila wakati.
Hii ni changamoto kubwa kwa vyama vinavyofikiria kuwa wanayo hati miliki ya mawazo yaliyoko kwenye hadhara yaani public domain).

RAIA MWEMA: Rais Magufuli amekuwa madarakani kwa takribani miezi minne sasa. Una maoni gani kuhusu utawala wake kwa muda huo?

Dr SLAA: Kwanza, kwa dhati kabisa, napenda kumpa pongezi Rais Magufuli kwa kutembea kwenye ilani aliyoihubiri na ahadi zake binafsi alizozitoa wakati wa kampeni za kutafuta urais.
Wakati naeleza msimamo wangu kuhusu nani anafaa kupigiwa kura sikuficha msimamo wangu.
Nilieleza kuwa kwa mtazamo wangu naona JPM (Magufuli) anaonyesha dhamira ya kweli ya kupiga vita ufisadi. Nadhani Taifa linashuhudia jitihada kubwa katika utekelezaji wa ahadi hiyo.
Tatizo mmoja kubwa, ambalo Watanzania tumelipigia kelele kwa zaidi ya miaka 20 ni tatizo la ufisadi. Tumeeleza mara kadhaa kuwa nchi yetu ni tajiri lakini wananchi wake wengi ni masikini wa kutupwa. Si kwa sababu nchi haina rasilimali bali utajiri wa taifa unaishia mikononi mwa kundi la watu wachache.

Tangu Serikali Kuu hadi Halmashauri zetu na hata Serikali za Mitaa na Vijiji; watu wachache wanajinufaisha wakati umati mkubwa unakondeana mahali pengine hata mlo wa siku ni wa shida.
Japo siko Tanzania na napata taarifa nyingi kutoka huko kupitia magazeti, mitandao ya kijamii na marafiki wanaonijulisha mambo mbalimbali yanayoendelea, naamini taifa zima, isipokuwa kundi la watu wachache ambao ama ni wanufaika wa ufisadi na wizi wa mali ya umma au wananufaika kisiasa na ajenda hizo ambazo zina mvuto kwa wananchi –japo wao waliisha kuikimbia ajenda ya ufisadi tangu walipowakaribisha mafisadi miongoni mwao. Wote ni mashahidi wa hatua kubwa zinazochukuliwa katika vita dhidi ya ufisadi.

Ili funufaike na rasilimali za Taifa kuna hatua kadhaa muhimu kama vile kufunga mianya yote ya ufisadi na wizi wa mali ya umma. Hili limefanyika bandari, TRA, Idara mbalimbali na taasisi za serikali. Hii kazi imefanyika kwa kiasi kikubwa, japo mianya bado inajitokeza hapa na pale.
Bunge nalo halijasalimika. Wengine tulikwisha kumtaka CAG afanye ukaguzi maalum wa Bunge letu ambalo kama ilivyoonekana katika Bunge la 10, lilikuwa pipa la kupitisha mali za umma kwa matumizi mabovu ya chombo chenyewe kilichopaswa kuisimamia serikali.

Wabunge, hasa wa upinzani, wamekuwa wakipiga kelele, lakini inapofikia mabilioni ya pesa waliyayotumia wenyewe kwa matumizi ya " hovyo" ikiwemo dalili za ufisadi wa wazi utadhani wanakuwa wamepigwa sindano ya ganzi. Wote kimya na au kupitisha hoja inayowahusu kwa sauti kubwa ya ndiyoooo. Hii ni hatari sana.
Ni marais wachache sana duniani wenye ujasiri wa kuwagusa wabunge, tena kama taasisi. JPM ameonyesha ujasiri wa ajabu hivyo anahitaji kupigiwa makofi ya kumtia moyo huyu shujaa asiyejali hata maslahi yake. Binafsi, nimemvulia kofia Rais wangu !
Najua watu watasema maneno mengi. Namshauri Rais azidi kumtumaini Mungu wake na dhamira yake imuongoze. Mahitaji ya kuondoa umaskini wa Watanzania yamuongoze na mapenzi ya Mungu kwa taifa letu yawe ndiyo dira yake.

Hakuna Taifa Mungu ameliumba liwe maskini, mwandishi mmoja mashuhuri aliwahi kusema; “Viongozi wenu wa Afrika ndiyo wamewafanya maskini na si mapenzi ya Mungu”. Wizi na ufisadi uliokuwepo ulikuwa wa kimfumo, hivyo hauwezi kuisha bila kugusa mizizi yake.
Kupiga vita dhidi ya ufisadi na wizi wa mali ya umma vinahitaji mshikamano, dhamira ya kweli, hatua za makusudi na za dhati. Ni vita vya taifa zima kwani tuwe chama tawala, tuwe upinzani tunachopigania ni maslahi ya taifa.
Kama tuna nia ya kweli na hilo ndilo lengo kuu basi tutatofautiana katika njia za kufikia hilo lengo kuu lakini vita ni vyetu wote. Na wala hakuna uadui kati ya chama na chama au mtu na mtu. Tutasimamia misingi yaani principles.

Hatua ya pili ni kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika kwa kuwasimamisha kupisha uchunguzi. Wanaoonekana na dalili za kuhusika kufikishwa kwenye vyombo vinavyohusika vya kiutawala na vya kisheria. Hali hiyo imefanyika na inaendelea kufanyika nchi nzima.
Kwa wote tuliokuwa tumevalia njuga vita dhidi ya ufisadi hii ni hatua ya kupongezwa na kuungwa mkono kwa nguvu zote. Hata maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa hayaingiliwi, yameguswa.
Haiangaliwi sura ya mtu mapambano yanaongozwa na maslahi mapana ya taifa, kama yalivyoidhinishwa na wananchi kwa njia ya kura zao wakati wa uchaguzi.

Hapa ndipo penye kelele nyingi na wengine tulizitegemea kwani ukiisha kuingilia chakula cha watu ujue kuwa wanufaikaji wote, mmoja kwa mmoja au wale wanaonufaika kwa njia yao ( indirect beneficiaries) au hata " fuata bendera" wanaoburuzwa kwa ushabiki tu.
Hata hivyo, kamanda anayejua ahadi yake kwa wananchi, wajibu wake kwa Mungu wake, kwa taifa lake na dhamira yake hatatishwa na kelele hizo. Kikubwa ni kwa mheshimiwa Rais na watendaji wake asiwe na dhamira ya wazi ya kumnyanyasa mtu bila sababu.
Hatua hiyo ni dhahiri pia itakumbwa na majungu mengi, umbeya, kusingiziana na kuchafuana. Ni kweli katika hatua hiyo wako wachache watakaokumbwa na mtego wa panya ambapo huingia wahusika na wasiohusika.

Lakini huwezi kuacha kuchukua hatua kwa ajili hiyo. Wahenga husema, 'Uamuzi lazima uchukuliwe, tena kwa wakati unaofaa hata kama baadaye utaonekana ni mbaya, utarekebishwa! Hii ndiyo hali tuliyonayo. Mfumo ulikuwa umeoza, ni lazima maamuzi magumu yafanyike, na wakati wa maamuzi magumu siyo wa kubembelezana.
Hatua kubwa ya tatu ni kurekebisha watendaji wakuu wa zile taasisi za ufuatiliaji na za kichunguzi kama PCCB ( Takukuru). Mara ngapi tulipiga kelele kuwa TAKUKURU yenyewe inahitaji kuundiwa TAKUKURU ya kuichunguza?
Hali hiyo ilikuwepo tangu ngazi ya taifa hadi ngazi ya Halmashauri za Miji, Manispaa na Wilaya. Ilihitaji ushujaa mkubwa kuigusa TAKUKURU ili Raisi asiwe pia mpelelezi wa mashauri ya rushwa na wizi wa mali ya umma.

Japo kwa kiwango kikubwa Polisi, Usalama wa Taifa, Idara ya DPP na Mahakama hawajuguswa sana ni imani yangu kuwa punde kutakuwa na "shake-up" (safisha-safisha) kubwa pia ili mifumo ianze kufanya kazi.
Kuna baadhi ya watu walianza kupiga kelele tangu siku ya kwanza baada ya JPM kuanza kuchukua hatua. Ni kweli katika uwanja wa mpira wako ambao kazi ya ni kushangilia sana, wako ambao wanaweza kumpiga jirani teke kwa kuwa mchezaji alikuwa karibu na goli na badala ya kufunga akapaisha mpira juu !

Ebu huyo mtaalamu wa kupiga kelele na kuwasema wenzake apewe mpira na aachiwe goli bila hata kipa tuone kama ataweza kufunga bao.
Namuomba Magufuli asikatishwe tamaa na hao wanaoponda kila analofanya. Tunawajua kwa vile wao –katika wakati muhimu sana waliwakumbatia mafisadi.
Leo wana lipi la kumuambia shujaa wa Watanzania? Mimi namuambia Magufuli kaza moyo au kaza buti wasemavyo vijana.
Ni imani yangu kuwa muda mrefu hautapita kabla nafasi zilizo wazi katika ngazi zote zipate watendaji waadilifu na waliochujwa vizuri kufanya kazi za umma.

Mfumo haujengwi hewani, bali kwa kutumia watu waadilifu, wanaoaminika na wanaowajibika. Kwa kuwa uadilifu, uaminifu na uwajibikaji ni tunu adimu sana iliyoachwa kutekekezwa kwa muda mrefu, unatakiwa uangalifu mkubwa sana katika kuwapata vinara wa kujenga mifumo mbalimbali itakayorudisha taifa letu kwenye reli.
Kwenye miezi yake minne ya kwanza, Rais ameingilia tatizo kubwa linalofanana na kansa katika taifa letu. Tatizo la dawa za kulevya. Mwenye macho au masikio haambiwi tazama au sikiliza.
Kwa muda mfupi, Serikali ya Awamu ya Tano imeingia mpaka kwenye kiini cha tatizo hilo. Magazeti na mitandao ya kijamii ni mashahidi wa idadi kubwa ya watu waliokamatwa katika siku hizi chache.
Na haya yamefanyika kimyakimya. Hakuna kelele. Hivi ndivyo namna ya kupambana na mtandao huu wenye fedha nyingi, silaha na ' network' pana.

Dr SLAA: Kama ningelikuwa mimi Rais wa Tanzania ningelifanya nini tofauti?
Watanzania wengi wanajua vision na mtazamo wangu tangu mwaka 2010 na hata kwenye ziara zangu mikoani na vijijini kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.
Nimezunguka nchi nzima mijini na vijijini. Watanzania wanajua nilisimamia nini na bado nasimamia nini. Kwa Kuwa Rais wangu anayatekeleza na mengine ambayo hata mimi sijayasema, wajibu wangu sasa ni kumpa nafasi ya kutekeleza hiyo vision yake kwa manufaa ya Watanzania.

Source: Raia Mwema - Dk. Slaa: Kama wewe si fisadi, unamchukia Magufuli kwa lipi?
Kias kikubwa nayakubali
 
hahahahahhaha...slaa wa raia Tanzania

Irrelevant

Soldiers do not run from the war field...Its only cowards wanaweza fanya ivo
 
Back
Top Bottom