comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar Mh Dr Mohammed Ali Shein amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya nchi, kujenga maelewano na mahusiano mazuri katika jamii.
Vyombo vya habari hivyo ni maonganisho sahihi katika jamii hususani katika masuala ya kupata na kutoa habari kwa jamii na Serikali wala sio maadui, hivyo wananchi na serikali iwaone sio maadui bali ni wadau wazuri wa maendeleo katika mustakabali wa nchi na ustawi wa jamii, Rais Shein ameyasema hayo Zanzibar leo wakati akiongea na vyombo vya habari katika mchango wao dhidi ya maendeleo ya nchi.
Chanzo: ITV