DR Shein na Baraza la mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DR Shein na Baraza la mawaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Oct 24, 2011.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Leo Rais JK amemwapisha Dr Shein kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri na kisha amehudhuria kikao chake cha kwanza cha baraza hilo tangu achaguliwe kuwa rais wa zanzibar mwaka jana. Hii ni kwa mujibu wa katiba kwani rais wa zenj anatakiwa kikatiba kuwa mjumbe wa barza la mawaziri. Najiuliza hivi kama matokeo ya uchaguzi zanzibar yangetangazwa yale ya ukweli kuwa Maalim seif kashinda, ina maana leo tungekuwa na serikali ya muungano ya Mseto???
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Yaani inachukuwa zaidi ya mwaka kuingia kwenye baraza la mawazir!!! Sasa kama kuna maamuzi yamepitishwa na hayana maslahi kwa ZNZ hivi atawambia nini wananchi wake. Au kwa nini baada ya mwaka mzima bila kuhudhuria vikao leo ndiyo ameona umuhimu wa kufanya hivyo??
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  naamini ni sehemu ya udhaifu mkubwa tulionao katika katiba yetu. ni kweli mwaka umepita yeye kama mjumbe halali wa baraza la mawaziri alikuwa hahudhurii vikao vya cabinet kwa sababu alikuwa hajaapishwa na JK, hakuna sababu za msingi ni kwanini alikuwa hajaapishwa muda wote huo
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa ccm haiwezekani. kama mshindi wa kweli maalim seif angetangazwa basi angekaa miaka 5 bila kuapishwa. huoni tu huyu wa ccm yao pamoja na kuwa ni wao lakini kisa tu kuna upinzani imechukua mwaka? walikuwa wakipima upepo kuona kama serikali ya mseto itawaathiri. wewe unacheza na ccm nini? hii mijamaa ni mimafya kwelikweli.
   
Loading...