figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema yeye hatishiki na maneno yanayosemwa dhidi yake na kusisitiza kuwa atabaki kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuwa hakujiweka mwenyewe bali ni kwa mujibu wa Katiba na Sheria.“Nimeyasikia maneno yanayosemwa lakini hayanitishi nami nitaendelea kubaki kuwa Rais wa Zanzibar.Umri huu sitishiki tena na kama wao wana ubavu wa kikatiba wajaribu kuniondoa” Dk. Shein alisema wakati akizungumza na vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa Maisara mjini Unguja jana.
Alibainisha kuwa Zanzibar inaongozwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria wala si utashi wa mtummoja anayetaka kuongoza nchi na kwamba hakuna njia ya mkato katika hilo.Katika mnasaba huo alieleza kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ndio yeye mamlaka ya kisheria katika suala la uchaguzi hivyo vyama vyote havina budi kutii maamuzi yake likiwemo la kufuta uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015.
“Tangazo la Tume la kufuta uchaguzi ni halali na limekuwa la kisheria baada ya kutangazwa katika gazeti rasmi la serikali hivyo sisi CCM tunasubiri Tume itangaze tarehe nyingine ya uchaguzi ili tushiriki” Dk. Shein alieleza.Alibanisha kuwa kukubali au kukataa kushiriki katika uchaguzi wa marudio ni uamuzi wa kila chama hivyo kama wengine wataamua kutoshiriki huo utakuwa uamuzi wao binafsi wala CCM haiwezi kuwaingilia.
“ZEC ndio yenye mamlaka yote sisi tutaridhia na wasipotaka hiyo ni hiari yao katika chama chao” Dk. Shein alisema huku akishangiliwa na vijana na wananchi waliohudhuria hafla hiyo.Aliongeza kuwa yamesemwa mengi kuhusu yeye na uchagazi na kwamba yeye naye anayo mengi ya kusema lakini atafanya hivyo wakati ukifika.
“yako mengi yamesemwa na yanaendelea kusemwa nami ninayo mengi lakini nitasema siku ikifika na nitasema kweli siku hiyo ikifika” Dk. Shein alisisizitiza na kuonesha anayo mengi moyoni yanayomkereketa.Kabla ya kuzungumza na vijana Dk. Shein ambaye aliambatana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokea maandamano ya vijana hao kutoka mikoa ya Zanzibar na Tanzania bara.