Dkt. Rioba wa TBC ataka kupigana na Gerald Hando wa E-FM kwa kuambiwa TBC imemshinda

ukweli unauma jaman.
ila inaweza kuwa Ryoba anakabiliwa na Umagulification kiasi anashindwa timiza wajibu na ndoto zake
 
kwa nini mlitafisiri kitendo cha lyoba kwamba anakwenda kuchukua bastola?....kwani anaendaga nayo baa
 
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Habari Tanzania TBC, Dkt. AYOUB RYOBA kama siyo watu kumshika na kuwaamua, nusura apigane na Mtangazaji wa kituo cha Redio cha EFM Gerald Hando.

Tukio hilo lilitokea katika Bar ya LILLY'S iliyoko Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya Gerad Hando kumwambia RYOBA kuwa ameshindwa kabisa kulifanya Shirika la TBC lionekane linaongozwa na Mkurugenzi mwenye elimu ya kutosha Kabisa ya kiwango cha Phd na aliyefundisha wana taaluma mbalimbali wa habari.

Baada ya ugomvi huo kuzuiwa na watu waliokuwepo karibu, DR.Ryoba aliondoka kuelekea kwenye gari lake ambapo ilitafsiriwa kuwa alikuwa anakwenda kuchukua Bastola.

Aidha Bosi huyo wa TBC alisikika akisema kuwa atamshughulikia Gerald Hando na hakuna wa kumfanya lolote.

Kwa mtu mwenye kiwango cha elimu ya PhD angeomba ushahidi wa kitaalamu kuthibitisha kauli ya Hando badala ya kusema atamshughulikia kwa njia ambazo hajazisema kitu ambacho ni hatari sana kwake kwani watu wengine waweza kumdhuru Hando na yeye kuwa a chief suspect.
 
Tatizo la TBC ni fungu hata aende nani pale lazima wapewe pesa.Huyo Hando hana adabu tu,na watu wa kwenye tasnia moja lazima muheshimiane kwenye public huwezi jua kesho mwenzako anaweza kuwa kwenye sehemu ya kukufinyanga ukajikuta unahamia burundi
 
Sasa ukiambiwa ukweli si ndii motivation ya kujipanga.. Mm nafurahi sana mtu anaponambia ukweli ambao naona yupo sahihi, najipanga kufanya bora aje anisifie.
Wengine wakiambiwa ikweli anajiona kadhalilishwa wakati sio sahihi. Kama huyo anaringia vyeti lakini utendaji ziro laiti angemsikiliza apate ushauri kwa asiye na phd pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtu mwenye kiwango cha elimu ya PhD angeomba ushahidi wa kitaalamu kuthibitisha kauli ya Hando badala ya kusema atamshughulikia kwa njia ambazo hajazisema kitu ambacho ni hatari sana kwake kwani watu wengine waweza kumdhuru Hando na yeye kuwa a chief suspect.
kwani pombe huwa inamtambua mtu mwenye PhD ili imheshimu.Pombe ni kama kifo huwa haibagui hata Magu akitandika anajisahau kama ni mkuu wa nchi. Ngoja nikatoe loki kwanza
 
Back
Top Bottom