Lakini ni Daktari (PhD Holder) na kama sikosei nilimsikia redioni akieleza jinsi alivyosoma. Au naye ni 'Dr' kama Maji Marefu na bosi wake, au ndio elimu ya Kitanzania!?Uwezo wa huyu bwana kisheria ni mdogo sana, hajui ana makosa ya kinidhamu na makosa ya kimaadili, ya kinidhamu ndiyo miaka saba, sasa bado ya kimaadili yanamngojea, pia haelewi maana ya Judicial Organs, hizi ni kamati huru hakuna wa kuziingilia, zinajitegemea hivyo alumbane na kamati siyo Rais wa TFF, pia ni dharau kwa wakili senior kwake kama Jerome Msemwa, anatafuta umaarufu.