Ngalikivembu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,959
- 874
Mara baada ya kuapishwa rasmi kuchukua majukumu yao,Waziri wa Ujenzi na Naibu wake (Dr Magufuli na Dr Mwakyembe) walifanya mkutano na watendaji wote wa Tanroads pale ukumbi wa Karimjee jijin Dar.Japo ilikuwa siku ya mapumziko Jumapili lakini mawaziri hao waliamua kukutana nao ili kuwapa "msimamo'' wao.Nilichokiona mimi na kustaajabia ilikuwa ni kuona mawaziri hao wakigawa ilani ya CCM.Hili nilishindwa kulielewa kidogo.Hawajui kuwa pale si wote ni wanachama wa CCM?Au ndio kusema kila mfanyakazi tayari anakuwa mwanachama indirect?Katika hili nadhani hawakuwa sahihi japo nia ni nzuri.Hivi atakapo kuja kubaini kuwa wengine waliamua kuzitupa jalalani watawafukuza kazi?
Naomba kusaidiwa katika hili.
Naomba kusaidiwa katika hili.