Ningelikuwa ni Zitto, Kitila au Mwigamba muda kama huu ningelikaa kimya tu.
Unamtuhumu kuwa Slaa ni muongo wakati maamuzi yalifanywa na jopo la watu kadhaa na kusomwa na Slaa.
Ina maama maamuzi yale yangelisomwa na Mbowe kama utaratibu unavyohitaji, si ajabu leo hii Kitila angesema Mbowe ni muongo.
Hili jambo linanikera hata mimi. Sijawahi kuwa mwanachama wa ccm wala CDM, bali napenda sana mabadiliko. Simjui Zitto, wala Mbowe wala yoyote. Na isitoshe siishi Tanzania na sitegemei ccm ili kuishi,nashangazwa sana na ukionyesha mtizamo tofauti unapewa chama hapohapo kuwa CCM, khaaa! Binafsi naichukia sana ccm na nikipewa uanachama hata wa jukwaani huwa inanikera. Wana CDM heshimuni mawazo ya wengine si kweli kwamba sote ni ccm. Nalisema hili kwa dhati kabisa ya moyo wangu. Hao ccm wanaomsapoti zitto bila shaka wana ajenda yao. Ila binafsi sina agenda yyte ila napenda kuona demokrasia ya kweli CDM isiwe copy & paste ya CCM
Hujui hata unachokiandika hapa ni nini bias mkubwa wewe!Why CCM unawataja tu walio bora lkn CHADEMA unawataja unao ona wewe sio bora?Why usifananishe na CHADEMA ya Prof Safari;Prof Baregu,John Mnyika na wengineo!Why usiitaje CCM ya akina Lusinde,Prof Kapuya,Madabida,Rage na wengineo wa hovyohovyo??
Nani kaisifia CCM?naichukia sana CCM na bila shaka nilianza kuichukia CCM ata kabla hujajua siasa ni nini LAKINI pamoja na chuki yangu hiyo lakini nautambua ukweli mchungu kuwa hii CCM Mbovu bado ni bora maradufu kuliko Chadema ya Mbowe na Slaa.Na uchaguzi wa kutoka kwenye "kibovu" kwenda kwenye "kibovu zaidi" sio uchaguzi wa mtu mwenye akili timamu.
Chadema ilikuwa na nafasi ya kujijenga kuwa tayari kutawala lakini ndio kwanza ipo busy kujidhatiti kwenye ubovu,tutaisaidiaje sasa?Tanzania itakuwa hovyo zaidi chini ya hii Chadema ya Mbowe/Slaa/Lema/Sugu/Msigwa kuliko ilivyo chini ya CCM ya Kikwete/Sitta/Membe/Mwakyembe/Magufuli.
Nani kaisifia CCM?naichukia sana CCM na bila shaka nilianza kuichukia CCM ata kabla hujajua siasa ni nini LAKINI pamoja na chuki yangu hiyo lakini nautambua ukweli mchungu kuwa hii CCM Mbovu bado ni bora maradufu kuliko Chadema ya Mbowe na Slaa.Na uchaguzi wa kutoka kwenye "kibovu" kwenda kwenye "kibovu zaidi" sio uchaguzi wa mtu mwenye akili timamu.
Chadema ilikuwa na nafasi ya kujijenga kuwa tayari kutawala lakini ndio kwanza ipo busy kujidhatiti kwenye ubovu,tutaisaidiaje sasa?Tanzania itakuwa hovyo zaidi chini ya hii Chadema ya Mbowe/Slaa/Lema/Sugu/Msigwa kuliko ilivyo chini ya CCM ya Kikwete/Sitta/Membe/Mwakyembe/Magufuli.
Duh...kumbe na wewe unajua Mbowe/Slaa/Lema/Sugu/Msigwa ni viongozi wa hovyohovyo?atleast akili yako imeongea kile ambacho moyo wako unajitahidkutokiona.
Kama Mh Sitta alivyowahi kusema,Chadema ina wigo mwembamba sana wa viongozi,hakuna namna utataja majembe ya Chadema bila kuwataja Mbowe/Slaa/Sugu/Msigwa na Lema,ndiyo viongozi wenyewe hawa...usiwanyanyapae..
..Na bahati mbaya majembe haya ndio yanalingana sifa na hao vidampa wa CCM uliowataja,so unaweza kuona tofauti iliyopo kati ya ubora wa CCM na ule wa Chadema ukizingatia uwezo wa majembe yake.
uzinzi wake umeujuaje?au alishavuruga familia yenu wote,by the way wewe unae waita wenzako nasty names u msafi?
Umeanza kunibandikia maneno yako yawe yangu!CCM ndiyo ina viongozi wa hovyohovyo na sio CHADEMA!!
Dr Slaa HAWEZI kuwa kiongozi wa hovyo kwa mwana siasa yyt active aliyepo CCM leo!Tuanze kutaja hapa sifa za Dr Slaa kulinganisha na kiongozi yyt yule aliyepo CCM!Nasubiri unitajie kiongozi yyt yule mwadilifu ndani ya hii CCM ya JK kumzidi Dr Slaa!
Kinacho onekana ni kutishika na akina Dr Mwakyembe wanapoita media kutuzuga watz kama wanafanya kazi!Kinachokutisha nni Magufuli na kilometer zake za uongo za barabara na mtu asiye na exposure atajua TZ ina barabara nzuri kweli kweli miaka 52 baada ya Uhuru!Hao unao waona wewe masiah ni viongozi hovyo hovyo kabisa na wlaistahili sasa wawe jela Ukonga kwa matumizi mabaya ya pesa zetu!
Nasubiri uchambuzi zaidi na nitashinda kwa hoja na ww utashinda kwa vioja!
Tuanzie hapa,ni nini uadilifu wa Dr Slaa?kumbuka..uadilifu haupimwi kwa maneno.
Dr Slaa anakiwanda cha uongo
Ni aibu kwa mtu aliyewahi kuwa mtumishi wa Mungu kusema uongo kwa taifa zima tena akizungukwa na wapika uongo wenzake
Mnyika anajidhalilisha kukaa na lile genge la wahuni wapika uongo
Mbowe na Dr Slaa mtuachie chama chetu na mumchukue na lema mwende nae
Uongo wa Dr Slaa ndiyo unesababisha UMEME upande kwa 78%?
Tuvulana tujinga tunapiga kimaisha lkn bado tu wapo kuisifia CCM!Matatizo haya tuliyo nayo ya watoto wetu kusomea madarasa ya nyasi hajaletwa na Mungu!
Lkn si wewe ndiye uliwaita viongozi wa CCM ni majembe?Sasa unanigeukia mm tena?
Labda wewe ndiyo uanze mkuu;nn sio uadilifu wa Dr Slaa na ikiwezekana relate ukosefu huo wa uadilifu wa Dr Slaa na matatizo haya makubwa ya uchumi yanatotukabili!
Nasubiri mjadala endelevu
NB:Je unajua kuna watumishi wa UMMA hadi leo hawajalipwa mshahara kwa sababu HAZINA hamna pesa?
Nimesema hivyo baada ya kuona ukidai kuwa Dr Slaa ni muadilifu kuliko yeyote,ndio maana nilipenda nijue hiyo definition yako ya uadilifu..
Hayo ya watumishi wa umma na matatizo ya nchi,kama nilivyosema sikubaliana na nchi inavyokwenda kwa sasa lakini tofauti na wewe ninatambua pia ukweli mchungu kuwa uongozi wa Chadema uliopo sasa,zingatia jinsi wanavyoiendesha Chadema,ni wa hovyo zaidi kuliko uongozi wa serikali iliyopo. So ukiniuliza mimi,nadhani chini ya uongozi huu wa Chadema basi hali ingekuwa hovyo zaidi kuliko ilivyo sasa.