Dr. Kipilimba atakuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa au Usalama wa Magufuli kisiasa?

Status
Not open for further replies.
Feb 26, 2013
30
47
Anaandika Comrade Ben-Rabiu Wa Saanane.

Nilifunzwa kusema ukweli,nikafunzwa kutilia shaka kila kitu.Doubting Everything. Leo Rais Magufuli amemteua Mkurugenzi Mkuu Mpya wa Usalama wa Taifa(TISS) Dr.Modestus Kipilimba. Kabla hajaapishwa baadae leo nafukua Makaburi mawili.

Haya tuanze, Mwaka jana kipindi cha Uchaguzi tulilalamika .Zipo tuhuma zilizopaswa kuwa cleared kwanza maana nafasi hii inahitaji Intergrity.Wengine tulitilia mashaka kustaafu kwa Rashid Othman muda huu hapo majuzi.Nanukuu yale ya Mwaka jana hapa.

"MKAKATI WA KUIBA KURA WANASWA

NEC YAHUSIHSHWA. MSIMAMIZI MKUU NI DR. MODESTUS KIPILIMBA

ALIKUWA MTUMISHI WA BOT, AKADAGANYA KACHUKUA LIKIZO KUMBE KAENDA NEC KWA KAZI MAALUM.


Niliposikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wamekubali matokeo kubandikwa ukutani kwenye vituo husika, niliwaza sana ni jinsi gani CCM inanusurika. Kwa bahati nzuri imegundulikwa kwamba mchezo wote utafanyika kwenye mfumo wa ujumlishaji wa matokeo "Tallying System".

Msimamizi mkuu wa hili zoezi ni Dr. Modestus Kipilimba ambaye katoka BOT (Bank of Tanzania) na kupelekwa ofisi za NEC kwa kile kinachoitwa kazi maalum....

* Dr. Modestus Kipilimba ni nani?..... (Tuanzie hapo)...

Dr. Kipilimba alikuwa mtumishi wa BOT Miaka kadhaa iliyopita. Baada ya BOT kuhusishwa na wizi wa mabilioni ya fedha katika taasisi hiyo taarifa zilitoka kuwa aliachishwa kazi kwa barua namba MFP/BOT/PF/24/03. Baada ya kufukuzwa kazi alikimbilia nje ya nchi (Uingereza) ambapo alienda kusoma zaidi.

Baada ya Prof. Ndulu kuwa gavana wa Bank, Ndugu Kapalimba haijulikani jinsi alivyorudi kazini. Ila ni wazi alipitia mlango wa nyuma, baada ya uongozi wa juu wa banki hiyo kupewa agizo la Dr. Kapalimba kurudishwa kazini. Dr. Kapalimba akaajiriwa tena kwa mara ya pili na kupewa cheo cha "Bank Advisor". Kwa muda mfupi akapandishwa cheo na kuwa mkurugenzi wa idara ya Risk Mgt(Maafa).

Mwezi uliopita Dr. Kapalimba kwa taarifa zilizopo BOT zinaonyesha Kapalimba kachukua likizo. Ila cha kushangaza huyo bwana yupo anafanya kazi NEC na kapewa idara nyeti ndani ya kurugenzi ya IT .Anaongoza kitengo cha TEHAMA Na pia ni yeye aliyepewa jukumu la kupokea na kusambaza makaratasi ya kupigia kura.

Dr. Kapalimba ni mtaalamu wa IT, aliyepeta elimu hiyo nje ya nchi na ni moja wa watu wanaosifika kwa utaalam huo. Idara nyingi za serikali imekuwa ikimtumia kwa operation mbalimbali...

NB:.. Baada ya hili kujulikana sasa tunaomba tume ya uchaguzi ikubali ombi la Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA, John Mnyika. La kutaka mfumo wa kujumuisha idadi za kura ukaguliwe mara moja na vyama vyoto wakiwemo CCM...

Kukagua mfumo husika ndio suluhu kwa sasa. Ila bila NEC kuruhusu hilo, bao la mkono litakuwa hapo...."

Mwisho wa Kunukuu habari hiyo.

Sasa Kabla Mwaka haujaisha Mhusika amepewa Ukurugenzi wa Usalama.Je hii ni Zawadi?

Je,atakua mkurugenzi wa Usalama wa Taifa au Usalama wa Magufuli kisiasa?

Je,Tunaweza kumuamini?

Anayo maadili yasiyotiliwa Shaka?

Oh Kabla sijasahau hivi ile Kampuni ya Infosys iliyomilikiwa na Charles Kitwanga iliyofanya kazi na Lugumi hivi Jina la Modestus Kipilimba si ndio hilihili?

Ni vyema tuhuma hizi na rekodi hii ingesafishwa kabla ya kupewa heshima kubwa kama hii.Tuhuma hizi sikuona kama ziliwahi kujibiwa popote .Ziliwahi kujibiwa?

Aluta Continua,Victory Ascerta....

Ben Saanane
 
Ben Saanane heshima kwako. Nakuomba usiwe msahaulifu na pia usiwe myopic.

Mheshimiwa Pinda aliwahi kusema kuwa hata asulubiwe namna gani hatakubali kujadili mambo fulani, tafakari ni mambo gani hayo?

La pili naamini unajua kwa nini Meremeta na kampuni zingine hazikujadiliwa bungeni.

La tatu sina uhakika sana lakini tulishawahi kujadili humu kuhusu straw companies.

Kuna mambo ambayo kwa nchi hayajadiliki kwa namna yoyote ile! Tukubali hivyo na tuendelee na maisha kama kawaida.

Tumpe ushirikiano boss wetu wa kitengo kinachofanya kazi kubwa bila mbwembwe.
 
Ben Saanane heshima kwako.
Nakuomba usiwe msahaulifu na pia usiwe myopic.
Mheshimiwa Pinda aliwahi kusema kuwa hata asulubiwe namna gani hatakubali kujadili mambo fulani,tafakari ni mambo gani hayo?
La pili naamini unajua kwa nini Meremeta na kampuni zingine hazikujadiliwa bungeni.
La tatu sina uhakika sana lakini tulishawahi kujadili humu kuhusu straw companies.
Kuna mambo ambayo kwa nchi hayajadiliki kwa namna yoyote ile!!!!Tukubali hivyo na tuendelee na maisha kama kawaida.Tumpe ushirikiano boss wetu wa kitengo kinachofanya kazi kubwa bila mbwembwe.
Salute!
.....laiti angepata ufunuo kujua mambo ktk idara za kiusalama yanavyofanyika...
....laiti angepata ufunuo kujua namna siri za mambo nyeti ya usalama wa taifa, zinavyotakiwa kutunzwa (kivitendo na kiutendaji).....
......tuseme tu pia, nchi hii ina hati hati ya kubomolewa na "kina joni kisomo, wajaa tamaa"
 
Salute!
.....laiti angepata ufunuo kujua mambo ktk idara za kiusalama yanavyofanyika...
....laiti angepata ufunuo kujua namna siri za mambo nyeti ya usalama wa taifa, zinavyotakiwa kutunzwa (kivitendo na kiutendaji).....
......tuseme tu pia, nchi hii ina hati hati ya kubomolewa na "kina joni kisomo, wajaa tamaa"
Ni kweli siri za kuiba kura hazijadiliki
 
Kila Nchi ina siri zake.......wala sishangai kwa yetu nayo kuwa na Siri zake........naungana na mchangiaji moja hapo juu anayeshauri tupige kazi maisha yaendelee, haya mengine mazito yatatutoa vibiongo.
 
Atakuwa boss wa TISS ambaye atamtii JPM. Usalama wa taifa mbona wapo kila sehemu Mabere Marando mjumbe wa kamati kuu ya Chadema ni afisa usalama wa taifa na anaifanya kazi yake mpaka sasa kwa unyenyekevu taarifa anapeleka sehemu husika .

Mkuu hilo jibu tosha kabsa wambie hata viongozi wakubwa wa maamzi ndani ya CHADEMA ni TISS na taarfa zao wanatuma kwa wakuu wao kiusahihi bila kujali itakadi zao.
 
Anaandika Comrade Ben-Rabiu Wa Saanane.

Nilifunzwa kusema ukweli,nikafunzwa kutilia shaka kila kitu.Doubting Everything. Leo Rais Magufuli amemteua Mkurugenzi Mkuu Mpya wa Usalama wa Taifa(TISS) Dr.Modestus Kipilimba. Kabla hajaapishwa baadae leo nafukua Makaburi mawili.

Je,Tunaweza kumuamini?

Anayo maadili yasiyotiliwa Shaka?

Oh Kabla sijasahau hivi ile Kampuni ya Infosys iliyomilikiwa na Charles Kitwanga iliyofanya kazi na Lugumi hivi Jina la Modestus Kipilimba si ndio hilihili?

Mkuu, nitakueleza kitu kimoja. Hapa wewe na mimi na wengineo tunatafuta "objectvity" katika mambo ya siasa. Hakuna kitu kama hicho. Siasa siku zote inakuwa na mambo yake mengi tu ya gizani ambayo hata siku kuja hayapaswi kumulikwa tochi. Na kama ukiamua kila kitu cha kisiasa unataka kimulikwe tochi basi unaweza kupata wendawazimu, au kuishia kutaka kuanzisha kikundi cha kwenda msituni.

There is no such thing as sanity in politics, na ili kuelewa mambo ya mengi ya siasa mara nyingine jifanye una akili za mwendawazimu.

Of course haituzuii every now and then kuwasema, just to show that they can fool some people some time, but not all the people all the times. Lakini dont expect the unexpected. Utakonda bure - au utaishia kuwa mwanasiasa, the worst decision mtu anayependa sanity can make.

Mie binafsi sio mwanasiasa kwa sababu I am so sane, to the extent that there is no way I can live or survive in that political world of insanity.
 
UKAWA wamechqnganyikiwa sana. Msiyemtaka kaja. Msubiri kipigo 2020
Kwa hiyo ataendeleza libeneke la 2015 na watu watamwangalia tu huyu anapaswa kwanza kuchezeshwa kwata kuanzia sasa hivi mpakaaajutue aliliyoyafanya mwaka jana kutuwekea dikteta uchwara
 
Hivi huko TISS hakukuwa na watu ambao wangefaa zaidi kupewa hiko cheo kuliko kumtoa mtu kutoka taasisi nyingine?
 
Atakuwa boss wa TISS ambaye atamtii JPM. Usalama wa taifa mbona wapo kila sehemu Mabere Marando mjumbe wa kamati kuu ya Chadema ni afisa usalama wa taifa na anaifanya kazi yake mpaka sasa kwa unyenyekevu taarifa anapeleka sehemu husika .
Tena nasikia watu hao huwa hawastaafu...
 
UKAWA wamechqnganyikiwa sana. Msiyemtaka kaja. Msubiri kipigo 2020
kweli we ni chaumbea ukiambiwa uthibitishe kauli yako utasemaje maana inazua walakini wa 2020 unachochea uvunjifu wa amani kwa majibu yako kijana chunga sana ulimi wako na mahaba niue yako .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom