Dr. Kikwete atembelea SUA; asema heri mtembea bure kuliko mkaa bure

kutembea kwingi nako huwa kelo
Kaa ndani kwako tu bila kutoka uone kama hujauza masofa na vitanda vyako mpaka sahani na vijiko. Wenzenu wanatoka kutafuta pesa, nyie mmejifungia ndani mnaishia kukamua watu visenti vyao mitaani. Kila siku tunataka wawekezaji, sasa hao wawekezaji bila kwenda kuwaonyesha hivyo vya kuwekeza watakujaje?...... Mgaagaaa na upwa hali wali mkavu!
 
JK bana utajikuta umempenda tu hata kama hutaki...leo alitembea Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine(SUA) na kuwaomba menejimenti ya chuo hicho wasisite kumtuma kwingineko duniani kama wana jambo wanahitaji msaada kwani yeye huwa anatembea sana, haha:

"Jamani kama mnalo jambo linawatatiza niambieni tu, mimi natumia ile kanuni ya mbwa ile, naamini heri kutembea bure kuliko kukaa bure...maana ukimwona mbwa anakimbia kimbia tu hivi bure anaweza akaokota FUPA, lakini ukikaa tu nyumbani hupati kitu"....hapo kikafatia kicheko cha kutosha:p (Dr.Kikwete akiwa Chuo Kikuu Sokoine leo tarh 20/11/2017)

Source: ITV Habari
Siku hizi washamba wamepungua, enzi ya kutembea tu ili ukaone mji imepitwa nawakati. Siku hizi tembea kwa malengo upate maisha.
 
Yupo kwa rasi simba?
Hata akae kwa ras Simba miaka 20 hakuna chochote kitakachobadilika. Kuna vichwa vingine vilisha goma we kuanzia s/msingi, O level, A level, Degree, Masters mpaka PhD kichwa kimegoma, nyie mnataka kumbebesha mzigo Ras Simba
 
Back
Top Bottom