Dr. Harison mwakyembe nakuheshimu sana, lakini......!

Dr. Harison mwakyembe nakuheshimu sana, lakini......!

Shagiguku

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
409
Reaction score
138
Mheshimiwa Dr Harison Mwakyembe,

Mimi ni mtanzania wa kawaida tu ninayeishi hapa mwanza, kipato changu ni cha chini sana, kwa kifupi naishi kwa kubangaiza sana kwaajili ya kupata mkate wangu wa kila siku.

Asubuhi ya leo nimeamka kuelekea kibaruani kwangu, mara konda wa dala dala akaanza kuomba pesa yake, nikampatia tsh 500/= naona ananirudishia tsh 100/= namuuliza vipi?? ananijibu kuwa nauli zimepanda. Kabla ya hata dakika moja haijaisha nikakusikia wewe kupitia radio iliyokuwa kwenye dala dala hilo ukisema kuwa, ".....Mimi kama Waziri wa Uchukuzi sina tatizo na ongezeko hili dogo la nauli za daladala.......!!!!""

Ni kweli kabisa kwako weye mheshimiwa mwakyembe ukiwa waziri mwenye dhamana ya usafiri (uchukuzi) huwezi kuwa na tatizo la ongezeko hili "DOGO LA NAULI" kwa kuwa tayari hutumii fedha yako ya mshahara (FEDHA YA FAMILIA YAKO) katika usafiri bali unatumia fedha yangu mimi na huyu anayesoma hii thread na mwanakijiji mwingine kule kijijini kupitia makato ya kodi zetu katika mishahara na pale tunapokwenda kununua bidhaa (VAT). Hivo kwako wewe hili haliwezi kuwa ongezeko kubwa la nauli, lakini kwangu mimi na huyu mtu anayesoma hii thread na yule mwanakijiji kule kwetu busega ni ongezeko KUBWA SANA LA NAULI (tafakari sana).

Nasema niongezeko kubwa sana la nauli kwa sababu zifuatazo:

1. Mimi na familia yangu tupo watu wazima 4 (wanne) na wanafunzi 2 (wawili) ambao kila siku za kazi inatulazimu kupanda dala dala kwenda na kurudi kazini na shuleni. Hivyo kila mmoja wetu sisi watu wazima wanne atapaswa kuacha barabarani tsh 800/= kwa siku. Na kwa sababu tupo wanne tunajikuta tunaacha barabarani tsh 3,200/= kwa siku. wanafunzi wapo wawili nao wanatumia 200/= kila mmoja kwenda shuleni hivo ni tsh 400/= kwa mwanafunzi mmoja kwenda na kurudi, na kwakua nao ni wawili wanajikuta wanaacha barabarani tsh 800/= kwa siku moja.

na sasa jumla ya fedha tunazoziacha barabarani sisi wa familia yangu ni 3,200/= + 800/= = 4, 000/= kwa siku.
na kwa juma moja tunaacha barabarani tsh 4,000/= x siku 5 za kazi (bado misele mingine ya maisha) = 20,000/=
na kwa mwezi mzima tunatumia tsh 20,000/= x majuma 4 = 80,000/= kama nauli.
Kumbuka hapo hakuna hesabu yoyote ya chakula kazini (najua wewe una chai/lanchi ofisini kwa kodi zetu)

2. Mheshimiwa mwakyembe hapo sijawazungumzia wanakijiji wa kule nyumbani kwetu busega ambao hujawapalulia hata barabara yao ya kutoka nyashimo kwenda bariadi, ambao naamini sasa na wenyewe kufikia kesho watapandisha bei ya mahindi kwa kuwa barabara yao hujaipalua na nauli ya kusafirishia (uchukuzi) wa mazao yao umeipandisha wewe ukishirikiana na sumatra. Na kama kweli wakipandisha naamini utazidi kuiweka familia yangu ya watu 6 katika hali mbaya sana ya kukaribia kumpigia hodi MUNGU kwa kuwa tutakuwa hatuna tena uwezo wa kununua mazao kutoka kijijini busega.

3. Katika ongezeko hilo "DOGO" la nauli sijasikia kutoka kwa mtu yeyote au popote likitajwa ongezeko jingine "DOGO" la mishahara kwa wafanyakazi wa serikalini au walio katika sekta binafsi.

4. Mheshimiwa mwakyembe, yaani mimi na watu wa familia yangu tunakuoneni wewe na mawaziri wenzako wote (sitaki kumtaja mheshimiwa RAIS kwa sababu yeye siyo waziri) katika baraza la mawaziri kama wachekeshaji fulani hivi (comedians) ambao uwezo wenu wa kufikiri umegota mahara fulani (mkapa aliposema kuwa watu ni wavivu wa kufikiri watu walimkejeli sana na kumbeza, lakini alikuwa sahihi sana) hivi mheshimiwa inaingiaje akilini kupandisha nauli za magari kwa ongezeko "DOGO" pasipo na ongezeko hata "DOGO" la mishahara? sijasikia popote kama mafuta yamepanda ki-hivo, Je mafuta yakipanda ki-hivo hiyo nauli unafikiria ita-shoot hadi wapi??

5. Mheshimiwa mwakyembe, yaani mimi na watu wa familia yangu tunakuoneni wewe na mawairi wenzako (simtaji mheshimiwa RAIS kwa sababu maalumu) kama dereva anayejaribu kuovateki katika daraja la mto wami bila kuangalia mbele na wakati huo huo kuna tenka la prime fuel likija mbele yake kwa kasi kubwa sana, hivi mnategemea nini kitatokea hapo???

6. Mheshimiwa mwakyembe, nina mambo mengi sana ya kukuambia wewe ukiwa kama waziri mwenye dhamana ya uchukuzi nchini, lakini nimekushangaa pia unapowashutumu watanzania kwamba hawaji kwenye vikao, eti unasema, "................., tatizo langu ni tabia yetu ya Watanzania wengi kukacha vikao halali vinavyojadili mambo yanayotuhusu na kuja kulalamika baadaye." Hivi nikuulize dr wangu mwakyembe, hivi inawezekana kweli watanzania wote tukaweza na kufanikiwa kuja kujadili katika vikao??? sasa kama unataka wote tuje ktk vikao nini maana ya uwakiishi, lakini pia hata tukiweza kuja kitakachotokea ni majadiliano na kuchukua maoni (kumbuka maoni huweza kukubaliwa au kukataliwa) na mwisho wa siku watu wachache ndo wanaaopashwa kutoa maamuzi ya majadiliano husika, na watu hao wachache wenye maamuzi ni wewe mheshimiwa mwakyembe, sumatra na baraza lenu la mawaziri, hivo hata kama tulijadili kwa pamoja lakini mkiamua kutupiga nyundo ya kichwa mnatupiga tu maana waamuzi wa mwisho ni ninyi.

7. Mheshimiwa mwakyembe, najisikia kulia kila nikilitaja jina lako kwa kuwa ulipoteuliwa kuwa waziri wa uchukuzi nilijenga imani kubwa sana kwako ambayo naona sasa inaanza kuporomoshwa na jambo kama hili. niliamini sasa RAIS anaanza kujenga timu ya wapiganaji (kosa lake naye - RAIS ni kumuondoa mheshimiwa samweli sitta (mr speed and standards katika usipika) wazuri wakiwemo pia John Pombekali Magufuli, Agray MwanRY, prof Tibaijuka na pengine angetuchanganyia (kama katiba ingekuwa inaruhusu na watu wa upinzani wachache......!!) kumbe nilikuwa naota ndoto za mchana.

8. Mheshimiwa mwakyembe, nisikuchoshe na maandiko marefu (pengine ni ya kipuuzi) kwa kuwa najua na ninaamini unamajukumu mengi sana ya kulifanyia taifa hili (kuliko upuuzi huu), lakini pia nikuambie tu kuwa, nimekuandikia na kukutaja sana wewe hapa kama SYMBOL ya viongozi wote katika maeneo yao ya kazi na dhamana tuliyowapatia watimize majukumu yao kwa kuangalia hali halisiya mtanzania wa kiwango cha chini kabisa cha maisha.
Sitaki niamini kwamba wewe mheshimiwa mwakyembe na mawaziri wote mlizaliwa mjini (hususani jijini dar es salaama) kiasi kwamba mnataka kutuambia kwamba hamuyafahamu maisha HALISI ya mtu wa kijijini. Naamini kwamba mmezaliwa na kuishi kijijini kwa viwango tofauti vya maisha (japo hamkukulia kijijini.

Sasa kwa nini leo mnakuwa wasaliti wa ndugu zenu, baba, mama, kaka, dada, wajomba, shangazi zenu walioko vijijini?
Kitu gani haswa ambacho ninyi hamkifahamu kuhusu maisha ya kijijini?
Hivi ni nani aliyeWAROGA hata mkaamua kusahau maisha na mazingira ambamo mmezaliwa?
Kumbukeni pale mlipoaanguka...., mkayaache matendo yenu ya zamani, mkayafanye yale yaliyo mapya.


Napenda kuwasilisha:
Nakala kwa:
1. Dr Harison Mwakyembe waziri wa uchukuzi - kwa kuliangalia kwa upya tena suala hili.

2. Baraza la mawaziri - kwa taarifa.

3. SUMATRA - kwa maamuzi yasiyozingatia uhalisia wa maisha ya watanzania.

4. Vyama vya upinzani - kwa kujiandaa kukabidhiwa nchi na CCM (kama itaendelea hivi)
 
Ongezeko dogo linatuumiza wadogo

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hayo ni maneno ya mwenye shibe hamjui mwenye njaa.

Watu wa namna hii wangependa kutuona watanzania tukiendelea kukwama kiuchumi na kimaisha kwa ujumla ili wazidi kututawala hadi milele.

Kwa gharama hizi kuna wazazi watashindwa kusomesha watoto wao kwa ongezeko hilo na hata kama wakiweza sio kwa kiwango cha kulizisha, hivyo watoto watapata elimu duni nk, maana yake ni kwamba wao viongozi wa juu kwa vile wana uwezo huo kwao sio shida.

Tulipo sio pazuri hata kidogo.
 
Huyu na Magufuli ndo majembe ya Maccm!! Magufuli alipandisha nauli kwa raia wa Kigamboni tena kwa kejeli za hali ya kutisha!! Hawatufai!

Makonda wa daladala huwa wanawasilisha pesa ya tajiri kabla ya saa nane mchana na wao kuendelea na shughuli zao. Leo Mwakyembe kabla hata ya kusubiria bajeti ipite wanakuja na ongezeko la nauli na kuiita dogo saaaana!! hawatufai!!
 
Mi naona mwendo huu ni mzuri ili wananchi waweze kujitambua na kuweza kufanya maamuzi magumu 2015
 
Back
Top Bottom