DR.EMMANUEL JOHN NCHIMBI ACHIA NGAZI
Siku zote mtu anayesema ukweli huchukiwa na watu wengi hata pengine kutafutiwa namna ya kuuawa, mfano, nabii Yeremia katika kitabu chake sura ya kwanza kwenye utangulizi anathibitisha haya kwakuwambia wayahudi kwamba; Wafalme,makuhani na manabii wa uongo hawakutumwa na Mungu kuja kuitawala Israel isipokuwa yeye lakini ukweli huu wayahudi waliupinga na kutafuta namna ya kumuua ili kupotosha ukweli.
Lakini ujumbe wake bado ulikuwa motomoto, nabii Yeremia aliwambia wayahudi kuwa Duniani wanadamu wanapenda uongo kuliko ukweli, lakini pia nabii Yeremia anakumbukwa sana kuhusu maneno yake juu ya Agano jipya (31:31-34)ambayo yanatumika katika sehemu ya pili ya Biblia, yaani Agano jipya ambalo lamhusu Yesu Kristo mpatanishi wa Mungu na binadamu (Waebrania 8:8-12).
Lakini bado Yesu kristo alipozaliwa na kuwambia Wayahudi kuwa yeye ndie mwana wa Mungu hawakuamini na hatimaye wakamsulubu msalabani mpaka kufa hii nayo inathibitisha kuwa siku zote mwanadamu anapenda uongo na unafiki kuliko ukweli.
Ndugu wasomaji wa makala hii mtakumbuka siku chache zilizopita kumekuwa na majibizano makali kati ya viongozi wa umoja wa vijana ccm Taifa na kada aitwaye James Rock Mwakibinga kuhusu ufisadi wa Mali za jumuiya hiyo kabla ya kutoa mawazo yangu juu ya mvatano huu yanipasa nijiulize maswali kadhaa kama ifuatavyo;
1, Je ni kweli waliyofukuzwa waliuza viwanja vya huko Iringa bila mwenyekiti wa Baraza la wadhamini kujua?
2, Na kama mwenyekiti wa baraza la wadhamini hakujua ni nani aliyeandika barua ya baraza la wadhamini kuidhinisha mali hizo kuuzwa kama taratibu zinavyoelekeza? Je ni nani aliyesaini hati ya uuzwaji wa viwanja hivyo kwa niaba ya baraza la wadhamini?
3, Na kama mwenyekiti wa baraza la wadhamini hakuhusika hizo nyaraka za kuhizinisha uuzwaji zilitoka wapi na ni nani aliyewasiliana na viongozi wa Ardhi kudhibitisha kuwa baraza la wadhamini limeridhia matumizi ya viwanja hivyo yabadilishwe kama taratibu za ardhi zinavyoelekeza?
4, Na kama mwenyekiti wa baraza la wadhamini alisaini na kuandika barua itakuaje mwenyekiti wa UVCCM Taifa asijue?
Ndugu msomaji wangu utakubaliana na mimi kama una akili timamu, haiwezekani wizi wa Mali za jumuiya ufanyike kwa miaka kadhaa halafu mwenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa asijue, na mwenyekiti wa Baraza la wadhamini asijue na hata kama hawakujua hii inatosha kuwafukuza kazi na kuwavua nyazifa zao maana hawako makini na walishindwa kuwajibika.
Na haiingii akilini kikao cha tarehe 13August 2016 kufukuza watu wa chini na kuacha vigogo ambao mimi nina amini ndio walioshawishi viwanja hivi kuuzwa.
Mimi binafsi huwezi kunishawishi kuwa Dr.Emmanuel Nchimbi, kama mwenyekiti wa baraza la wadhamini hakuhusika, siamini kama mwenyekiti wa jumuiya Taifa mh,Sadifa Juma hakuhusika na huwezi kunishawishi kuwa Katibu mkuu ndugu Sixtus Mapunda aliiba nyaraka bila viongozi wengine kujua, je ni kweli aliiba na barua ya mwenyekiti wa baraza la wadhamini ili kuidhinisha uuzwaji? Je aliweza kufoji saini ya mwenyekiti wa baraza la wadhamini? na kama alifoji mbona Kikao hakikuliongelea hili?
Mimi ningekuwa mwenyekiti wa baraza la wadhamini ningeachia ngazi nisingesubiri kuaibishwa kiasi hichi.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ukiona Chama cha siasa kina jumuiya ya vijana regelege ujue ni hatari kwa maendeleo ya chama hicho, ni kweli jumuiya ya umoja wa vijana ngazi ya Taifa na jumuiya ya UWT tangu mwaka 2012 zimepoteza mvuto, na badala ya kutumikia chama cha Mapinduzi zimekuwa zikitumikia watu wenye pesa na watu wenye majina makubwa na ndo maana UVCCM Taifa wanashinwa kuwachukulia hatu watu wanaotuhumiwa
Ombi langu kwa viongozi wangu watiifu wa Chama cha Mapinduzi Taifa fanyeni uchunguzi wa kina katika jumuiya hii wanachama wengi wanailalamikia sana kwa ufisadi na kujilimbikizia Mali maana wao kwa wao wanaogopana.
Mwisho ushauri wangu kwa vijana wenzangu,ni kwamba vijana ni jeuri ya chama tusiwe waoga kuwataja mafisadi ndani ya chama Chetu kwakuofia kukosa nafasi za uteuzi, huu ni muda muafaka wa kukemea maovu yote yaliomo ndani ya chama hiki tusipofanya hivyo tutakuja kujuta baadae maana sasa ndo tumempata mwenyekiti mahiri na mtetezi wa wanyonge mh,Dr.John Pombe Magufuli hakika tumsaidie jukumu hili.
Namalizia kwakunukuu ahadi za mwanachama wa Chama cha Mapinduzi ahadi namba tano inasema"Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu" mwisho wa kunukuu.
Imeandaliwa na wenu
Comrade,
Mwita Nyarukururu
mwitanyarukururu@gmail.com.