Pagan Amum
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 1,932
- 4,400
Nahisi sasa ni wazi masaa na dakika za Dr. Dau (Mkurugenzi mstaafu wa NSSF) kukaa uraiani zinahesabika, baada ya habari zinazotalawa za ubadilifu wake.
Nimesikia jana Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kumhoji "kumfanyia interogation" kwa zaidi ya masaa 4 tokana na ubadhirifu wa zaidi ya Billion 179 uliofanyika chini yake akiwa ni DG wa NSSF..
NB: Asante Rais Magufuli kwa kuamua kupambana na mafisadi na majizi, waliotuibia kwa zaidi ya miaka 10.
=====
MODERATOR:
Taarifa hii si ya kweli
Nimesikia jana Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kumhoji "kumfanyia interogation" kwa zaidi ya masaa 4 tokana na ubadhirifu wa zaidi ya Billion 179 uliofanyika chini yake akiwa ni DG wa NSSF..
NB: Asante Rais Magufuli kwa kuamua kupambana na mafisadi na majizi, waliotuibia kwa zaidi ya miaka 10.
Hatimaye DK. Ramadhan Dau, aliyekuwa mkurugenzi wa Shirila la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
Dk. Dau anatuhumiwa kuingiza NSSF hasara ya mabilioni ya shilingi, kutokana mikataba ya kinyonyaji. Amekuwa katika shirika hilo kwa miaka 15.
Taarifa kutoka serikalini na taasisi nyingine zinazoshughulikia uchunguzi zinasema, Dk. Dau ambaye aliong’olewa NSSF 15 Februari mwaka huu, atafikishwa kwa mahakamani, kujibu tuhuma za ufisadi zilizoibuliwa ndani ya shirika hilo.
Tuhuma nyingine ni matumizi mabaya ya madaraka, uzembe na ukiukwaji wa taratibu katika miradi ya uwekezaji na vitega uchumi mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Miongoni mwa miradi hiyo, ni ujenzi wa daraja la Kigamboni; hoteli ya kitalii jijini Mwanza, mradi wa ujenzi wa majengo katika mji mpya wa Kigamboni, uwekezaji kwenye jengo la biashara la Mzizima na mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya.
Wakati huo huo kuna taarifa kuwa wakurugenzi wakuu wa NSSF akiwemo Magori nao wamehojiwa na TAKUKURU kutokana na tuhuma za ubadhirifu na rushwa.
Magori ambaye ni Director wa Operations anatuhumiwa kuwa alipokea mabilioni toka kwa makampuni ya madini huko Geita wakati Eunice anatuhumiwa kupokea pesa toka makampuni lukuki ya matangazo, pia sakata la staff uniforms na kahusishwa na kampuni ya MARIEDO BOUTIQUE.
Eunice pia anatuhumiwa kupokea rushwa kwa ajili ya kufanikisha kuwapatia kazi watu walioomba kazi NSSF.
Stay tuned, kesho Alhamis gazeti la MSETO linaanika kila
kitu.
Source: Mwanahalisi
=====
MODERATOR:
Taarifa hii si ya kweli