DPP aombwa kuingilia kati baba wa mtoto ajulikane

DPP aombwa kuingilia kati baba wa mtoto ajulikane

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
Moshi. Mama mzazi wa mwanafunzi wa kidato cha nne aliyepewa ujauzito, amemuomba Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), aagize kufanyike vipimo vya Vinasaba (DNA) kubaini baba wa mtoto.

Mzazi huyo, Saadia Ramadhan ambaye ni mkazi wa Chekereni Wilaya ya Moshi, alitoa ombi hilo jana baada ya Mahakama kumuachia mtuhumiwa kwa kukosekana ushahidi wa kibiolojia.

Mtuhumiwa katika kesi hiyo namba 506 ya 2016, Mrisho Mkwama aliachiwa huru Julai 21 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Moshi, Pamela Meena baada ya kukosekana kwa ushahidi huo.

Hakimu Meena alisema mwanafunzi huyo alipopimwa Julai 27 alibainika kuwa na ujauzito wa miezi mitano, lakini swali ni nani aliyempa ujauzito huo.

“Kujibu swali hilo la vipimo vya kibaiolojia (DNA) ni muhimu ili kuthibitisha baba wa mtoto. Sielewi kwa nini upande wa mashtaka haukufanya hivyo.

“Tuhuma hizi kwa kiasi kikubwa zinahitaji ushahidi wa kibaiolojia kuliko ushahidi wa kawaida wa shahidi. Daktari amethibitisha ni mjamzito lakini hakusema nani ni mhusika,” alisisitiza.

“Sasa hivi huyu mjukuu ana umri wa miezi tisa na wakati kesi inasikilizwa tayari mtoto alikuwa ameshazaliwa. Kwa nini upande wa mashtaka haukuomba vifanyike vipimo vya DNA?”Alihoji.

Kutokana na hukumu hiyo, mzazi wa mtoto huyo ameiomba ofisi ya DPP kuingilia kati kwa kuwa wakati kesi inaendelea, mtoto wake alikuwa tayari amejifungua.

Katika utetezi wake alioutoa Juni 23 mwaka huu, mtuhumiwa alikanusha akisema anashangaa kutajwa wakati hamfahamu huyo mwanafunzi na wanaishi vijiji tofauti.

Alisema hajawahi kukutana na mwanafunzi huyo na wala kuwa na uhusiano naye.

Hata hivyo, katika ushahidi wake, mwanafunzi huyo alidai mtuhumiwa alianza kuomba awe na uhusiano naye tangu mwaka 2015 lakini alikataa hadi Machi 2016 alimlazimisha wakutane kimwili.

Alidai mtuhumiwa alimpa Sh2,000 na kuondoka zake na hakuweza kumwambia mtu yeyote kwa madai kuwa mshtakiwa alimtisha.

Chanzo: Mwananchi
 
Nadhani sasa kipimo cha DNA kinatakiwa kuwepo kila mkoa, ili iwe rahisi kung'amua vitu kama hivi
 
Back
Top Bottom