Doyo: kwanini sijajiunga na CHADEMA.

dandabo

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
303
176
Niko Handeni, Tanga na ADC wana mkutano wao hapa. Doyo anasema baada ya kuondoka cuf hakujiunga na cdm au nccr kwasababu vyama vyote hivyo vina tabia zinazofanana na cuf. Anasema cuf iliwatimua wao, nccr ikawatimua akina Kafulila na Cdm ikawatimua madiwani 5 Arusha. Anasema kwa tabia yake yakutovumilia ubabe ndani ya vyama basi hata huko watamtimua. Anasema ametimuliwa cuf baada ya kuhoji matumizi ya chama wakati wa kampeni huko igunga. Anasema igunga alikabidhiwa kata mbili kuongoza kampeni na kutumia jumla ya sh l milion 6 tu. Kwa kata zote za igunga walitumia tshs milion 80, lkn taarifa za vikaoni zikaonyesha matumizi ya tshs mil mia tatu! Alipohoji ikawa sababu ya kutimuliwa
 
ana mkosi

Niko Handeni, Tanga na ADC
wana mkutano wao hapa. Doyo anasema baada ya kuondoka cuf hakujiunga na
cdm au nccr kwasababu vyama vyote hivyo vina tabia zinazofanana na cuf.
Anasema cuf iliwatimua wao, nccr ikawatimua akina Kafulila na Cdm
ikawatimua madiwani 5 Arusha. Anasema kwa tabia yake yakutovumilia
ubabe ndani ya vyama basi hata huko watamtimua. Anasema ametimuliwa cuf
baada ya kuhoji matumizi ya chama wakati wa kampeni huko igunga.
Anasema igunga alikabidhiwa kata mbili kuongoza kampeni na kutumia jumla
ya sh l milion 6 tu. Kwa kata zote za igunga walitumia tshs milion 80,
lkn taarifa za vikaoni zikaonyesha matumizi ya tshs mil mia tatu!
Alipohoji ikawa sababu ya kutimuliwa
 
Lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola, hivi anategemea hiyo ADC itafikia hatua ya kuenea nchi nzima na kuchukua dola lini?
 
Huyu Doyo kila siku yeye malalamiko ya Igunga kaishaama CUF saizi nae ana chama chake kinachotakiwa ajikite kwenye chama chake cha ADC au anatafuta huruma.
 
Na mchango wako pale cuf ulikuwa nini au utakumbukwa kwa kitu gani cuf tofauti na kuhoji matumizi au wewe ndiye auditor wa chama?
 
ADC, CUF, NRA, UPDP, Jahazi Asilia, SAU, n.k. pamoja na CCM vina mfanano fulani katika siasa za nchi yetu.
 
Yawezekana ajui utaratibu wa kuhoji....haiwezekani mtu alete chokochoko akaachwa kwenye chama...Asiyekubali kuongozwa kamwe si kiongozi mzuri.....
 
Waliotimuliwa kila moja alitimuliwa kwa sababu zake.
Kama akili yake iko hivyo alitakiwa atimuliwe mapema sana.
 
Vizuri ajihusishe na kuendeleza chama chake kipya. Hata kama amekosewa ajufunze kuchora mstari na then asonge mbele ktk siasa
 
Doyo ndo nani kwanza? Eti na yy anajiona ni public figure! Kwanza anaonekana ni mtu wa taarabu 2´
gosh... Shame on him potty guy.

Shardcole.
 
Nini sera ya ADC? ni kulalamikia vyama vingine?ni kuhoji matumizi ya fedha za kampeni?
 
Huyu Doyo kila siku yeye malalamiko ya Igunga kaishaama CUF saizi nae ana chama chake kinachotakiwa ajikite kwenye chama chake cha ADC au anatafuta huruma.

wewe mbona ni gamba lakini kutwa kucha unalia lia na cdm?
 
Back
Top Bottom